Ukishangaa ya msanii wa vichekesho Idris Sultani utayaona ya baadhi ya makampuni ya simu. Eng Kamwelwe na TCRA tusaidieni

Enzi na Enzi

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2020
Posts
888
Reaction score
821
Msanii idris sultan na mwezake walifikishwa mahakama ya kisutu kwa makosa ya matumizi mabaya ya mtandao, moja ya makosa waliyokuwa nayo ni pamoja na yeye Idris kutumia namba isiyo yake, na mwenzake alishtakiwa kwa kuruhusu line yake itumiwe na mtu mwingine. Nakumbuka mahakama ya Kisutu iliwapa onyo.

Sasa kama moja ya kosa alilokutwa nalo Idris na mwenzake la Idris kutumia line isiyokuwa yake na mwenzake kushtakiwa kwa kuruhusu line yake itumiwe na mtu mwingine.

Ninachotaka kumweleza Waziri Kamwele, na yeye azielekeze Taasisi au Mamlaka zinazozisimamia kampuni za simu hasa TCRA nawao wachukue hatua ya kuzionya baadhi ya kampuni za simu zinazofanya yafuatayo.

1. kugawa namba za wateja wa makampuni yao kwa watu au kampuni nakuanza kutuma matangazo yao ya michezo ya kubahatisha na utapeli wanaofanyiwa watanzania. Mf. Unaambiwa namba yako imeshinda 5ml. Hivyo tuma shilingi kadhaa ili ukomboe (baadhi yawatu wanaibiwa)

2. Unashtukia namba mfano 5555 imeleta ujumbe namba yako imejishindia bahati nasibu ya tsh. Mf.20ml. Tuma neno au herufi au namba kwenda namba flan ili kushiriki bule naukifanya hivyo tu! Ujue kilasiku watakuwa wanakuchaji pesa ktk account yko. Pamoja na mambo mengine mengi tu ambayo yameperekea mataperi wa tuma pesa kwenye namba hii kutoisha pamoja na usajiri huu mpya.

Kama idris sultani alishtakiwa kwa makosa niliyoyataja yy na mwenzake yakiwemo na mengine hamuoni nanyie mnatakiwa kuyaonya makampuni yasimu yanayo gawa namba za watanzania bila ridhaa yao?

Hayo nimachache tu lakini yako mengi sana, wadau nanyie mtaongezea kero zilizopo ambazo mamlaka husika hazishughulikii labda kama wananufaika kwayo.
 
Ni Logic ndogo tu Ndugu huyu Idris Sultani wako anaiingizia Mapato Serikali? Hivi hujui tu kuwa Makampuni haya ya Simu yanaitajirisha Serikali?
 
Binafsi ninakeleka 'na meseji zinazo tu wa kwangu kuwa mitume pesa kwenye namba fulani
 
Makampuni ya simu yanatoa wapi power of Antony yakugawa.
1.line niliyonunua mimi kwa hela zangu.

2.line niliyosajiri kwa kitamburisho cha kitaifa tena kwa mujibu wa sheria?

3.line ambayo naweza kushitakiwa endapo nitampa hata baba yangu mzazi kuitumia?

4.line ambayo natakiwa kuitoa mimi mwenyewe kwa mtu yoyote?

5.line ambayo ni bank , ni bank ya siri kubwa ambayo hata mkewangu hawezi kuingia na kusoma vitu bila ridhaa yangu namimi siwezi fanya hivyo kwenye line ya mke wangu wao niakinani?

6. Line ambayo kila kukicha tcra wanasisitiza kutompa mtu simu kuitumia? Kwanini wao wanagawa?

Mwisho! Hivi sheria zetu huwa zinang'ata masikini na waganga njaa pekee?
 
Ni Logic ndogo tu Ndugu huyu Idris Sultani wako anaiingizia Mapato Serikali? Hivi hujui tu kuwa Makampuni haya ya Simu yanaitajirisha Serikali?

Siyo idris wangu! Hoja siyo idris wala pesa! Hoja ni USAWA WA KISHERIA. Kama nipesa basi hata idris asingelala lupango nakupelekwa mahakamani.

Simtetei! Natafta usawa wa kisheria na jisi watu wanavyoibiwa.
 
Hayo makampuni ya Simu kabla ya kutumia mawasiliano kutoka kwao unapaswa kufahamu vigezo na masharti yao! Matangazo ya Huduma zao ni kawaida! Ila matangazo na jumbe zingine waweza kulalamika au kuomba zikawa hazikufikii!

Ila kutumia laini ya mwingine wote wanasisitiza hairuhusiwi!
 
Siyo idris wangu! Hoja siyo idris wala pesa! Hoja ni USAWA WA KISHERIA.
Kama nipesa basi hata idris asingelala lupango nakupelekwa mahakamani.
Simtetei! Natafta usawa wa kisheria na jisi watu wanavyoibiwa.

Usawa ( Haki ) na Pesa kwa nchi nyingi za Kimasikini barani Afrika ambazo bado zinaongozwa Kibabe ( Kiimla ) ni Vitu viwili tofauti kabisa Ndugu.
 
Hayo makampuni ya Simu kabla ya kutumia mawasiliano kutoka kwao unapaswa kufahamu vigezo na masharti yao! Matangazo ya Huduma zao ni kawaida! Ila matangazo na jumbe zingine waweza kulalamika au kuomba zikawa hazikufikii!

Ila kutumia laini ya mwingine wote wanasisitiza hairuhusiwi!

Sasa haiiluhisiwi , sawa!kwa nini wanagawa line za watu?
Mbona wale wanitumie pesa kwa namba hii hawaishi?
Kulalamika nimeeleza kuwa nimelalamika sana lkn hamna kitu.

Nakumbuka sijalalamikia matangazo kutoka vodacom.
Matangazo yavoda yanaonekana nikutoka vodacom.

Nahoji hawa wa 5555
Na wa hadithi ya kuzimu! Nani kakwambia nataka hadithi ya kuzimu?
Nahawa wa nimeshinda bahati nasibu wakati sijacheza.

Ukisema niyakwao voda! Unamaanisha wao ndio wanatuibia?
Wao ndio wanasema tumecheza bahati nasibu tutume hela tukomboe zawadi?

Vodacom ni vodacom! Cjaingia mkataba na tatu mzuka wala mcheza kamari!
Wanawapaje namba yangu?
Ukilalamika hawachukui hatua.
 
Matangazo yavoda yanaonekana nikutoka vodacom...
Line si mali yako, wewe ni mpangaji tu, ndio maana ni rahisi kwa mwenye nyumba kukwambia punguza kelele ila wewe huthubutu.

Mbona tv ni yako na vipindi vya channel hupangi wewe na matangazo unatazama kama kawaida?

Acha hizo, hiyo ni platform ya matangazo kama platform nyingine.

Ukiambiwa jiunge upate mlio wa sauti, usijiunge. Mbona ukiambiwa KAMA KWELI UNAMPENDA UTAMLINDA hukimbilii dukani kuzinunua?

Acha hizo weweeee. Mwenye tangazo lake atapeleka kwenye mitandao na litakufikia tu. Hutaki, tengeneza mtandao wako.
 
Siyo tu hao hata baadhi ya staff wa tume ya utumishi wa umma wanawapa loan officers wa bank kadhaa. Mf.ABC nk. hususani wale watumishi wapya.
Makampuni ya simu yanatoa wapi power of Antony yakugawa.
1.line niliyonunua mimi kwa hela zangu.
2.line niliyosajiri kwa kitamburisho cha kitaifa tena kwa mujibu wa sheria?
3.line ambayo naweza kushitakiwa endapo nitampa hata baba yangu mzazi kuitumia?
4.line ambayo natakiwa kuitoa mimi mwenyewe kwa mtu yoyote?
5.line ambayo ni bank , ni bank ya siri kubwa ambayo hata mkewangu hawezi kuingia na kusoma vitu bila ridhaa yangu namimi siwezi fanya hivyo kwenye line ya mke wangu wao niakinani?
6. Line ambayo kila kukicha tcra wanasisitiza kutompa mtu simu kuitumia? Kwanini wao wanagawa?

Mwisho! Hivi sheria zetu huwa zinang'ata masikini na waganga njaa pekee?
 
Hujui una contract yenye terms and conditions?

Wewe umedandia mjadala bora ukae kimya wanaume wajadili.
Unaponunua line ya sim huwa kuna terms of contract za hivyo!
Pitia upya kusoma kijikitabu cha line yasim km kunahicho unachokisema.

Wewe utakuwa msukuma a.k.a nduhu tabu!
 
Line si mali yako, wewe ni mpangaji tu, ndio maana ni rahisi kwa mwenye nyumba kukwambia punguza kelele ila wewe huthubutu.

Mbona tv ni yako na vipindi vya channel hupangi wewe na matangazo unatazama kama kawaida?

Acha hizo, hiyo ni platform ya matangazo kama platform nyingine.

Ukiambiwa jiunge upate mlio wa sauti, usijiunge. Mbona ukiambiwa KAMA KWELI UNAMPENDA UTAMLINDA hukimbilii dukani kuzinunua?

Acha hizo weweeee. Mwenye tangazo lake atapeleka kwenye mitandao na litakufikia tu. Hutaki, tengeneza mtandao wako.

Mfano wako uliotoa ni mfano MFU! ila acha tukusaidie, vipindi vya television vinategemeana visimbuzi! Ndio maana mtu unachagua kisimbuzi utakacho kulingana na chanel unazozitaka!
Lakini pia huwezi kushtakiwa na mtu yyte ukiamua kumpa mtu yyte kisimbuzi chako tofauti na line.

Wala huwezi kuambiwa sajili kisimbuzi chako kwa kitambulisho cha nida km line ya sim.

Hivyo wewe unajadiri mjadara ambao uko juu ya uelewa wako, KAA KIMYA.
 
Yaani hata ukipata emergency huruhusiwi kutumia simu ya mtu basi serikali iweke public call za simu basi ili watu wawe wanatumia kwa kulipia
 
Sasa haiiluhisiwi , sawa!kwa nini wanagawa line za watu?
Mbona wale wanitumie pesa kwa namba hii hawaishi?
Kulalamika nimeeleza kuwa nimelalamika sana lkn hamna kitu.

Nakumbuka sijalalamikia matangazo kutoka vodacom.
Matangazo yavoda yanaonekana nikutoka vodacom.

Nahoji hawa wa 5555
Na wa hadithi ya kuzimu! Nani kakwambia nataka hadithi ya kuzimu?
Nahawa wa nimeshinda bahati nasibu wakati sijacheza.

Ukisema niyakwao voda! Unamaanisha wao ndio wanatuibia?
Wao ndio wanasema tumecheza bahati nasibu tutume hela tukomboe zawadi?

Vodacom ni vodacom! Cjaingia mkataba na tatu mzuka wala mcheza kamari!
Wanawapaje namba yangu?
Ukilalamika hawachukui hatua.
Suala la kugawa namba makampuni ya simu tutayalaumu bure ,hivi mimi kwa mfano nikiamua nitume ujumbe wa tuma hela kwenye namba hii ni mpaka niende voda au airtel nipate namba za watu ?si ninabuni namba tu meseji imfikie yeyote
 
unakuta kwenye namba yako ya simu imeingia hela, ndani ya muda mfupi unapigiwa simu au sms na mtu usiemfaham kua kuna hela imeingia kimakosa kwenye simu yako(utapeli). swali langu wanajuaje kama hela imeingia kwenye simu yngu ndani ya muda mfupi?
 
Mfano wako uliotoa ni mfano MFU! ila acha tukusaidie, vipindi vya television vinategemeana visimbuzi! Ndio maana mtu unachagua kisimbuzi utakacho kulingana na chanel unazozitaka!
Lakini pia huwezi kushtakiwa na mtu yyte ukiamua kumpa mtu yyte kisimbuzi chako tofauti na line.

Wala huwezi kuambiwa sajili kisimbuzi chako kwa kitambulisho cha nida km line ya sim.

Hivyo wewe unajadiri mjadara ambao uko juu ya uelewa wako, KAA KIMYA.
Mpe mtu hicho kisimbuzi chako halafu akifika huko aendako akichakachue kiwe na uwezo wa kushika mpaka channel za dstv, halafu kishtukiwe ndio utajua kama hicho kisimbuzi ni chako kweli au kina wenyewe. Utashtakiwa na mtafungwa wote kwa kosa la kula njama za kuibia kampuni husika(dstv/azam), soma mikataba iliyopo utajua kuwa wewe ni mpangaji aka mkodishaji tu, huna chako. Si line ya simu, si king'amuzi.
 
Back
Top Bottom