#COVID19 Ukiniambia kwanini napinga ripoti ya Tume ya CORONA, majibu yangu ni mepesi kabisa

#COVID19 Ukiniambia kwanini napinga ripoti ya Tume ya CORONA, majibu yangu ni mepesi kabisa

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Walioleta hii ripoti ni wenye elimu kubwakubwa (Maprofesa, PhDs', Masters, Degrees) na wengineo wamo humo na inawezekana "La saba pia wamehusika kwa namna moja au nyingine, inawezekana kabisa dereva aliyewapeleka Ikulu ni Form Four Failure, ana leseni yake ya NIT akapata CONNECTION yuko pale anaendesha gari ya PhD holder pale.

Inawezekana kabisa aliyebadili tairi njiani ni mshikaji tu akiyeishia "La saba", huyo ndo kanusuru maisha yao kwa kuwabadilishia tairi lililochoka na kuweka jipya. Na akalipwa kiasi fulani cha fedha. Mlipaji huyu ni serikali kupitia kwa PhD holder anaepelekwa field kupata majibu ya maswali yake kujenga hoja kwenye tume ya Corona.

Kinachonishangaza ni kuona Elimu zetu hazitusaidii, tangu siku ya kwanza ilipotangazwa kuanzishwa Tume ya Corona, niliuliza maswali yafuatayo:-

1: Tume inaweza kuja na mapendekezo tofauti na Yale ya WHO?
2. TUME hii itakuja na majibu yasiyoacha shaka kwa Wananchi?
3: Tume hii itakiri kuwa CORONA nchini haipo?
4: Tume hii itaonesha athari halisi zilizopo mitaani bila kuacha shaka?
5: Tume hii itakubali kukosolewa?

Baada ya kitambo kidogo, majibu yametoka, maswali yangu yote yamejibiwa.
1: Tume haijavuka mapendekezo ya WHO hata moja, hakuna pendekezo la tume linalopingana na WHO, wamefanya ku_copy na ku_paste kila kitu. Sijaona dira yetu kama taifa ni ipi kuhakikisha tunaishi kulingana na Uhuru wetu kama taifa.

2: Tume imekuja na majibu yenye mashaka kwa wananchi, hakuna mtu asiye na shaka ma majibu ya tume kuanzia kwenye VITABU hivyo vikubwa 6.

3: Tume haijakubali kuwa CORONA ipo au haipo isipokuwa inazungumzia ujio wa WIMBI la 3 ambalo ni hatari zaidi, yaani TUME imefanyia kazi "HEAR SAYING" , kwamba na yenyewe inakubaliana na utabiri bila yenyewe kufanya ujasusi kujua iwapo ni taarifa za kweli ama si za kweli.

4; TUME imeshindwa kutupatia majibu sahihi kwamba hii chanjo tutakayochanjwa ilitengenezwa maalumu kwa ajili ya Kinga ya mlipuko upi? Maana hadi sasa tuko katika wimbi la PILI, chanjo hii ilikuwa maalumu kwa kundi la mlipuko upi, moja Kati ya ile miwili au kwa utakaokuja huo wa 3... Tume imefeli hapo katika kuainisha aina ya mlipuko na chanjo tunayoipokea ni kwa ajili ya mlipuko upi na ilitengenezwa maalumu kwa mlipuko upi.

5. Tume imeshindwa kutuelezea mafanikio ya chanjo zote hizo ni nchi zipi zimefanikiwa kuzuia maambukizi mapya baada ya kupatiwa chanjo hizo.

6: Tume imeshindwa kukubali au kukataa kuhusu athari za vifo vitokanavyo na chanjo hizi ikiwa tutadhurika na chanjo hizi, isipokuwa Tume imeihakikishia serikali kuwa ni chanjo salama na zenye ufanisi. Lakini muda huohuo inazitaja chanjo zote kuwa ni fanisi, muda huohuo inapata kigugumizi kuitaja chanjo ambayo wao wamejiridhisha nayo kuwa ni nzuri na salama.

7: Tume imeshindwa kutuambia katika mataifa ambayo viliripotiwa vifo vitokanavyo na watj kuchanjwa hizi chanjo zilitokana na nini na kwanini wao kama time wahisi hii chanjo itakuwa salama zaidi kwetu kuliko huko zilikoua wananchi wa mataifa mengine.

Ni kweli kabisa mimi sina elimu kubwa kama ya hawa MAPROFESA, ila ninaamini kuna utofauti mkubwa sana kati ya ELIMU na AKILI.

UTOFAUTI WAKE UPO HIVI: Akili ni kile kinachobakia baada ya kuondoa yote uliyofundishwa darasani.

Kwa mujibu wa mwanafalsafa wa zamani kidogo, Robert Einstein kwamba kuna watu wakiondoa yale waliyofundishwa darasani, vichwa vyao vinabaki vitupu. Kitu pekee walichojaza kichwani ni yale waliyofundishwa darasani. Hawa ndio hujisifia vyeti, au idadi ya "digrii" walizonazo. Hawana akili, japo wana elimu.

Einstein alisema hakuna uhusiano kati ya elimu na akili. Kuna watu wana elimu lakini hawana akili, na wengine wana akili lakini hawana elimu. Ni bora uwe na akili ukose elimu, kuliko uwe na elimu ukose akili.

Kaka yangu Malisa GJ aliwahi kusema kwamba Icons wa Sayansi kama Isaac Newton, Galileo Galilei na Archimedes of Syracuse hawakuwa na elimu yoyote ya cheti, diploma wala degree, lakini walikua na AKILI. Ugunduzi wao mpaka leo unaiongoza dunia.

Akili siku zote ni "superior" kuliko elimu kwa sababu akili ndio ilibuni elimu. Yani watu wenye akili walikaa wakakubaliana waanzishe utaratibu ambao utamuwezesha mtu kukaa darasani na kujifunza kwa kipindi fulani, kisha apimwe kwa mitihani na atunukiwe cheti. Ubunifu huo ulifanywa na wenye akili. Jiulize mtu wa kwanza kutunukiwa degree duniani alifundishwa na nani?

Kwa hiyo niseme tu kwamba ambao hatuna hizi PhDs mtuheshimu vilevile kwa maana tunazo "akili" za kutambua michongo yenu kwa urahisi zaidi kuliko kale kamstari kembamba kanachotenganisha akili nyingi na ukichaa.

C&P
 
IMG_20210520_115011.jpg
 
Kinachoonekana hapo kwenye tume ni kwamba. Wameambiwa wakirudisha majibu basi wawe na majibu yanayopendezewa na mataifa yaliyokubwa na wimbi kubwa la ugonjwa. Baada ya mkuu kufunga barakoa kwenye kila kona alipotokea basi ni kithibitisho kuwa lazima majibu ya korona iwepo.

Ninachojiuliza yale mavitabu makubwa zaidi ya matatu, inamana imebeba mapendekezo 19 pekee?? alafu yote ni yale ambayo hayakupi muda kuyafikiria kwa ukubwa (yan lazima wangeleta majibu yale)
 
Karibu Tanzania.

Nchi ambayo kila "takataka" ina utaalamu wa kila kitu.

No wonder.

Tanzania hakuna mtu mwenye uhakika na Afya yake na hajui cha kufanya.

1- Akitokea babu wa Loliondo watu wote huko huko

2- Akitokea mganga maarufu kutoka Nigeria watu wote huko

3- Akitokea sheikh anasoma Dua watu wote huko

4- Akitokea "Mwamposa" watu wote wanaenda huko kukanyaga mafuta na kufa huko huko

5- Akitokea Nabii TB Joshua anaombea watu, watu wote huko

6- Akitokea herbalist clinic anajitangaza kwenye TV anaponesha watu, watu wote huko

Watu hawana uhakika wamsikilize nani, kila mtu mjuvi. Wako tayari kuquestion masuala ya kitaalamu yenye ushahidi lakini ndumba au maombi yasiyo na ushahidi hakuna.

No wonder, Watanzania ni watu wa Ajabu.

Jaribu kuuliza wataalamu wa Afya wanaojihusisha na masuala ya clinical outreach na community awareness watakwambia.

Mtanzania hata ukimwelimisha kutumia chandarua utapata tabu sana. Muda wote anajihisi hisi tu kwamba kuna watu wana nia mbaya na wao.

Nenda mikoani huko,

Wajawazito wanashauriwa hudhurieni Clinic mpate chanjo yenye vitamini ya FOLIC ACID hawataki, finally wanazaa watoto wenye ULEMAVU wa vichwa vikubwa halafu wanaanza kusema wamerogwa. Watoto wenye vichwa vikubwa 👇👇

1621525323649.png


Wodini huko ni vichekesho, Mtoto anazaliwa kitovu cha mtoto kinapakwa mavi ya tembo, ukiuliza sababu inafichwa.

Ukifanya CLTS ( Community-Led Total Sanitation ) ili angalau uweke mipango ya kuboresha afya utapata tabu.

Hata takwimu tu utazipata kwa shida, mtaalamu akifika kwenye kaya, akiuliza hapa mkuu wa Kaya yuko wapi anafichwa.

Na akitokeza ukauliza kwa mkuu wa kaya, mna watoto wangapi anaficha, anaona kama unampeleleza sijui uue watoto wake sijui uwapunguze.

Bahati mbaya sana kulikuwa na CONSIPIRACY THEORIST ikulu, kaongeza jeraha kabisa kwenye hali.

Serikali itapata tabu sana kuelimisha watu labda itumie wasanii wa Bongo fleva.

Anyway, ndio nchi yangu. Na sisi ndio watanzania
 
Ukitathmini weledi wa waliounda tume na ukiangalia kilichowasilishwa na hao wenye weledi unagundua kuwa mifumo ya kielimu ina tatizo mahali, ina dumaza ubongo baada ya kuukuza ubongo.
Ripoti za hizi tume huwa zinatumika kama rubber stamp, wajumbe wa tume hupima mwelekeo wa aliyewateua na kupitisha ripoti inapotakiwa.

Kama ingekuwa ni awamu ya tano nisingeshaa kama tume hii hii ingekuja na kusema kwamba malimao, tangawizi na kujifukiza ni bora kuliko chanjo na pia hakuna corona.

Hilo tatizo linaanzia huko huko mashuleni na vyuoni, mtafiti yupo tayari kupika takwimu alizopata na kupindisha uandishi wake ili aendane na mawazo ya supervisor wake amalize shule apate cheti cha Masters au PhD. Mtu kama huyo hata siku moja hawezi kujiamini na hata akienda kazini atafanya madudu yale yale.
 
Ina maana hata nyongeza ya kupiga nyungu hawjatoa hoja yoyote! Duuh, yajayo yanatia kizunguzungu!
 
Hii ni moja ya tume kimeo kuwahi kutokea tz, imeleta majibu ya kinadharia kupita kiasi.

Ili kupambana na corona, mama angeendeleza model ya Magu.

Saizi corona wameanza kuipigia chapuo sana, na itaanza kukaa kwenye akili ya watu tena, kitu ambacho kitaleta hofu na taharuki, ambayo hupelekea kinga ya mwili kushuka, hatimaye watu wataanza kufa kwa presha bure.

Mimi naamini punde watu watakapoanza kuchanjwa, kuna kiasilimia watabinuka tu.

Bora wafuate model ya Magu, hiyo ndiyo 95% effective. Tumeishudia, hakuna cha wimbi wala mtoto wake na wimbi.

Mwanzo mama alikuwa vizuri, ila jakaya anamharibu.
 
Vyovyote iwavyo, tume imewafurahisha chadema,hilo ndio la msingi zaidi hayo mengine hayana haja.

Maana tokea mwanzo walihitaji kiongozi mwenye kuitambua corona kwa kauli na vitendo, ndio huyu mama sasa kupitia tume.
 
Back
Top Bottom