Ukipita karibu na kituo cha bodaboda ukiwatazama tu wanawasha pikipiki

Paspii0

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2020
Posts
638
Reaction score
1,043
Baadhi ya Bodaboda wa Bongo ni miyeyusho sana. Ukiwa katika pitapita zako karibu na kituo chao,ukiinua kichwa kutazama upande wao, bam! ,Wamewasha pikipiki zao zote,chapu kukufuata, kabla hata hujawaita ,ukiwaambia nipo around sihitaji usafiri,tena chapu kwa haraka pikipiki zao zinarudishwa kijiweni kwao na wanaendelea na mission zao kwa spidi ya ajabu. Unajiuliza, hawa ndio maafisa usafirishaji wenyewe?😀

Sasa, imekuwa kawaida, wapita njia wanakatiza vituo vya bodaboda huku vichwa chini, kama vile wanaaga maiti!,Hawawezi hata kubahatisha kuangalia, wanajua tu, kama macho yao yakikutana na ya bodaboda—hapo maisha yanakuwa magumu,hukupanga kuongea nao basi lazima uongee au utikise kichwa kuonesha sihtaji huduma yenu 😄

Lakini, wakiona mdada mzuri, mashalla, mwenye maliwato safi,jamaa wanakuwa kama satellite au CCTV kamera,macho ya kutisha!,Watamkodolea mpaka apotee mbali na wataishia kubaki na kimuhemuhe 😂 Hapa ndipo tunaweza kusema maadui wakuu wa kizazi hiki ni Ujinga, Maradhi, Umasikini na Nyege.

Hali imekuwa hivi; wengine wanapigania kupata mahitaji ya kila siku, chakula, mavazi, malazi na… sex! 😅 Na tunavyojua, ukiwa na haya, basi, vitu vingine havina maana tena!

Basi, tumieni vizuri kazi zenu, ziwanufaishe na familia zenu, msiishie tu kutembea barabarani bila faida yoyote.
Miyeyusho na kiki hazitusaidii!.
 
Mikoani uwasha na kufanya ivyo wakiona mabinti au wamama ,wanaume awapandi pandi boda ,ila Dar uwasha hata wakiona wanaume na kuwakimbilia mayai mayai sana huu mkoa
🤓Dar mkoa nyoronyoro, kaumbali kidg tu unakodi boda
 
Mkuu siku hizi nao washajua hawasubiri muwatazame, wanavizia usafiri wowote utakaosimama karibu na kituo chao wanawasha kuja kuangalia kama kuna abiria, hadi kuna muda unajiuliza hawa hayo mafuta yao si yatakuwa yanaishia kwenye hiyo nenda rudi ya kufuata abiria wasiohitaji bodaboda
 
Ndio ubunifu wao bana 😄,yamkin kuna faida jioni kwenye kufunga mahesabu
 
Hii tabia ya bodaboda ni ya hovyo na inakera sana, wengine ukiwa mbali wanakupia honi hovyo.
Haha hii ndio inakera bora kuitwa Ofisa ,mwebye miwani,sogea mwisho na konda wa daladala
 
Baadhi ya Bodaboda wa Bongo ni miyeyusho sana. Ukiwa katika pitapita zako karibu na kituo chao,ukiinua kichwa kutazama upande wao, bam! ,Wamewasha pikipiki zao zote,chapu kukufuata, kabla hata hujawaita ,ukiwaambia nipo around sihitaji usafiri,tena chapu kwa haraka pikipiki zao zinarudishwa kijiweni kwao na wanaendelea na mission zao kwa spidi ya ajabu. Unajiuliza, hawa ndio maafisa usafirishaji wenyewe?😀

Sasa, imekuwa kawaida, wapita njia wanakatiza vituo vya bodaboda huku vichwa chini, kama vile wanaaga maiti!,Hawawezi hata kubahatisha kuangalia, wanajua tu, kama macho yao yakikutana na ya bodaboda—hapo maisha yanakuwa magumu,hukupanga kuongea nao basi lazima uongee au utikise kichwa kuonesha sihtaji huduma yenu 😄

Lakini, wakiona mdada mzuri, mashalla, mwenye maliwato safi,jamaa wanakuwa kama satellite au CCTV kamera,macho ya kutisha!,Watamkodolea mpaka apotee mbali na wataishia kubaki na kimuhemuhe 😂 Hapa ndipo tunaweza kusema maadui wakuu wa kizazi hiki ni Ujinga, Maradhi, Umasikini na Nyege.

Hali imekuwa hivi; wengine wanapigania kupata mahitaji ya kila siku, chakula, mavazi, malazi na… sex! 😅 Na tunavyojua, ukiwa na haya, basi, vitu vingine havina maana tena!

Basi, tumieni vizuri kazi zenu, ziwanufaishe na familia zenu, msiishie tu kutembea barabarani bila faida yoyote.
Miyeyusho na kiki hazitusaidii!.
Siyo Pemba aisee, huku wananidhamu wakati mwingine wanakataa hata kutoa namba.
 
Back
Top Bottom