Ukipigiwa simu kwa private no.....................

Ukipigiwa simu kwa private no.....................

mzeelapa

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2010
Posts
1,118
Reaction score
404
Nimepokea message hii toka kwa washikaji zangu mbalimbali

"
Ukipigiwa simu kwa private no. au akaandika call kwa red colour usiipokee ni mionzi unaparalise na kufa. Imetokea kenya watu wamekufa. julisha ndugu & jamaa wote."

Kaelimu kangu ka science kananifanya isiniingie kichwani, hebu mabingwa mmeshapokea sms za aina hii?
 
HII IMEENEA SANA...ILA TUSIISADIKI MOJA KWA MOJA WALA KUIPUUZA MOJA KWA MOJA.....tuwe macho kujua ukweli wake......!
 
tumechoka....kuna thread nyingi sana km hizi humu jamvini wajameni...........
 
Tetesi hizi zinatia shaka sana.ila tuchukue tahadhari na wataalam wa elekronikia watueleze ili kuondoa hofu ndani ya jamii. Kwani unaweza zuka uvumi mwingine kwa lengo la kunga hofu tu.

Nimekuwa napokea simu za namna hiyo PRIVATE ila hazikuwa na rangi yoyote na ila mawasiliano yalikuwa si mazuri. Unajua simu nyingi za nje uwa zinaandika private.

Any way solution /majibu ya kitaalam yanatakiwa haraka .
 
Nimepokea message hii toka kwa washikaji zangu mbalimbali

"
Ukipigiwa simu kwa private no. au akaandika call kwa red colour usiipokee ni mionzi unaparalise na kufa. Imetokea kenya watu wamekufa. julisha ndugu & jamaa wote."

Kaelimu kangu ka science kananifanya isiniingie kichwani, hebu mabingwa mmeshapokea sms za aina hii?
..hapa nani anakuwa mpigaji mana hii inakuwa kama simu ya kifo..Je ni Shetani au malaika mtoa roho?? au mitambo ya simu!?:confused2:
 
Innovation in business nategemea na mimi nianzishe kampuni yangu ya simu za mkononi nispread msgs ukijamba saa moja na sekunde 60 unafariki tafadhali mjulishe na mwenzio by keep forwarding mie nakuwa na gain MONEY..... How does it sound? Habari hiyo huipati kwenye google si kwenye CNN wala TIBISII yaani kila mnacho ambiwa mnakubali tu hamtumii akili ya ziada? Ama kweli sometimes common sense is not common...
 
Mods, unganisheni hizi threads ziko kama mbili au tatu zinaongelea jambo hilihili!
 
hakuna lolote.
kisayansi mionzi ya kukuangamiza, hadi ikufikie wewe , ujue Tayari handset imeparanganyika, maana hakuna hANDSET INAYOWEZA KUKABILIANA NA KISHINDO cha mionzi inayoweza kumuangamiza binadamu.
huu ni uvumi, ni umbeya, mtu kakaa kichwani mwake kaamua kuenea ujinga.
hatudanganyiki, acha nirejee jukwaa la siasa, nikajadiri mbinu za kuing'oa ccm na Mafisadi.
 
Hakuna kitu hapo.isije ikawa ccm wanataka kuzuia watu kuwasiliana.walishasajili namba na mmeshaona voda wanavyohujumu upinzani.hatudanganyiki.au mmeshasahau uzushi wa mtoto mla watu muhimbili,popo bawa na mtu wa manyoya pale ubungo.hizi ni abrakadabra anazosema mjengwa
 
Dah! Jamaa anaonekana yuko serius kweli!.
 
Hakuna kitu hapo.isije ikawa ccm wanataka kuzuia watu kuwasiliana.walishasajili namba na mmeshaona voda wanavyohujumu upinzani.hatudanganyiki.au mmeshasahau uzushi wa mtoto mla watu muhimbili,popo bawa na mtu wa manyoya pale ubungo.hizi ni abrakadabra anazosema mjengwa
we we! Usimtaje huyo khabari yake nzito, shauri yako.
 
UZUSHI KUHUSU MADHARA YA MAWASILIANO YA SIMU

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imepata malalamiko kutoka kwa watumiaji wa simu za mkononi kwamba kuna ujumbe unaosambazwa kwamba ukipokea simu utapata madhara.

Mamlaka ya Mawasiliano inapenda kuwahakikishia wananchi kwa ujum;a kwamba taarifa zinazoenezwa ni za uzushi na sio za kweli. Wananchi wanaombwa kupuuza uzushi huo kwa kua hauna ukweli wowote.

Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, kuna tafiti nyingi zimefanyika sehemu nyingi duniani, ambazo zimeonyesha kwamba kiwango cha mawimbi ya mawasiliano hakina madhara kwa afya ya binadamu. Mamlaka inashauri watumiaji wa huduma na wananchi wote kwa ujumla, kuendelea kuwa na imani na teknolojia mpya zikiwemo za mawasiliano ya simu, utangazaji na utumiaji wa kompyuta, ambazo hutumiwa ulimwenguni kote bila kuleta madhara yoyote.

Madhumuni ya Mamlaka ya Mawasiliano na watoa huduma za mawasiliano kwa ujumla ni kuwaletea wananchi wa Tanzania mawasiliano bora kwa kujenga miundombinu, kutoa huduma bora na matumizi mema.

Uzushi unaoenea upuuzwe kwa kuwa hauna ukweli wowote.

Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
 
Back
Top Bottom