Ukishachafuka mitandaoni ni vigumu kuoga ukatakata

Ukishachafuka mitandaoni ni vigumu kuoga ukatakata

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Kuna hukumu zinazoweza kumfuata mtu maisha yake yote hata kama alishakuwa mtu mwema.
nazo ni hukumu kupitia mitandao ya kijamii. mitandao ya kijamii ina kumbukumbu pana kuliko tunavyodhani.

picha, video au ujumbe unapochapishwa whatsapp, instagram, facebook au tiktok unaweza kunakiliwa na kusambazwa tena. hivyo, kuufuta sehemu ulipoanzia hakumaanishi umetoweka kabisa.
kadiri watumiaji wapya wanavyojiunga, wanaweza kuukuta na kuusambaza upya hata baada ya muda mrefu.

Mamlaka ya mawasiliano tanzania (TCRA ) imekuwa ikionya kuhusu maudhui yanayowekwa mitandaoni na kusisitiza matumizi makini.

ni muhimu kufikiria kabla ya kuchapisha jambo lolote, kulinda faragha, kuhakiki taarifa na kuepuka maudhui yanayoweza kudhalilisha au kuumiza wengine.
haya yote nayazungumza kwa kurejelea video za hivi karibuni za wanafunzi waliomaliza kidato cha nne wa shule ya sekondari aboud jumbe waliovuma kwa kauli zisizo na maadili.
video hizo zilipoenea, hukumu zilianza kutolewa kila upande. wapo walioona ni matokeo ya malezi mabaya, wengine wakahusisha tukio hilo na kufuata mkumbo, kukosa uchaji wa mungu na kudhoofika kwa mifumo ya malezi na maadili.

taarifa zilizotolewa zinabainisha kuwa oktoba 26, 2026 wanafunzi hao walikutana na uongozi wa wilaya ya kigamboni wakiwa pamoja na wazazi na walimu wao.

katika kikao hicho, inasadikiwa waliomba radhi mbele ya mkuu wa wilaya, maofisa wa ustawi wa jamii na wazazi, wakiahidi kutorudia tabia hiyo. kuomba msamaha ni ishara ya kukubali
 
kuna tabia na vijitabia ukishaona umeacha kuvifanya ..... unaanza kupevukaa
 
katika kikao hicho, inasadikiwa waliomba radhi mbele ya mkuu wa wilaya, maofisa wa ustawi wa jamii na wazazi, wakiahidi kutorudia tabia hiyo. kuomba msamaha ni ishara ya kukubali
1793602261900.png

 
Back
Top Bottom