MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 21,387
- 44,030
Watu wanaoomba kazi kwa sasa ni wengi mno ila bado waajiri wana changamoto ya kupata wafanyakazi watakaoenda sawa na maono ya kampuni zao. Ni ngumu kupata kijana mchapakazi, mwaminifu na makini kuendana na biashara. Unaweza pata mchapakazi na smart ila akawa na hitilafu kwenye uaminifu. Au ukapata mwaminifu ila sio smart. Kimsingi kupata mtu aliyenyooka ni mtihani. Wengi huomba kazi ili kutibu tu njaa na sio kuwa pia na malengo makubwa hasa kuongeza ujuzi.
Ni vijana wachache huomba kazi wakiwa na malengo ya kupata uzoefu na ujuzi kwenye fani zao. Wengi ni kutibu njaa tu. Kwa hiyo ndugu mwajiri ukipata mfanyakazi asiye na vipengele hakikisha unaenda naye sawa kwa manufaa ya kampuni yako. Tena akiwa wa marketing and sales ndo umkumbatie zaidi. Biashara ni watu. Hii tabia ya kuwaletea karaha wafanyakazi kisa wewe unataka kuonyesha uboss wako ni upuuzi mtupu.
USIMVURUGE MFANYAKAZI anayetimiza majukumu yake vizuri. Mrekebishe kidiplomasia anapokosea ila sio kumpanikisha kisa kosa dogo tu. Biashara nyingi zimeyumba kutokana na wafanyakazi wazuri kuondoka.