#COVID19 Ukiniambia kwanini napinga ripoti ya Tume ya CORONA, majibu yangu ni mepesi kabisa

#COVID19 Ukiniambia kwanini napinga ripoti ya Tume ya CORONA, majibu yangu ni mepesi kabisa

Hii ni moja ya tume kimeo kuwahi kutokea tz, imeleta majibu ya kinadharia kupita kiasi.

Ili kupambana na corona, mama angeendeleza model ya Magu.

Saizi corona wameanza kuipigia chapuo sana, na itaanza kukaa kwenye akili ya watu tena, kitu ambacho kitaleta hofu na taharuki, ambayo hupelekea kinga ya mwili kushuka, hatimaye watu wataanza kufa kwa presha bure.

Mimi naamini punde watu watakapoanza kuchanjwa, kuna kiasilimia watabinuka tu.

Bora wafuate model ya Magu, hiyo ndiyo 95% effective. Tumeishudia, hakuna cha wimbi wala mtoto wake na wimbi.

Mwanzo mama alikuwa vizuri, ila jakaya anamharibu.
Sukuma gang mtapata tabu sana, ulishasikia ile ya mchawi kafa ghafla kabla hajakabidhi misukule yake kwa mchawi mwingine? Misukule hubaki ikitanga tanga uraiani na kuogopesha watu.
 
Vyovyote iwavyo, tume imewafurahisha chadema,hilo ndio la msingi zaidi hayo mengine hayana haja.

Maana tokea mwanzo walihitaji kiongozi mwenye kuitambua corona kwa kauli na vitendo, ndio huyu mama sasa kupitia tume.
Kama mmelijua hilo basi inabidi sukuma gang mwende mkajinyonge sasa, sioni kazi yenu kwa sasa mana mwendazake kaisha sepa/sepeshwa na corona
 
Kwanini chanjo na sio vidonge?
Pia punguza maneno.. changia kuwaelimisha..
Aisee kwani chanjo ni nani alikwambia ni lazima iwe sindano?

Siku ukizaa mtoto ukampeleka clinic ndio utajua kuna chanjo mpaka za matone "Drops"
 
Hakika hili janga la corona linalazimishwa hapa nchini,wanaoshabikia hatua zinazochukuliwa na mataifa mengine no wazi wanafaidika kwa namna moja ama nyingine.
Bila aibu kamati ile inapendekeza serikali iangalie uwezekano wa kufungia watu(lockdown)
Luku tu imezingua siku tatu tu lakini nchi nzima chali, kumbe watu wengi wananunua LUKU ya buku mbili mpaka tatu kila baada ya siku moja au mbili, sasa wafungie uone njaa itakavyowababua
 
Aisee kwani chanjo ni nani alikwambia ni lazima iwe sindano?

Siku ukizaa mtoto ukampeleka clinic ndio utajua kuna chanjo mpaka za matone "Drops"

Hapana jua swahili.. nifundishe pliziii.
 
Karibu Tanzania.

Nchi ambayo kila "takataka" ina utaalamu wa kila kitu.

No wonder.

Tanzania hakuna mtu mwenye uhakika na Afya yake na hajui cha kufanya.

1- Akitokea babu wa Loliondo watu wote huko huko

2- Akitokea mganga maarufu kutoka Nigeria watu wote huko

3- Akitokea sheikh anasoma Dua watu wote huko

4- Akitokea "Mwamposa" watu wote wanaenda huko kukanyaga mafuta na kufa huko huko

5- Akitokea Nabii TB Joshua anaombea watu, watu wote huko

6- Akitokea herbalist clinic anajitangaza kwenye TV anaponesha watu, watu wote huko

Watu hawana uhakika wamsikilize nani, kila mtu mjuvi. Wako tayari kuquestion masuala ya kitaalamu yenye ushahidi lakini ndumba au maombi yasiyo na ushahidi hakuna.

No wonder, Watanzania ni watu wa Ajabu.

Jaribu kuuliza wataalamu wa Afya wanaojihusisha na masuala ya clinical outreach na community awareness watakwambia.

Mtanzania hata ukimwelimisha kutumia chandarua utapata tabu sana. Muda wote anajihisi hisi tu kwamba kuna watu wana nia mbaya na wao.

Nenda mikoani huko,

Wajawazito wanashauriwa hudhurieni Clinic mpate chanjo yenye vitamini ya FOLIC ACID hawataki, finally wanazaa watoto wenye ULEMAVU wa vichwa vikubwa halafu wanaanza kusema wamerogwa. Watoto wenye vichwa vikubwa [emoji116][emoji116]

View attachment 1791926

Wodini huko ni vichekesho, Mtoto anazaliwa kitovu cha mtoto kinapakwa mavi ya tembo, ukiuliza sababu inafichwa.

Ukifanya CLTS ( Community-Led Total Sanitation ) ili angalau uweke mipango ya kuboresha afya utapata tabu.

Hata takwimu tu utazipata kwa shida, mtaalamu akifika kwenye kaya, akiuliza hapa mkuu wa Kaya yuko wapi anafichwa.

Na akitokeza ukauliza kwa mkuu wa kaya, mna watoto wangapi anaficha, anaona kama unampeleleza sijui uue watoto wake sijui uwapunguze.

Bahati mbaya sana kulikuwa na CONSIPIRACY THEORIST ikulu, kaongeza jeraha kabisa kwenye hali.

Serikali itapata tabu sana kuelimisha watu labda itumie wasanii wa Bongo fleva.

Anyway, ndio nchi yangu. Na sisi ndio watanzania
Nimekuelewa vyema mkuu
 
Supreme Court has canceled universal vaccination

In the United States, the Supreme Court has canceled universal vaccination. Bill Gates, US Chief Infectious Disease Specialist Fauci, and Big Pharma have lost a lawsuit in the US Supreme Court, failing to prove that all of their vaccines over the past 32 years have been safe for the health of citizens! The lawsuit was filed by a group of scientists led by Senator Kennedy.

Robert F. Kennedy Jr .: “The new COVID vaccine should be avoided at all costs.

I urgently draw your attention to important issues related to the next vaccination against Covid-19.

For the first time in the history of vaccination, the so-called mRNA vaccines of the latest generation directly interfere with the patient's genetic material and therefore alter the individual genetic material, which is genetic manipulation, which was already prohibited and was previously considered a crime.
The coronavirus VACCINE IS NOT A VACCINE! ATTENTION!
What has always been a vaccine?
It was always the pathogen itself - a microbe or virus that was killed or attenuated, that is, weakened - and it was introduced into the body in order to produce antibodies.
Not even a coronavirus vaccine!
She's not that at all!
It is part of the newest group of mRNA (mRNA) allegedly "vaccines"
Once inside a human cell, mRNA reprograms normal RNA / DNA, which begins to make another protein.
That is, nothing to do with traditional vaccines! That is, it is an instrument of genetic influence. Gene weapon! That is, they were going to destroy from earthlings, and the survivors will become GMOs!
Following the unprecedented mRNA vaccine, the vaccinated will no longer be able to treat the symptoms of the vaccine in an additional way.
Vaccinated people will have to come to terms with the consequences, because they can no longer be cured by simply removing toxins from the human body, as in a person with a genetic defect such as Down syndrome, Klinefelter syndrome, Turner syndrome, genetic heart failure, hemophilia, cystic fibrosis, Rett syndrome, etc. ), because the genetic defect is forever!

This clearly means:
if a symptom of vaccination develops after mRNA vaccination, neither I nor any other therapist can help you, because
DAMAGE CAUSED BY VACCINATION WILL BE GENETICALLY Irreversible.

❗Workman library rightly observe that according to professor mike Yeedon Vaccination is a weapons of genocide of the 21st century.

Former Pfizer Chief Scientist Mike Yeedon has once again expressed his position that it is too late now to save those who have been injected with a substance publicly called "the Covid-19 vaccine."

He encourages those who have not yet received the lethal injection to fight for their lives, those around them and the lives of their children.

The internationally renowned immunologist goes on to describe a process that he says will kill the vast majority of people:
"Immediately after the first vaccination, about 0.8% of people die within two weeks.
The average life expectancy of survivors will be a maximum of two years, but it also decreases with each new "injection". "

Additional vaccines are still being developed to cause deterioration in certain organs, including the heart, lungs and brain.

After two decades at Pfizer, Professor Yedon was familiar with the functions and research and development goals of pharmaceutical giant Pfizer, and states that the ultimate goal of the current "vaccination" regime can only be a massive demographic event that will make all world wars put together, like Mickey's staging Mouse.

"Billions of people have already been sentenced to certain, inevitable and painful death. Anyone who receives the injection will die prematurely, and three years is a generous estimate of how long they can survive."

Posted to Workman Library
 
Walioleta hii ripoti ni wenye elimu kubwakubwa (Maprofesa, PhDs', Masters, Degrees) na wengineo wamo humo na inawezekana "La saba pia wamehusika kwa namna moja au nyingine, inawezekana kabisa dereva aliyewapeleka Ikulu ni Form Four Failure, ana leseni yake ya NIT akapata CONNECTION yuko pale anaendesha gari ya PhD holder pale.

Inawezekana kabisa aliyebadili tairi njiani ni mshikaji tu akiyeishia "La saba", huyo ndo kanusuru maisha yao kwa kuwabadilishia tairi lililochoka na kuweka jipya. Na akalipwa kiasi fulani cha fedha. Mlipaji huyu ni serikali kupitia kwa PhD holder anaepelekwa field kupata majibu ya maswali yake kujenga hoja kwenye tume ya Corona.

Kinachonishangaza ni kuona Elimu zetu hazitusaidii, tangu siku ya kwanza ilipotangazwa kuanzishwa Tume ya Corona, niliuliza maswali yafuatayo:-

1: Tume inaweza kuja na mapendekezo tofauti na Yale ya WHO?
2. TUME hii itakuja na majibu yasiyoacha shaka kwa Wananchi?
3: Tume hii itakiri kuwa CORONA nchini haipo?
4: Tume hii itaonesha athari halisi zilizopo mitaani bila kuacha shaka?
5: Tume hii itakubali kukosolewa?

Baada ya kitambo kidogo, majibu yametoka, maswali yangu yote yamejibiwa.
1: Tume haijavuka mapendekezo ya WHO hata moja, hakuna pendekezo la tume linalopingana na WHO, wamefanya ku_copy na ku_paste kila kitu. Sijaona dira yetu kama taifa ni ipi kuhakikisha tunaishi kulingana na Uhuru wetu kama taifa.

2: Tume imekuja na majibu yenye mashaka kwa wananchi, hakuna mtu asiye na shaka ma majibu ya tume kuanzia kwenye VITABU hivyo vikubwa 6.

3: Tume haijakubali kuwa CORONA ipo au haipo isipokuwa inazungumzia ujio wa WIMBI la 3 ambalo ni hatari zaidi, yaani TUME imefanyia kazi "HEAR SAYING" , kwamba na yenyewe inakubaliana na utabiri bila yenyewe kufanya ujasusi kujua iwapo ni taarifa za kweli ama si za kweli.

4; TUME imeshindwa kutupatia majibu sahihi kwamba hii chanjo tutakayochanjwa ilitengenezwa maalumu kwa ajili ya Kinga ya mlipuko upi? Maana hadi sasa tuko katika wimbi la PILI, chanjo hii ilikuwa maalumu kwa kundi la mlipuko upi, moja Kati ya ile miwili au kwa utakaokuja huo wa 3... Tume imefeli hapo katika kuainisha aina ya mlipuko na chanjo tunayoipokea ni kwa ajili ya mlipuko upi na ilitengenezwa maalumu kwa mlipuko upi.

5. Tume imeshindwa kutuelezea mafanikio ya chanjo zote hizo ni nchi zipi zimefanikiwa kuzuia maambukizi mapya baada ya kupatiwa chanjo hizo.

6: Tume imeshindwa kukubali au kukataa kuhusu athari za vifo vitokanavyo na chanjo hizi ikiwa tutadhurika na chanjo hizi, isipokuwa Tume imeihakikishia serikali kuwa ni chanjo salama na zenye ufanisi. Lakini muda huohuo inazitaja chanjo zote kuwa ni fanisi, muda huohuo inapata kigugumizi kuitaja chanjo ambayo wao wamejiridhisha nayo kuwa ni nzuri na salama.

7: Tume imeshindwa kutuambia katika mataifa ambayo viliripotiwa vifo vitokanavyo na watj kuchanjwa hizi chanjo zilitokana na nini na kwanini wao kama time wahisi hii chanjo itakuwa salama zaidi kwetu kuliko huko zilikoua wananchi wa mataifa mengine.

Ni kweli kabisa mimi sina elimu kubwa kama ya hawa MAPROFESA, ila ninaamini kuna utofauti mkubwa sana kati ya ELIMU na AKILI.

UTOFAUTI WAKE UPO HIVI: Akili ni kile kinachobakia baada ya kuondoa yote uliyofundishwa darasani.

Kwa mujibu wa mwanafalsafa wa zamani kidogo, Robert Einstein kwamba kuna watu wakiondoa yale waliyofundishwa darasani, vichwa vyao vinabaki vitupu. Kitu pekee walichojaza kichwani ni yale waliyofundishwa darasani. Hawa ndio hujisifia vyeti, au idadi ya "digrii" walizonazo. Hawana akili, japo wana elimu.

Einstein alisema hakuna uhusiano kati ya elimu na akili. Kuna watu wana elimu lakini hawana akili, na wengine wana akili lakini hawana elimu. Ni bora uwe na akili ukose elimu, kuliko uwe na elimu ukose akili.

Kaka yangu Malisa GJ aliwahi kusema kwamba Icons wa Sayansi kama Isaac Newton, Galileo Galilei na Archimedes of Syracuse hawakuwa na elimu yoyote ya cheti, diploma wala degree, lakini walikua na AKILI. Ugunduzi wao mpaka leo unaiongoza dunia.

Akili siku zote ni "superior" kuliko elimu kwa sababu akili ndio ilibuni elimu. Yani watu wenye akili walikaa wakakubaliana waanzishe utaratibu ambao utamuwezesha mtu kukaa darasani na kujifunza kwa kipindi fulani, kisha apimwe kwa mitihani na atunukiwe cheti. Ubunifu huo ulifanywa na wenye akili. Jiulize mtu wa kwanza kutunukiwa degree duniani alifundishwa na nani?

Kwa hiyo niseme tu kwamba ambao hatuna hizi PhDs mtuheshimu vilevile kwa maana tunazo "akili" za kutambua michongo yenu kwa urahisi zaidi kuliko kale kamstari kembamba kanachotenganisha akili nyingi na ukichaa.

C&P

Bwana Mshana kwa maoni yangu pana mambo ya msingi sana umeyaruka labda ili kufanikisha uliyotaka kusema. Kwa mfano mfano hili:

1. "Tangu kuingia kwa ugonjwa wa COVID-19 nchini mwezi Machi 2020, Tanzania imekumbwa na mawimbi mawili makubwa na hivi sasa kutokana na mwenendo wa ugonjwa huo katika mataifa mengine duniani na kuna tishio la kutokea kwa wimbi la tatu hapa nchini."

=====> Hili limo kwenye ripoti ya tume lakini wewe unadai kwenye #3 kuwa tume haijasema Corona ipo au la? Bwana Mshana umepatwa pepo gani mchafu kutokea Lumumba?

Hapa mbona ni wazi hawakutaka tu kistaarabu kuwataja kwa majina vigogo kweli kweli walio koronwa vilivyo na huyu kirusi?

2. Kwamba tume ingekuja na mapendekezo tofauti na WHO?

====÷> hapa inaweza ukawa hujaitendea haki tume. Inawezekana tume tokea katika utafiti wake usiohusiana na WHO imekuwa na matokeo yanayofanana na WHO.

Kwa maana nyingine yawezekana matokeo ya WHO ndiyo yaliyofanana na ya wataalamu wetu.

Hata kama walikuta kufanana huko wewe ulitaka watoe majibu ya tofauti tu ili kumridhisha nani? Kila awamu ya ukaidi wa kijima jima haipo tena!

Ningependa kukudonyolea yako yote na yao pia kukuonyesha wao wako juu sana. Labda nitakapopata mapumziko mkuu nitaendelea. Kwa sasa niko kwenye kuchapa kazi kweri kweri. Nitakurejea.

Ila nisiache kukunong'oneza tu mkuu:

"Ripoti ya tume kwa ujumla wake iko vizuri sana. Pia zingatia kina msukuma hawawezi kuacha kununa kwa uwepo wa ripoti kama hiyo.

😂😂😂😂😂😂😂😂!
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]!
Ripoti ya tume kwa ujumla wake iko vizuri sana. Pia zingatia kina msukuma hawawezi kuacha kununa kwa uwepo wa ripoti kama hiyo.[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Walioleta hii ripoti ni wenye elimu kubwakubwa (Maprofesa, PhDs', Masters, Degrees) na wengineo wamo humo na inawezekana "La saba pia wamehusika kwa namna moja au nyingine, inawezekana kabisa dereva aliyewapeleka Ikulu ni Form Four Failure, ana leseni yake ya NIT akapata CONNECTION yuko pale anaendesha gari ya PhD holder pale.

Inawezekana kabisa aliyebadili tairi njiani ni mshikaji tu akiyeishia "La saba", huyo ndo kanusuru maisha yao kwa kuwabadilishia tairi lililochoka na kuweka jipya. Na akalipwa kiasi fulani cha fedha. Mlipaji huyu ni serikali kupitia kwa PhD holder anaepelekwa field kupata majibu ya maswali yake kujenga hoja kwenye tume ya Corona.

Kinachonishangaza ni kuona Elimu zetu hazitusaidii, tangu siku ya kwanza ilipotangazwa kuanzishwa Tume ya Corona, niliuliza maswali yafuatayo:-

1: Tume inaweza kuja na mapendekezo tofauti na Yale ya WHO?
2. TUME hii itakuja na majibu yasiyoacha shaka kwa Wananchi?
3: Tume hii itakiri kuwa CORONA nchini haipo?
4: Tume hii itaonesha athari halisi zilizopo mitaani bila kuacha shaka?
5: Tume hii itakubali kukosolewa?

Baada ya kitambo kidogo, majibu yametoka, maswali yangu yote yamejibiwa.
1: Tume haijavuka mapendekezo ya WHO hata moja, hakuna pendekezo la tume linalopingana na WHO, wamefanya ku_copy na ku_paste kila kitu. Sijaona dira yetu kama taifa ni ipi kuhakikisha tunaishi kulingana na Uhuru wetu kama taifa.

2: Tume imekuja na majibu yenye mashaka kwa wananchi, hakuna mtu asiye na shaka ma majibu ya tume kuanzia kwenye VITABU hivyo vikubwa 6.

3: Tume haijakubali kuwa CORONA ipo au haipo isipokuwa inazungumzia ujio wa WIMBI la 3 ambalo ni hatari zaidi, yaani TUME imefanyia kazi "HEAR SAYING" , kwamba na yenyewe inakubaliana na utabiri bila yenyewe kufanya ujasusi kujua iwapo ni taarifa za kweli ama si za kweli.

4; TUME imeshindwa kutupatia majibu sahihi kwamba hii chanjo tutakayochanjwa ilitengenezwa maalumu kwa ajili ya Kinga ya mlipuko upi? Maana hadi sasa tuko katika wimbi la PILI, chanjo hii ilikuwa maalumu kwa kundi la mlipuko upi, moja Kati ya ile miwili au kwa utakaokuja huo wa 3... Tume imefeli hapo katika kuainisha aina ya mlipuko na chanjo tunayoipokea ni kwa ajili ya mlipuko upi na ilitengenezwa maalumu kwa mlipuko upi.

5. Tume imeshindwa kutuelezea mafanikio ya chanjo zote hizo ni nchi zipi zimefanikiwa kuzuia maambukizi mapya baada ya kupatiwa chanjo hizo.

6: Tume imeshindwa kukubali au kukataa kuhusu athari za vifo vitokanavyo na chanjo hizi ikiwa tutadhurika na chanjo hizi, isipokuwa Tume imeihakikishia serikali kuwa ni chanjo salama na zenye ufanisi. Lakini muda huohuo inazitaja chanjo zote kuwa ni fanisi, muda huohuo inapata kigugumizi kuitaja chanjo ambayo wao wamejiridhisha nayo kuwa ni nzuri na salama.

7: Tume imeshindwa kutuambia katika mataifa ambayo viliripotiwa vifo vitokanavyo na watj kuchanjwa hizi chanjo zilitokana na nini na kwanini wao kama time wahisi hii chanjo itakuwa salama zaidi kwetu kuliko huko zilikoua wananchi wa mataifa mengine.

Ni kweli kabisa mimi sina elimu kubwa kama ya hawa MAPROFESA, ila ninaamini kuna utofauti mkubwa sana kati ya ELIMU na AKILI.

UTOFAUTI WAKE UPO HIVI: Akili ni kile kinachobakia baada ya kuondoa yote uliyofundishwa darasani.

Kwa mujibu wa mwanafalsafa wa zamani kidogo, Robert Einstein kwamba kuna watu wakiondoa yale waliyofundishwa darasani, vichwa vyao vinabaki vitupu. Kitu pekee walichojaza kichwani ni yale waliyofundishwa darasani. Hawa ndio hujisifia vyeti, au idadi ya "digrii" walizonazo. Hawana akili, japo wana elimu.

Einstein alisema hakuna uhusiano kati ya elimu na akili. Kuna watu wana elimu lakini hawana akili, na wengine wana akili lakini hawana elimu. Ni bora uwe na akili ukose elimu, kuliko uwe na elimu ukose akili.

Kaka yangu Malisa GJ aliwahi kusema kwamba Icons wa Sayansi kama Isaac Newton, Galileo Galilei na Archimedes of Syracuse hawakuwa na elimu yoyote ya cheti, diploma wala degree, lakini walikua na AKILI. Ugunduzi wao mpaka leo unaiongoza dunia.

Akili siku zote ni "superior" kuliko elimu kwa sababu akili ndio ilibuni elimu. Yani watu wenye akili walikaa wakakubaliana waanzishe utaratibu ambao utamuwezesha mtu kukaa darasani na kujifunza kwa kipindi fulani, kisha apimwe kwa mitihani na atunukiwe cheti. Ubunifu huo ulifanywa na wenye akili. Jiulize mtu wa kwanza kutunukiwa degree duniani alifundishwa na nani?

Kwa hiyo niseme tu kwamba ambao hatuna hizi PhDs mtuheshimu vilevile kwa maana tunazo "akili" za kutambua michongo yenu kwa urahisi zaidi kuliko kale kamstari kembamba kanachotenganisha akili nyingi na ukichaa.

C&P
Hii nchi Duuuu, yaani Usanii mpaka aibu, ptyuuuuu, hivi kweli ndani ya siku tuseme 40 tangu tume ambayo hatujui hata iliundwa lini et imesha fanya kazi na kuandika vitabu vikubwaaaaaa kadhaa Kama vile, aisee vile vitabu nilivyo vishuhudia nivikubwa kuliko hata BIble eti, na siyo kimoja,WaTz tunaonekanaga wajinga Sana.
 
Yaweza kua sawa asilimia mia usemayo mkuu, mimi nije tu na hii ukweli ni kua haya yote tunasema hapa sababu tumestirika dhidi ya Covid 19 na tusitirike daima,Ndo maana waswahili wakasema ugonjwa ukikubali ni ngumu kuikataa dawa, Unafikir India wanaweza jiuliza kuhusu chanjo kua ni feki au sio feki?? Na je hadi sasa tushapokea chanjo ngapi za maradhi mbalimbali hapa mjini kwetu?, nani aliunda tume kukubali au kukataa ikiwa zipo hizo chanjo na bilashaka wewe na mwanao mshapata sivyo? Wanasayansi wetu washagundua chanjo ipi au kubaini makosa gani kwa chanjo ainishwa hadi leo? Lazima ifahamike kua sisi tulishakua sampuli zao tokea miaka mingi na hatuwezi jinasua kwa makala kama hizi au KIRAHISI hivyo basi linalo wezekana lifanyike sababu sisi hata chanjo moja tu hatuna zaidi ya upuuzi nyungu,
Kama huwez pambana nao ungana nao tusilete propaganda (Mfano tuu kwa hali ya Ebola pale DRC ilivyo kua Unafikir walikua na muda wa kuuliza chanjo ni feki au sio feki? )

Sent from my SM-M115F using JamiiForums mobile app
 
Waliounda tume wapelekwe hapo SA tu wadungwe chanjo ya AstraZeneca then tuwafuatilie kwa wiki kama 8 hivi tuone hali zao.

Tume ya kipuuzi sana. Nilipoona wameshindwa kugusia chochote kwenye chanjo hata moja tu, nikahisi hii tume ilijifungia room mahali flani, wakazama google na kucopy ugoro kutokea huko
 
Mimi Nataka hivi viongozi wote wa serikali wakubali kuchanjwa hadharani bila kuleta kiini macho siwao wamekubaliana na chanjo waanzae Sasa wao
 
Mkuu hata huku hospitali ukiwauliza watumishi wenzako vipi wakianza kutoa chanjo ya Corona utachoma?

Atakwaambia mimi sichomi hata iweje

Kipindi kile corona imeshika Moto walisema viongozi wetu wameshachoma chanjo sisi huku hatupewi chanjo[emoji1][emoji1]

Yaaani kweli tuna elimu ila akili hatuna
 
Musiwalaumu Tume maana hamjui kazi walio pewa.

Tume imefanya kazi kwa matakwa ya mwajili tu.
 
Luku tu imezingua siku tatu tu lakini nchi nzima chali, kumbe watu wengi wananunua LUKU ya buku mbili mpaka tatu kila baada ya siku moja au mbili, sasa wafungie uone njaa itakavyowababua
Kabisa mkuu,tuombe maamuzi ya serikali yasiwe kushurutisha kama majirani zetu Kenya.Kufa kwa njaa ni uhakika kuliko hiyo corona
 
Back
Top Bottom