Ukishangaa ya Polepole usisahau kushangaa ya mwendazake na Mama



1. Unafahamu Job description ya mkuu wa wilaya? Unajua mkuu wa wilaya ana report kwa nani?

2. Maamuzi ya serikali yanafanyika kwenye vikao vya chama? So viongozi wa CCM wanaingia kwenye baraza la Mawaziri au vya watendaji wa juu wa serikali?

3. Msemaji wa sasa umemsikia anakemea maovu yoyote ? Au awamu hii hakuna maovu

4. Hapa unaongea in generally tu kwamba hata mjumbe wa nyumba kumi na yeye ni sehemu ya mambo maovu ya serikali
 
Hata mm limenishangaza ..sie watanzania ni wajinga na wepesi kudanganywa ...mara hii washasahau lowasa alichowafanya
 
Kamba haikuwa ndefu na pia walimchoka kila siku anaomba alete wakyuba bongo kwa msaada wa ufadhili wa Tanzania kuja kufundisha au kutibu, kwa gharama za bongo......
Kyuba ni choka mbovu ile mbaya, hata Bangladeshi inaafadhali....
wew bhana wewe kyuba njaa sana? kwamba kule kamba haifiki
 
Sitashangaa akifanya mwanaccm mwingine sarakasi za polepole tukaendelea kurukaruka kama mazuzu. Nimeona hata wapinzani wanashangilia kweli kweli na kumwona Polepole shujaa wao.🥺🥺🥺
Mko wachache sana wenye huu upeo

Wengi hamtuelewi… chakandumuz na wapinzani wengi hasa vijana wanachwza game ya chama dume

Utasikia February 2026 polepole anapewa nafasi ya uongozi

Siku tutakapoacha siasa za vyama na uhafidhina tutapona Kama taifa
 
Kwenye nchi hizi zetu masikini zilizokithiri ufisadi, ulafi, matabaka na ujanja ujanja mwingi, hakuna namna utafanikiwa kuongoza kwa kutumia demokrasia.
Ukiwa kiongozi sahihi na mwenye maono utalazimika tu kutumia udikteta ili kunyoosha mambo.
Ndiyo maana pamoja na risasi zake wananchi bado walimkubali JPM na wanammiss sana.
 
Wakati haya yanatokea Polepole alikuwa hana cheo chochote CCM wala Serikalini!!!
 
Hata mm limenishangaza ..sie watanzania ni wajinga na wepesi kudanganywa ...mara hii washasahau lowasa alichowafanya
Aliwaambia waviringishe mikono kuwa ndo mabadiriko yenyewe baadae akasema zake CCM
 
Wakati haya yanatokea Polepole alikuwa hana cheo chochote CCM wala Serikalini!!!
Inaelekea wewe ndo una wiki moja tangu umjue Polepole. Hata hujishughulishi kujua historia na mtu
 
abracadabra za POLEPOLE, ni HARAKAHARAKA

View: https://youtu.be/HK4ZQBXg6Xw?t=18
View: https://youtu.be/HK4ZQBXg6Xw?t=123
 
Sitashangaa akifanya mwanaccm mwingine sarakasi za polepole tukaendelea kurukaruka kama mazuzu. Nimeona hata wapinzani wanashangilia kweli kweli na kumwona Polepole shujaa wao.🥺🥺🥺
Polepole na Bashiru Ally ni mojawapo wa watu walioshirikiana na Magufuli kuinajisi demokrasia hapa nchini, wawili hawa ndiyo walikuwa madalali wa kununua wapinzani uchwara na walitajirika sana kwenye projrct hii haramu, hivyo huyu ni mhuni kama wahuni wengine tu wa CCM.
 
Alikuwa compromised!
Ndio za wazee wa zamani, kila kitu usalama wa taifa hata wauza kahawa walikuwa wanaitwa usalama wa taifa.....
nyerere hapa alikuna sana kichwa kwa CKT, na kumuweka kizuizini kila kukicha sababu siasa zake za kulazimisha kila mtu afuate anavyotaka yeye
 
Ngoja tukupe somo kidogo.

Utawala bila mifumo dhabiti ya nchi ni sawa na kuendesha gari bovu.

Msingi wa kuwa na mifumo dhabiti ya kiutawala ni Katiba na sheria.

Kama una katiba inayompa mamlaka makubwa Rais atafanya anachojisikia yeye na humfanyi chochote.

Matokeo yake kila kiongozi anaendesha nchi kwa utashi wake. Hakuna wa kumhoji. Lakini kungekuwa na mifumo imara ya Katiba na sheria hawezi. Uchawa unaouona sasa hivi ni matokeo ya Katiba na sheria mbovu.

Kwa hiyo ukisikia watu wanadai katiba mpya maana yake wana akili kuliko anayeaminishwa kuwa katiba ni kijitabu tu, bora ya Quran.
 
Hawa na mwendazake ndo walituletea terminologies hizi;
1. Wasiojulikana
2. Kuteka, na kuua watu.
3. Uchawa.
4. Tanzania ya mwendazake
5. Vita ya kiuchumi kwa kupiga risasi wananchi wake nk.
 
NALUDIA TENA CCM NI ILE ILE NA WATU NI WALEWALE..INGEKUWA HAO WOTE WANAYASEMA MANENO WANATAFUTA CHAMA CHAO BASI TUNGEWAJADILI KIVINGINE...HAPA CHAKUJIFUNZA NI CCM INATENGENEZA TATIZO HALAFU INAKUJA KUTATUA KIVINGINE.
 
NALUDIA TENA CCM NI ILE ILE NA WATU NI WALEWALE..INGEKUWA HAO WOTE WANAYASEMA MANENO WANATAFUTA CHAMA CHAO BASI TUNGEWAJADILI KIVINGINE...HAPA CHAKUJIFUNZA NI CCM INATENGENEZA TATIZO HALAFU INAKUJA KUTATUA KIVINGINE.
CCM ni chama chenye resilience ya hali ya juu, humfrey anaenda kuteseka sana, na vyama pinzani havimtaki maana alivifanyia ushirikina sana akiwa awamu ya 5
 
CCM ni chama chenye resilience ya hali ya juu, humfrey anaenda kuteseka sana, na vyama pinzani havimtaki maana alivifanyia ushirikina sana akiwa awamu ya 5
Watasema siasa haina adui wa kudumu. Lowasa alikuja na kuzungusha mikono eti ndo mabadiliko na baadae akatuacha akarudi zake .

Polepole atakuja na kuzungusha shingo, safari hii madaktari wajiandae kupokea wagonjwa wa shingo.
 
2 Wakorintho 5:17
[17]Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…