Habari zenu,
Kuna ile tabia unaenda dukani unanunua kitu unazidishiwa au chenji inarudi imezidi.. Kuna wengine waungwana husema papo hapo na kuna wengine hutoka na speed 120km/h bila kuangalia nyuma asije kuitwa.
Sasa tuje upande wa matibabu. Ikitokea umeenda kununua Dawa iwe Dukani/Duka la Dawa/Hospital ukazidishiwa kwenye package utarudisha au utanyamaza ukatumie na siku nyingine?
Na nini madhara yake au faida yake, Kumbuka umenunua haijalishi ni wapiii.