Ukiona mwanamke kaacha kukupenda, achana naye kabla hujaachwa

Upo sahihi mkuu, nilikua na demu nilitokea kumpenda na yeye akanipenda.

Kwa kuwa nilikua na kazi na yeye hana nikaamua kumpambania mpaka akapata kazi tena nzuri ofisi ya mshkaji angu.

Aliivyoanza kushika vipesa vya hapa na pale nikaanza kuona mabadiliko. Ikawa sometimes nikiomba faragha visingizio haviishi, mara niko bize kazini mara naumwa, nikitaka kwenda kumpokea kazini anajivuuuta kunijibu na wakati mwingine nikifika kazini kwao nakuta ameshaondoka nikimchek ananiambia Amepata lift.

Kufikia hapo mie red flag 🚩 zikaanza kujionyesha bila kificho lakini kidume sikutaka kuamini hali halisi nikazidi kukaza shingo.

Kuna siku nampigia simu ikawa inatumika kama dk5 hivi mfululizo(kidume najipa moyo labda anaongea na mama yake) baada ya hapo simu ikawa inaita ila haipokelewi baadae ikawa haipatikani kabisaaa hakuna siku nilipagawa kama siku hiyo.

Baada ya muda kidogo naona txt inaingia nikaifungua kwa kimuhemuhe, sasa kila nikiisoma naona mbona kama hii txt hainihusu mimi? Kumbe demu alikosea badala ya kumtumia bwana ake mpya akawa ameituma kwangu. Daaaaah!!!! Hakuna siku niliumia kama siku ile, nampigia kumuuliza akanichana live kwamba kwa sasa hayupo comfortable kuwa na mimi labda tupeane likizo. Nilichofanya nikafuta kila kitu kumuhusu halafu nikaanza mtihani mzito wa kumsahau ilichukua muda ila nilifanikiwa
 
Mapenzi hayashauriwi, wenye maamuzi magumu kwenye mahusiano ni watu exceptional, si kila mtu anaweza ni wachache sana.
Watu wengi wanajifunza kuhusu mahusiano kupitia matukio halisi wanayokutana nayo.

Unajifunza through experience or by making mistakes, that's it.

But through learning the hard way ndipo wengine afya ya akili haipo sawa ndipo kuumizana na kuuana, kutokuamini mwanaume/mwanamke, ulevi n.k.

Kama Adam alishindwa hadi kuzingatia maagizo aliyopewa na MUNGU, akamsikiliza mwanamke, hii kitaalamu tunaitaje? na shetani alivyo na akili huwa anafahamu sisi wanaume dawa yetu ni wanawake.
 
Ku'mamake alaaniwe yeye na viazi vyake
 
Inauma sana aisee.
 
Umefanya vizuri kufuta namba zake.
Mwanamke akikuomba space, ni kwamba amempata mbadala wako ila bado haamini kama jamaa anampenda , so anaplay safety net kwamba mambo yakigoma anarudi kwako.
Usimrudie huyo mpumbavu. Afadhali umepona.
 
 
Hongera
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…