Infinite_Kiumeni
JF-Expert Member
- Jan 23, 2023
- 382
- 687
Hautakiwi kumpa hisia za furaha muda wote, hautakiwi muongee vya kuboa kila muda. Usiogope kumwambia maneno ambayo unaona ni makali bila kumtukana/kumdhalilisha.
Usiogope kumwambia kitu kibaya usichokipenda kuhusu yeye, lakini isiwe kitu ambacho hakirekebishiki kama vile umbile la pua yake. Nzuri ni kumwambia kitu kuhusu tabia yake, na kiuzuri zaidi ni pale ukimsifia kisha ukamponda pia.
Mfano, unajua unanivutia lakini una ka ukorofi, hiyo ndo maana fupi ya kuchombeza. Unamwambia maneno ambayo ki kawaida haambiwi na wengine, au hayakubaliki kuongea hadharani, au mengine mwingine anaweza kutafsiri kama ni udhalilishaji, lakini kwa mwanamke anayekupenda ataona ni chombezo tu.
Pia unapomchombeza mwanamke ni kwamba unavuka mipaka ya mazungumzo ya kawaida. Ambayo utajisikia aibu kuongea ukiwa kwenye daladala lililojaa, lakini hutakiwi kuonea aibu pale unapoona mwanamke naye anakukubali. Hatokasirika bali atafurahia.
Mfano kama hivi na nimeelezea vizuri kwenye kitabu jinsi ya kuongea na mwanamke. Kuna mwanamke nlikutana naye tukaongea kawaida tu kujuana, nliona amebeba mazaga ya kupika, nkamuuliza msosi anaoenda kupika na kama anapikaga kitamu akaniambia ndio, kisha kukawa na ukimya, nkamwambia inabidi nionje mwenyewe ili nijue akasema haina shida.
Hapo utaona ni mazungumzo ya kawaida ila nkayabadili kwa kumwambia “Simpatii picha kama na mpishi naye ni mtamu kama chakula chake.” Akacheka na kufurahi zaidi akasema sijui, nkamjibu “Itabidi nionje vyote kwanza ili nijue.” kisha nikabadili mada.
Akafurahi zaidi, kuliko ningemwambia tu hongera na kumsifia anajua kupika wakati sijui lolote kuhusu msosi wake, au ningebadili mada baada ya ye kusema haina shida, nakua nimebaki katika mazungumzo ya kawaida bila kumfanya ajisikie hisia ya tofauti, au ningeendelea kuongelea chakula juu juu tu bila kumchombeza.
Kuchombeza hakutakiwi kuisha. Hata kama una mke wako wa miaka 30, usisahau kumchombeza. Kumchombeza mwanamke kunamfanya afikirie penzi ye mwenyewe na wewe kuliko kuongea kawaida na kuomba penzi.
Usisahau kumchombeza mpenzi wako.