Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Uchawi ni roho kamili, roho huwa haifi kirahisi. Hivyo mchawi akifa hata kama alipokuwa hai hakumrithisha mtu ofisi yake, usitegemee ule uchawi utapotea. Automatically uchawi utamtafuta mrithi atafundishwa katika ulimwengu wa Roho naye atakuwa mkubwa kuliko hata muasisi wake.
Muhimu: Huwezi kuushinda uchawi na wachawi kwa kutokuamini kuwa kuna uchawi. Kwasababu hiyo ndio maana uchawi hauishi bali unakua tu. Inasemekana kuwa Mwafrika huroga ili amtese mtu tu ndipo moyo wake hufurahi, while mzungu huroga ili apate hitaji lake.
Turudi kwenye mada, Uswahilini kuna watu hawataki kufanya kazi za nguvu hivyo hutumia uchawi chuma ulete kujipatia kipato( kiyao tunaita CHITOLA).
Kama una mfereji wa shilingi wachawi huweka wakusanya pesa ndani mwako ambao ni mende, panya, mijusi n.k. Uchawi (roho) inapewa vazi la wadudu au wanyama ili usishtuke mapema.
Utajikuta unapata pesa husongi mbele, unapata pesa matatizo yanakuja, unajua umetumia ku solve matatizo kumbe umepigwa.
Wakati mwingine magonjwa, vifo, ajali, mikosi hutumiwa hawa wadudu kukuletea nyumbani kwako.
Ushuhuda wa kweli: Niliishi Temeke nyumba moja ya kupanga, ile nyumba panya hawakauki, ukitia sumu utawaua kesho utamwona tena panya mwingine. Sikuamka haraka. Wakati nahamia kwangu nilihama na panya mmoja, kila nikiweka sumu hafi watakufa panya wa kawaida tu. Siku moja wife akaniambia kuwa huyu panya si wa kawaida , alirudia hili neno kama mara 3.
Siku moja nikiwa kazini nikampigia simu wife kuwa huyo panya mwisho wake umefika. Siku zilizofuata chache sana nikaambiwa tumefanikiwa kumuua yule panya. Sasa nyumba yangu haijawahi kuguswa tena na panya yeyote. Kuna mjusi vivyo hivyo alileta mazoea nikamfuta kabisa.
Sio wadudu wote ni wa kichawi, wengine huja kwaajili ya mazingira kuwa rafiki kwao, ila cha msingi ni kuwa makini, unaweza kujikuta unaishia pabaya.
Binafsi nilitumia maombi kuwaangamiza, nawashauri tumieni maombi au njia nyingine ambazo mnajua kuwa uchawi hautaweza kusimama endapo zitatumika. Kuna jamaa aliibiwa sana, baada ya kuapply maombi wakafa panya wengi akapewa notice ya kuhama mara moja na mwenye nyumba wake.