Ukiona unafundishwa mambo haya ujue unatatizo la msingi

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Wakuu Kwema!!

Taikon sina mengi. Leo ni haya tuu.

1. Ukiona unafundishwa namna ya kuishi na Mumeo au Mkeo, basi jua unatatizo la msingi.

2. Ukiona unafundishwa namna ya kuweka akiba, jua unatatizo la msingi.

3. Ukiona unafundishwa namna ya kutafuta Utajiri, Jua unatatizo la Msingi.

4. Ukiona unafundishwa namna ya kumtafuta Mungu, jua unatatizo la msingi.

5. Ukiona unafundishwa namna ya kuwalea watoto wako WA kuwazaa, jua unatatizo la Msingi Sana.

6. Ukiona unafundishwa namna ya kuyatunza mazingira unavyoishi, sijui mahali pakuhifadhia kinyesi, sijui mahali pakulala, Jua unatatizo la msingi.

7. Ukiona unafundishwa style za chumbani ukiwa na Mwenza wako, ujue unatatizo la msingi Sana.

8. Ukiona unataka kufundishwa namna ya kupata vitu uvipendavyo, Jua unatatizo la msingi.

9. Ukiona unamtegemea Mchungaji ati ndio akuombee Kwa Mungu, jua unatatizo la msingi kuliko unavyotegemea.

10. Ukiona unafundishwa namna ya kuzungumza, jua unatatizo la Msingi.

Mambo mengine haupaswi kufundishwa.
Hata mnyama hawezi kufundishwa Mambo hayo.

Taikon wa Fasihi
Dar es salaam
 
Huyu alieanzisha huu nae tunamuweka kwenye kundi gani

Ni kweli watu wengi wana matatizo mengi ya msingi Sana,na hii imepelekea kutoa fursa kwa watu wengine kujifanya wanaweza kutatua hayo matatizo.chanzo cha utapeli.watu wanapigwa hela ndefu kwa matarajio hewa kabisa.
 
Nadhani kwa mujibu wako pekee.
Tatizo la msingi ni vile tu we waliona, kwako laweza kua si la msingi na kuona kama ni mtu tu kujiongeza lakini kwa mwingine ikawa tofauti.
Jifunze kipya chochote unachoona kina manufaa kwako.
Hakuna aliezaliwa anajua ni kuelimishana na kukumbushana pale inapobidi.
 
Wewe mtata kweli mkuu
 
4. Ukiona unafundishwa namna ya kumtafuta Mungu, jua unatatizo la msingi.
Acha upuuzi..kama huamini wa mganga ambao babu na bibi zako waliwaamini na kutumia mitishamba wakaoana wakaziliana hadi kupatikana wewe bure wa hedi..leo unajifanya kuona havifai..kaa utulie na upompoma wako.

Usitake kila mtu aamini unachokiamini wewe.

#MaendeleoHayanaChama
 
Ngoja na mm nichangie kidogo

Ukiona unafundishwa table manner.... angali wewe ni mtu mzima....Ujue una tatizo la msingi....
 
Back
Top Bottom