Ndalilo
JF-Expert Member
- Jan 30, 2013
- 3,343
- 7,516
Na tatizo kubwa ni pale kushindwa nje ya box, kusema kwa kadiri tulivyofungiwa.Karibu Tanzania.
Nchi ambayo kila "takataka" ina utaalamu wa kila kitu.
No wonder.
Tanzania hakuna mtu mwenye uhakika na Afya yake na hajui cha kufanya.
1- Akitokea babu wa Loliondo watu wote huko huko
2- Akitokea mganga maarufu kutoka Nigeria watu wote huko
3- Akitokea sheikh anasoma Dua watu wote huko
4- Akitokea "Mwamposa" watu wote wanaenda huko kukanyaga mafuta na kufa huko huko
5- Akitokea Nabii TB Joshua anaombea watu, watu wote huko
6- Akitokea herbalist clinic anajitangaza kwenye TV anaponesha watu, watu wote huko
Watu hawana uhakika wamsikilize nani, kila mtu mjuvi. Wako tayari kuquestion masuala ya kitaalamu yenye ushahidi lakini ndumba au maombi yasiyo na ushahidi hakuna.
No wonder, Watanzania ni watu wa Ajabu.
Jaribu kuuliza wataalamu wa Afya wanaojihusisha na masuala ya clinical outreach na community awareness watakwambia.
Mtanzania hata ukimwelimisha kutumia chandarua utapata tabu sana. Muda wote anajihisi hisi tu kwamba kuna watu wana nia mbaya na wao.
Nenda mikoani huko,
Wajawazito wanashauriwa hudhurieni Clinic mpate chanjo yenye vitamini ya FOLIC ACID hawataki, finally wanazaa watoto wenye ULEMAVU wa vichwa vikubwa halafu wanaanza kusema wamerogwa.
Wodini huko ni vichekesho, Mtoto anazaliwa kitovu cha mtoto kinapakwa mavi ya tembo, ukiuliza sababu inafichwa.
Ukifanya CLTS ( Community-Led Total Sanitation ) ili angalau uweke mipango ya kuboresha afya utapata tabu.
Hata takwimu tu utazipata kwa shida, mtaalamu akifika kwenye kaya, akiuliza hapa mkuu wa Kaya yuko wapi anafichwa.
Na akitokeza ukauliza kwa mkuu wa kaya, mna watoto wangapi anaficha, anaona kama unampeleleza sijui uue watoto wake sijui uwapunguze.
Bahati mbaya sana kulikuwa na CONSIPIRACY THEORIST ikulu, kaongeza jeraha kabisa kwenye hali.
Serikali itapata tabu sana kuelimisha watu labda itumie wasanii wa Bongo fleva.
Anyway, ndio nchi yangu. Na sisi ndio watanzania
Tufanye utafiti wa kila kitu kabla ya kuhukumu kwa elimu inayotufanya kushindwa kusonga mbele. Kama mavi ya tembo hayakumdhulu mtoto, kwanini hayakumdhulu? Kama yalitumika kwenye hiyo jamii, kwanini? Walianzaje? Yana kitu gani zaidi kinachoweza kuwa useful?
Unakimbilia kupinga bila kuchambua