Ukisikia kua uyaone ndo haya sasa: Bhufakale dawa ya kuchelewa kufariki (kufa)

Ukisikia kua uyaone ndo haya sasa: Bhufakale dawa ya kuchelewa kufariki (kufa)

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
6,944
Reaction score
14,351
Habari za Leo mabibi na mabwana.

Mnamo 14/05/2024 tulimzika mzee mmoja kijijini kwetu jina (..)

Mzee yule alikuwa amemuoa shangazi yangu Mimi. Chanzo Cha kifo chake ni ugonjwa wa kisukari uliodumu Kwa muda mrefu.

Baada ya kuzunguka huku na huko na hospital mbalimbali kutafuta matibbu ya ugonjwa huu na kudanganywa na Kila aina ya wanatiba asilia kuwa wanaponesha.

Hatimae mzee huyu alizirudia tiba za hospital (vidonge).

Ikumbukwe mzee huyu kaugua kisukari zamani kidogo ni zaidi ya miaka 10 ana kisukari.

Hadi mwishoni mwa mwaka 2023 Hali yake ilizorota sana na kuandamwa na magonjwa mbalimbali.

Mapema mwezi wa kwanza mwaka huu walimpeleka sengerema mission na kupewa rufaa Hadi bungando.

Na walipofika pale wakakutana na bro yangu yupo hapo (Dr)

Baada ya vipimo kufanyika waliambiwa in,Figo nk havifanyi kazi Tena hivyo wakaambiwa warudi wasubiri lolote(kama mnavyojua kauli hii humanisha kifo)

Yule kaka akawaambia mlichoambiwa ni sahihi kuliko kusafirisha maiti ni Bora msafirisheni ingali Bado Yu hai.

Nifupishe kisa hiki

Mwezi wa pili baada kwenda kijijn nikaona ni Vyema na haki Nami nikamuone huyu mgonjwa.

Nikafika nikamkuta mgongwa anakula Kwa mrija ametibolewa hivyo uji unapita Kwa mrija na kukojoa pia anakojoa Kwa mirija.

Kwakweli Hali yake haikuwa nzuri Wala hakuna matumaini kabisa.

Daima ndg wa karibu walikuwa wanakaa hapo nyumbani wakisubiri Kila anaye Toka ndani awaambie lolote.

Niliondoka nikiwa najua kabisa Kwa Hali hii mzee wetu huyu siku3 hatoboi.

Mwezi wa 1 ukakata wa pili ukakata watatu na wanne pia ukaisha Ngoma bila bila.

Madaktari wenyewe walikuwa wanashangaa sana. Kila wanapokuja.

Ilifikia kipindi hata kula Hali Wala kunywa maji hanywi.

Lakini kufa hafi. Hadi tarehe 9/5/2024 Watoto wakakaa kikao wakasema jambo hili sio sawa jamani hii haiwezekani Wala hatujawahi ona.

Ndipo wakasema aitwe mmoja wa baba zao wakubwa kwenye ukoo wao nae ni mzee sana kwenye miaka 87+ Hivi.

Baada tu ya kufika pale wakamueleza Hali ILIVYO ndipo akawapa Siri hii..... ....

Akawaambia walichanjwa dawa inayoitwa "BHUFAKALE" Hii ni Kwa kisukuma tafsiri yake kufa zamani.

Ndipo wakaambiwa kuwa nendeni mkamtoe kwenye nyumba ya bati mwekeni kwenye nyumba ya nyasi mlazeni humo halafu mbomoeni (waezue zile nyasi juu ya paa)

Iwapo atapata mwanga wa jua tu(kivuli Cha jua) atakufa muda huohuo hatachukua muda na kama Hana hiyo dawa basi mtamrejesha kwenye nyumba ya bati.

Kweli baada ya kutoka huko hawakuchukua muda wakamtoa na kumuingiza jikoni maana ndo nyumba ya nyasi pekee ilikuwa imebakia pale.

Ilipofika saa 3 asubuhi ya tarehe 12 mzee akafariki ni baada tu ya kupata huo mwanga wa jua.

Hii ni ngumu kidogo kuamini wale wa Kwa mwamposa, Baraka, mzee wa upako, Malisa l, kiboko wa wachawi nk.

Mzee alikuwa mfugaji mkubwa sana.

Siku ya mazishi 14/5/2024

Nikabahatika kuonana na mzee mmoja wa makamo nikaanza ulizia hii imekaaje na Nini faida yake?

Aliniambia mengi lakini Kwa kifupi tu alisema kuwa

Wazee wa zamani walikuwa na Imani ya kwamba akiwa na hiyo dawa kwanza inaendana na Baraka na laana

Akikubariki amekubariki na utafanikiwa pia akikulaani wewe umelaanika yamkini hata ungeoga mafuta ya mwamposa Bado laana yake isingekutoka.

Pili akasema waliamini akichelewa kufa manake atakula mali yake vizuri Hadi anakufa kashabakiza kidogo tu.

Maana yeye anakuwa anajua kabisa kuwa huenda ugonjwa huu ndo utaniondoa ila Kwa sababu ya dawa hii niliyochanjiwa Wacha Nile Mali zangu.

Je ulikuwa unalijua hili mwana JF?

MWISHO.
 
Mzee alikuwa ameanza kuoza chumbani kwakwe palikuwa hakutamaniki
Ni yale maana kuna mzee nilimuona alikuwa na miaka zaidi ya 110 , walikuwa wanamtoa nje kweny jua kama wanamuanika kila siku .

Chumba anachokaa kinatoa harufu mpaka siku aliyokufa walifurahi sana , maana hata wajukuu zake walikuwa na wajukuu.
 
Back
Top Bottom