Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Kutokana na ugumu au vipaumbele vya maisha, watu wengi wanajitahidi kupunguza matumizi ya fedha yasiyokuwa ya lazima. Sasa wewe kipato chako hakitoshelezi kufanya sherehe ya harusi kubwa, huku ukitaka sherehe yako ianzie labda milioni 20, wakati wewe kianzio ulichonacho labda milioni 1; hizo zingine unategemea upate kwa watu, kwa njia ya kuchangisha, huo sio uungwana.
Kwa nini ujibebeshe mzigo usioweza, na matokeo yake ni kuwapa wachangiaji majukumu ambayo si ya lazima. Starehe upate wewe, kwa nini usumbue wengine?
Ukiniona nipo kwenye ndoa na sijawahi kukupa kadi ya harusi kwa ajili ya mchango; usiniletee kadi yako ya mchango wa harusi.