Pre GE2025 Ukiona kiongozi Mkubwa anahama chama peke yake tambua kwamba hakuwa na Watu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwi Kwi Kwi sasa hapa anayelia ni nani jamani?
 
Hana akili yule nakumbuka alikuwa analialia kipindi mwakalebela kauza nyumba yake ndani ya wiki akashangaa yeye mshindi
 
Mtoa mada kuna namna huwa anatokwa na akili
 
Kiufupi chadema ilishajifia huku kitaa ni kama haipo kabisa
 
Chawa at work!
 
Mbowe ni vyema aka ruhusu uchaguzi huru na wa haki katika chama na kuruhusu wagombea uenyekiti wa chama wengine waweze kumchallange ili kama kweli wanachama bado wanamuhitaji basi itadhihilika kuliko kutuaminisha kwamba watu wote huko chamani wanamtaka yeye tu.

Hii itampa sifa ya kuendelea kuongoza ingawa ana muda mrefu Sana kama mwenyekiti.

kiufupi sisi tusiofungamana na chama chochote hatuoni Kama Kuna demokrasia huko zaidi ya mbowe kuongoza chama kama mali yake binafsi ingawa sio tatizo la chadema peke yake.

Ili kutengeneza picha nzuri ndani ya chama mbowe anatakiwa kuwa tayari kuachia uenyekiti ama sivyo watu wenye akili timamu hawawezi kukipa majukumu ya kuongoza nchi chama kinachoongozwa na mtu mbinafsi kama mbowe
 
Mimi binafsi siafikiani kabisa na alichofanya Msigwa lakini kwa upande mwingine ametumia haki yake ya uhuru wa kuchagua atakacho.

Hili swala la kum discuss kila mara hata ikiwa ni discussion negative kumuhusu ki uhalisia zinazidi kumpaisha tu kuliko kumdidimiza. Inajenga picha kama vile kuondoka kwake kumeumiza sana CHADEMA.

Ikiwa Slaa aliondoka na chama kipo hai mpaka leo, Msigwa ni nani hasa??

Ifikie wakati ikubalike kuwa kaondoka na maisha yanaendelea. Hizi discussions za kila dakika kumuhusu zinampa kiki zaidi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…