..This is too hard..marekani naonaga kwenye shows watu wanajitolea kupima live.......matokeo wengi hushindwa kuyabeba....
kwa hali ya tanzania mkemia mkuu anakuambia kuwa asilimia 50% tangu wameanza kupima ...wamebambikiwa watoto.....so hili tatizo ni kubwa ....sana ..ni wazi kuwa inawezekana sample size yao ikawa kweli na ukakuta asilimia 50% ya kinababa labda tunalea wana si wetu!!!!!
Huu ni momonyoko mkubwa wa kijamii ...wote wanaume kwa wanawake wamekuwa malaya...lakini kinadada chonde chonde...msifanye usawa kwenye hili ..kwani matokeo ya mwanamke kuwa na mpenzi nje ni kumzalia mumewe mwana wa nje[sipendi kutumia jina mwanaharamu ,kwani hana kosa]......nadhani hata dini ya kiislamu inapotoa adhabu kubwa kwa mwanamke anayekamatwa na zinaa kuliko mwanamke ....pamoja na kuwa sikubaliani na aina ya adhabu ni wazi inatokana wao kuangalia mazilla ya mwanamke kuwa na wapenzi wengi....
sasa ufanye nini ukigunduA?.....inategemeana kama mtoto mwenyewe ndio huyo huyo ..huna budi kumuacha mkeo..huo ni ushahidi ambao hata kama ni ndoa ya kikatoliki iliyo ngumu kuvunja wanakubali...lakini mwanamme baada ya hapo lazima akubali mfadhaiko mkubwa na mwanamke anaweza jitetea kuwa alienda nje kwa kuwa wewe hukuweza kumzalisha....ambapo jamii ya sasa itamuamini na kukuacha wewe mwanamme na aibu zaidi....hapo ndio maana wengine huvumilia ...na kujitahidi kujitafutia mtoto wa halali ....na ikitokea amempata nje ya mkewe basi huwa na kifua cha kumtosa mkewe ......na ataungwa mkono...kwa kuwa tayari ana mtoto mkewe hatakuwa na utetezi....
ikiwa mkeo ameteleza na labda kati ya watoto wannne ametokea mmoja si wako.....wengi humalizana kiutu uzima...kwani mwanamume huangalia zaidi welfare ya wale watoto wake watatu na kuamua kuvumilia......lakini hii humnyima mwanamke haki ya kumuuliza mmewe lolote kuhusu ..mahusiano!!!
Tukiangalia historia miaka ya nyuma hapakuwa na utamaduni wa kuangalia mtoto au kumchambua....mtoto akishazaliwa wanasema ..kitanda hakizai haramu......,hakuna ambaye wala alidhubutu kutuhumu ..hilo..unless mwanamke hakuwa na mme au ni mjane na hakuolewa tena...hapo watajiuliza na alitakiwa kutoa jibu!!!....tena wazee wa zamani ....akisikia mtu amemzalisha mkewe wala hakuwa na hasira ..ukizingatia watu walikuwa na wake wengi....atasema tu kuwa umemsaidia kulima shamba ....yeye anavuna!....kimsingi watotot ulikuwa utajiri[mahari -wakike],nguvu kazi....[wakiume]....watu walitamani wake zao wazae kila mwaka sembuse kuanza kuchambua nasaba!!!
siku hizi pia maisha ni gharama so ukizalisha mke wa mtu mwanamume anaumia mengi ..ikiwemo mateso aliyoyapata kulea mimba ya mkewe,kumtibia wakati wewe umetulia tulii...gharama za malezi ,masomo na mengineyo...alafu ndio aje asikie kabambikiwa lazima apagawe!!.