Ukiona mtu mzima analia ujue kuna jambo

Ukiona mtu mzima analia ujue kuna jambo

MZEE WA USSOKE

Senior Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
120
Reaction score
42
Habari ya Jumatatu wazalendo wenzangu

Kumekucha na makucha yake,macho na masikio ni kwa wajumbe wa bunge la katiba wanaokula pesa zetu bure.

Jambo lililonifanya niandike ninachokiandika ni kitendo cha mtu mzima Ole Sendeka kulia,swali langu ni

Kweli mtu huyu anauchungu na Taifa hili kuliko watu wote?

Nadhani kuna kitu kimejificha nyuma yake.na amekubali kutumika ili wengine waliomtuma waonekane smart mbele ya watanzania.

nilichogundua ni kuwa kuna wabunge wa CCM na wabunge wa wanachi kupitia ccm.na sasa tutaona wabunge wa wananchi ni akina nani na wabunge wa ccm kama ole sendeka ni nani na nani.

Yetu macho na masikio.kama Mungu yupo upande wetu nani atakuwa kinyume nasi.

"Nchi yote sauti moja"
 
Huyu ole sendeka ni poyoyo tu. Alilia baada ya kikao chao cha 'caucus' cha majuzi kukubali kura za siri, wazo ambalo siku zote ccm imekuwa ikipinga na kusisitiza kura za wazi. Akaona kwa mwendo huo ccm itabwagwa katika chaguzi na hatimaye itaondoka madarakani - na yeye ubunge ndio bye bye. Ndio maana aliusuta uongozi wa ccm, akiwamo Pinda.

Hata hivyo kesho yake kiliitishwa kikao kingine na kutoa maamuzi na msimamo wa awali wa kura za wazi. Kwa maana hiyo machozi yake yamezua jambo!!!
 
Kura ziwe za wazi ili mbichi na mbivu zijulikane!
 
Back
Top Bottom