Mkuu kulikuwa na maasi ya aina mbili, uasi wa kwanza ni ule alioufanya "Malaika Lusiferi" na kuwashawishi "malaika wenzake" wengine pia wakaasi. Kisha baada ya huo uasi wa kwanza ukatokea tena uasi mwingine, huu ni ule wa wale malaika waliokuja duniani na kuoa mabinti na kuzaa nao.
Kundi hili la malaika waliozaa na wanadamu, baada ya gharika walikamatwa na kufungwa kwenye vilindi vya giza(YUDA 1:6) lakini Lusiferi na kundi lake wao hawakukamatwa mpaka ile siku atakapokuja YESU kwa mara ya pili(UFUNUO 20:1-3).
Baada ya maasi haya kufanyika, hakuna tena uasi utakaofanyika Mbinguni, Malaika wote waliobakia ni Watiifu kwa BWANA MUNGU.
Mkuu ni jina tu, fahamu kwamba wote hawa wanaitwa "wana wa MUNGU"(MWANZO 6:1-2). Unaweza ukawaita "malaika waasi", lakini baada ya kuasi walipewa jina la ujumla ambalo ni "Mashetani" maana yake ni "Maadui". Jina "Shetani" siyo jina lao la asili, wao ni malaika isipokuwa tu wao ni "waasi".
Ni kama vile kikundi cha "uasi" kikitokea katika nchi, utaona jinsi watu wanavyokipa majina ya ajabu ajabu ingawa waasi ni wananchi tu wakawaida.