Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii ya nne, imesha chacha!Naunga mkono hoja, hasa hiyo namba 4,,
Ni upuuzi. Hivi dunia hii itadiliki kudanganya kweli? Walikuwa na lao jambo. Ila sasa Kagera wajiangalie sana, wasipokuwa makini hizo mechi za play off zinawaondoa kwenye ramani, maana maboss wa mpira hapa nchini sana allege nao. Itawabidi wajiandae kwelikweli.Kwani kabula taarifa haijatolewa official bodi haikukaa kujiridhisha?
Vp kati ya livescore zetu na zako zipi sahihi.Kaeni na live score zenu duniani msimamo wa tff upo wazi inaangaliwa head to head stand atacheza play off kagera kashuka daraja Team ya kinafiki sana ninafuraha sana hapa tunapiga mvinyo tu asanteni sana mbao fc
BODI YA LIGI YAIREJESHA KAGERA SUGER PLAY OFF.
HEMED KIVUYO.
Bodi inayosimamia ligi kuu Nchini imekiri Kuwepo kwa Makosa ya takwimu Na kuirejesha timu ya Kagera suger katika ligi kuu ambapo sasa inacheza hatua ya play off.
Akingea Na ITV mtendaji mkuu wa bodi hiyo Boniface wambura AMESEMA kwa Makosa hayo ofisi yake inawajibika kwa kumpa adhabu aliyepotosha takwimu hiyo.
Kwa Mustakabali huo timu ya Stand United in ashuka daraja moja kwamoja Na Kagera suger italazimika kucheza michezo miwili ya play off ili kupata ridhaa ya Kuendelea Na ligi kuu msimu ujao
Gentamicine ktk sababu zako vp umebaki na ngapi?
Usiempenda bado yupo!Mkuu yaani nina furaha ya ajabu kwa Kagera Sugar Kushuka rasmi Daraja leo. Malipo ya ' Unafiki ' Mwenyezi Mungu huyalipa hapa hapa duniani tena ukiwa hai na unayashuhudia kabisa.
Aaahaaa imekula kwako Kagera haijashuka [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji872]KWANZA
Klabu yangu ‘ pendwa ‘ ya Simba imekuwa Bingwa tena na Kukabidhiwa rasmi Kombe lake ili iweze Kuiwakilisha vyema Tanzania ya Rais wangu Mpendwa Dkt. John Pombe Magufuli katika Michuano ya Kimataifa ya Klabu Bingwa Afrika ambapo nina uhakika kwa kuwa mwaka huu tumefika hatua ya Robo Fainali basi Msimu ujao ni Kufika Nusu kisha Fainali na hatimaye tunabeba Kombe kabisa.
PILI
Klabu inayotoka Nyumbani kabisa ( Mkoa wangu wa Asili ) wa Mara ( Musoma ) ya Biashara United imebaki Ligi Kuu hivyo bado Msimu ujao wana Mara wote watakula raha na Mkoa utakuwa Kimchezo na Maendeleo yatazidi Kupatikana. Kwa kuendelea Kubaki Ligi Kuu kwa Msimu ujao nina uhakika Vipaji vingi vya Soka vilivyopo Mkoani Mara vitaonekana ili kurudisha enzi za Wachezaji kama akina George Magere Masatu, Bita John, Elias Maguri, Rajab Msoma, Kimune Mwita, Chacha Marwa, Ally Mchumilla na GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE bila kusahau na wengineo wengi sana ambao walicheza Klabu za TP Lindanda ( Pamba FC ) na wengine kwa sasa wanacheza Vilabu mbalimbali kama Mbao FC, Alliance FC, Mwadui FC, KMC FC huku wengi Wao wakiwa katika Timu za Majeshi za Ruvu, Mgambo na wengine wakiwa Timu za Polisi. Kitakwimu Mkoa wa Mara ( Musoma ) unashika Namba Tano ( 5 ) kwa Kutoa Wachezaji wenye Vipaji vya Soka / Kabumbu nchini ukitanguliwa na Mikoa ya Morogoro, Kigoma, Tabora na Mwanza pekee.
TATU
Klabu ya Rafiki yangu Kipenzi na Kocha Bora Kijana kabisa na Nahodha aliyekuwa na Mafanikio Simba SC Mtani wangu wa ‘ Kiha ‘ Suleiman Abdallah Matola ya Lipuli FC imebaki Ligi Kuu na nina uhakika Msimu ujao itafika mbali sana.
NNE
Klabu nisiyoipenda na ninayoichukia mno pamoja na Kocha wake ambaye ‘ hatupendani ‘ kabisa tokea akiwa Mchezaji Mecky Maxime ya Kagera Sugar imeshuka rasmi Daraja. Huyu Kocha ni ' Mnafiki ' mkubwa na ana ' Uyanga Uyanga ' mwingi, wa wazi wazi wala hafichi ambapo Yanga ikicheza na Kagera Sugar huwa anapanga Kikosi ' dhaifu ' makusudi ili Kagera Sugar ifungwe na Yanga lakini akijua anacheza na Simba SC huyu Kocha huwa anatumia muda wake mwingi kuwahimiza Wachezaji wake ' wakaze ' sana huku hadi akiwaahidi ' Zawadi ' nono Wachezaji wake ambazo zingine nyingi huwa anakuwa amepewa na wana Yanga ili tu ' aifunge ' Simba na huku hadi Yeye mwenyewe akishiriki katika ' Kuiroga ' Simba ili Kagera Sugar ishinde.
Kocha Mecky Maxime amevuna alichokipanda na kama wana Simba SC ' tulivyoilaani ' Toto Afrika ambayo nayo ilikuwa na ' Upuuzi ' huu huu wa Kagera Sugar kwa ' Kuikazia ' Simba kupitia kwa Kocha Wao ' Mnafiki ' mwingine Mzee John Tegete ' tumeilaani ' pia na Kagera Sugar na tutahakikisha haipandi tena Ligi Kuu kama ambavyo Simba tunaifanyia ' Fitna ' Kubwa Toto Afrika isipande Ligi Kuu na haitopanda na hazitopanda ng'o hadi wakome / zikome.
Nawasilisha.
Jichome kidole uko nyuma ili tuone hasira zakoHao BODI YA LIGI ni ' Wapumbavu ' kabisa na Kuanzia leo ' nimewadharau ' na nina ' Hasira ' nao Kishenzi ' Wapuuzi ' wakubwa.