Pre GE2025 Ukiona kiongozi Mkubwa anahama chama peke yake tambua kwamba hakuwa na Watu

Pre GE2025 Ukiona kiongozi Mkubwa anahama chama peke yake tambua kwamba hakuwa na Watu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wewe huwezi kujua Mikunjo ya uso wako bila msaada wa Kioo. Kioo kwa upande huu ni sisi. Kwa kawaida mtu mmoja hata akiwa MBOWE hawezi zidi chama. Unavyolia lia na kuanzisha sredi za kipuuzi, unaonesha alivyowaumiza kutoka.

Imagine unalinganisha mwenyekiti wa kanda na mtu ambaye kikatiba amepewa kipande cha nchi. Mtu ambaye analindwa na Bunduki 7 ambazo kikatiba hata Waziri Mkuu hana, hata Makamu wa Rais hajapewa kikatiba! Watu wenye kuwa na mwanajeshi nyuma yake ni JWTZ kwa upande wa Rais, Mkuu wa Mkoa ni Polisi na Mwenyekiti wa Kijiji Mgambo. Unalinganisha Mwenyekiti wa Kanda wa Chadema na Mkuu wa Mkoa, hapo si umewehuka kwa Msigwa kutoka chadema! Tuliza akılı kwanza.

Jaribu kuacha kuweweseka. Tulia kwanza. Msigwa ni mpango wa Mungu.
Kwi Kwi Kwi sasa hapa anayelia ni nani jamani?
 
Viongozi wengi wakubwa kwenye vyama vya siasa wanaokubalika wanapoondoka kwenye vyama vyao huondoka na kijiji, kwa maana wanaondoka na wafuasi wao, maana wanakuwa nao, Lowassa alipokwenda Chadema alikuja mpaka na watu wa Usalama wa Taifa, alihama na Polisi na alihama na viongozi kadhaa, wengine ili wasidhuriwe walihama kimoyomoyo akiwemo Emmanuel Nchimbi na Sofia Simba .Wengine wamefia Chadema akiwemo Dkt Makongoro Mahanga.

Sasa ukiona Kiongozi anahama peke yake jua kwamba lilikuwa galasa, hakuwa na watu na kama ni hivyo huyo mtu maana yake alikuwa selfish na tabia yake kwa ujumla ianze kutiliwa mashaka..
Hana akili yule nakumbuka alikuwa analialia kipindi mwakalebela kauza nyumba yake ndani ya wiki akashangaa yeye mshindi
 
20240701_005919.jpg
 
Wewe huwezi kujua Mikunjo ya uso wako bila msaada wa Kioo. Kioo kwa upande huu ni sisi. Kwa kawaida mtu mmoja hata akiwa MBOWE hawezi zidi chama. Unavyolia lia na kuanzisha sredi za kipuuzi, unaonesha alivyowaumiza kutoka.

Imagine unalinganisha mwenyekiti wa kanda na mtu ambaye kikatiba amepewa kipande cha nchi. Mtu ambaye analindwa na Bunduki 7 ambazo kikatiba hata Waziri Mkuu hana, hata Makamu wa Rais hajapewa kikatiba! Watu wenye kuwa na mwanajeshi nyuma yake ni JWTZ kwa upande wa Rais, Mkuu wa Mkoa ni Polisi na Mwenyekiti wa Kijiji Mgambo. Unalinganisha Mwenyekiti wa Kanda wa Chadema na Mkuu wa Mkoa, hapo si umewehuka kwa Msigwa kutoka chadema! Tuliza akılı kwanza.

Jaribu kuacha kuweweseka. Tulia kwanza. Msigwa ni mpango wa Mungu.
Mtoa mada kuna namna huwa anatokwa na akili
 
Kiufupi chadema ilishajifia huku kitaa ni kama haipo kabisa
 
Viongozi wengi wakubwa kwenye vyama vya siasa wanaokubalika wanapoondoka kwenye vyama vyao huondoka na kijiji, kwa maana wanaondoka na wafuasi wao, maana wanakuwa nao.

Lowassa alipokwenda Chadema alikuja mpaka na watu wa Usalama wa Taifa, alihama na Polisi na alihama na viongozi kadhaa, wengine ili wasidhuriwe walihama kimoyomoyo akiwemo Emmanuel Nchimbi na Sofia Simba. Wengine wamefia Chadema akiwemo Dkt Makongoro Mahanga.

Sasa ukiona Kiongozi anahama peke yake jua kwamba lilikuwa galasa, hakuwa na watu na kama ni hivyo huyo mtu maana yake alikuwa selfish na tabia yake kwa ujumla ianze kutiliwa mashaka.

PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Mchungaji Peter Msigwa ahamia CCM
Chawa at work!
 
Mbowe ni vyema aka ruhusu uchaguzi huru na wa haki katika chama na kuruhusu wagombea uenyekiti wa chama wengine waweze kumchallange ili kama kweli wanachama bado wanamuhitaji basi itadhihilika kuliko kutuaminisha kwamba watu wote huko chamani wanamtaka yeye tu.

Hii itampa sifa ya kuendelea kuongoza ingawa ana muda mrefu Sana kama mwenyekiti.

kiufupi sisi tusiofungamana na chama chochote hatuoni Kama Kuna demokrasia huko zaidi ya mbowe kuongoza chama kama mali yake binafsi ingawa sio tatizo la chadema peke yake.

Ili kutengeneza picha nzuri ndani ya chama mbowe anatakiwa kuwa tayari kuachia uenyekiti ama sivyo watu wenye akili timamu hawawezi kukipa majukumu ya kuongoza nchi chama kinachoongozwa na mtu mbinafsi kama mbowe
 
Mimi binafsi siafikiani kabisa na alichofanya Msigwa lakini kwa upande mwingine ametumia haki yake ya uhuru wa kuchagua atakacho.

Hili swala la kum discuss kila mara hata ikiwa ni discussion negative kumuhusu ki uhalisia zinazidi kumpaisha tu kuliko kumdidimiza. Inajenga picha kama vile kuondoka kwake kumeumiza sana CHADEMA.

Ikiwa Slaa aliondoka na chama kipo hai mpaka leo, Msigwa ni nani hasa??

Ifikie wakati ikubalike kuwa kaondoka na maisha yanaendelea. Hizi discussions za kila dakika kumuhusu zinampa kiki zaidi tu.
 
Back
Top Bottom