Ukiomba msaada humuoni mtu ila ukifa wanatoa michango ya maana!

Ila msiba wako pesa wanayo
Hii ni kwa sababu binadamu wamekosa uaminifu. Watu wanatumia uongo kuomba misaada hata pale ambao hawana shida kubwa. Wewe unaweza ulikuwa na shida ya kweli lakini umekuwa victim kwa sababu ya uongo wa wengine. Mimi katika vitu vilivyonishangaza muda nilioishi hapa duniani ni binadamu kuotokuwa waaminifu kwenye mambo ya fedha. Kwa upande mwingine ukisikia kwenye kufa watu wanakuwa na uhakika ya kuwa ni shida ya kweli. BTW hili ni jambo zuri kwa sababu linafanya watu wajitume na kufanya kazi badala ya kuwa ombaomba. Kazi ni kipimo cha utu.
 
Yani mtu umemkopesha mfano 500k hajakulipa mwaka mzima, afu aje akuombe tena 100k utampa ?
ukiombwa mkopo 500k mpe ambayo hata akipotea nayo haitakuathiri labda 150k,akipotea jumla na usimuulize hatakaa aje kukuomba tena hela.
 
Kipindi chote wanatayarisha msiba ulikuwepo wapi na ulijuwaje kuhusu hiyo michango yote na matumizi bila ya wao kujua kama haujafariki.
Halafu kumbe ulikuwa mfanyakazi kwanini ulishindwa kuomba mkopo kazini!
 
Kwa hiyo walianza michango na matayarisho ya kukufukia bila kuuona na kuthibitisha mwili wako?Marehemu acha fiksi basi!
 
Kama uliwahi kushuhudia hilo ilikuwa upambane
 
Hata mimi nimeomba msaada kwa watu 3 wapo kimya ila siku nikifa watatoa mahela kibao.Daaah
 
Mimi nimekuchangia kwa uwezo wangu kisha wewe unasimama hadharani na kusema "eti nimekuchangia kidogo sana"! Hauna shukurani wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…