Ukisikia Watu Wanataja Neno “Faida” Usifikiri Ni Kitu Rahisi Kihivyo!

Ukisikia Watu Wanataja Neno “Faida” Usifikiri Ni Kitu Rahisi Kihivyo!

Economist Jay

Member
Joined
Feb 18, 2016
Posts
42
Reaction score
51
Neno FAIDA linasikika sana katika masikio ya watu kila siku, ni kati ya maneno ambayo hata kutamkika kwake ni rahisi. Kutokana na sababu hii watu wanavutwa sana wanaposikia kuwa faida inapatikana kwa kuuza kitu (bidhaa au huduma) kwa bei ambayo ni ya juu kidogo ikilinganishwa na kununulia bidhaa husika au ikilinganishwa na gharama za uandaaji wa bidhaa yenyewe hadi kufika sokoni.

Baada ya watu wengi kuvutwa na kuamua na wao kuwa miongoni mwa wale wanaouza bidhaa au huduma kwa ajili ya kutafuta kitu kinachoitwa ‘faida’, wengi wao hawajui ugumu uliopo hadi kuipata hiyo faida, pia hawajui namna gani ya kufanya kuweza kuipata faida hiyo.

Faida katika biashara haipatikani kirahisi kama wengi wanavyodhani, faida kupatikana kwake siyo rahisi kama neno lenyewe jinsi lilivyo, ni makosa makubwa kuingia biashara kuwa mkumbo, eti kwa sababu umeambiwa na wenzako kuwa kwenye biashara kuna faida.

Biashara ina tabia ya kuhudumia watu, kwa hiyo nazungumzia tabia za watu. Ili uweze kupata faida unapaswa kuhakikisha kuwa biashara yako imefikia hatua ya kulenga vitu vyote muhimu ambavyo mwanadamu anahitaji.

Kwanza kabisa unatakiwa kufahamu kuwa, jamii yetu haina pesa za kutosha, kwa kifupi watu wana vipato vya chini sana. Kutoka na na hali hii, kila mmoja huweka Mipango madhubuti ya kuhakikisha anatumia pesa yake vizuri bila kupoteza hata shilingi moja kwenye mambo ya hovyo hasa bidhaa au huduma atoayo mtu, kwa sababu anajua yeye ni masikini hivyo katika uchaguzi wa bidhaa za kununua anahitaji kuhakikisha vitu Fulani kwanza kwenye bidhaa yako ndipo afanye uamzi.

Pili, mahitaji ya binadamu hayana kikomo, lakini pesa ambazo mwanadamu anazimiliki zina kikomo, hivyo wateja au jamii iko makini sana na jambo hili maana uzembe wa kuchagua bidhaa ukifanyika, unaweza kupoteza pesa yake bila kumpa faida yoyote. Kumbuka faida ya mteja ni kile anachokipata kutoka kwenye bidhaa aliyonunua kwako.

Ukishafahamu kuwa wewe muuzaji unapambana na mambo ya binadamu ambayo hayana kikomo (human wants) lakini kile unachotaka kutoka kwao (pesa) kina kikomo basi suala la kutafuta faida ni suala nyeti sana kwako.

Katika mazingira hayo, tunajifunza kuwa usifanye biashara kama mzaha Fulani au kwa kutumia mazoea fulani ambayo wewe mwenyewe umeiga kutoka kwa wafanyabiashara wajinga.

Ili uweze kupambana na mwanadamu anayepangilia vizuri matumizi ya pesa yake, unatakiwa na wewe sasa uwe na Mipango ya kuhakikisha kuwa hiyo pesa yake inakuja kwako. Huwezi kupata faida kizembe kizembe tu eti kwa sababu una biashara. Kumbuka kuna biashara na wafanyabiashara majina tu, unatakiwa kuwa na bidhaa ambayo inamshawishi mtu na kuamua pesa yake kuileta kwako.

Je, wewe unafanya nini kwenye biashara yako hadi unishawishi Mimi kuwa bidhaa yako inanifaa na hata kama nikiacha pesa yangu kwako sitajuta nikifika nyumbani na kuanza kuitumia?

Mtu kutoa pesa yake kirahisi rahisi huwa haiwezekani, ndiyo maana wateja wengine wanaitwa wasumbufu katika biashara, kitu ambacho ni makosa kuwaita hivyo-eti wasumbufu!! Mteja anayehoji sana ni mtu ambaye anatendea haki asili yake, kwa sababu anaamini pesa ikishatoka mfukoni hairudi, hadi kukomaa tena kuipata. Sasa jiulize, ni nani yuko tayari kununua mashine mbovu ya kutolea nakala hapo kwenye duka lako kisha iharibike ahangaike tena kuitafuta?

Kama wewe ni mfanyabiashara, unathamini vipi pesa za wenzako? Unadhani pesa ya mtu unaweza kuichukua kwa kufanya biashara ya kijanja janja? Kwa kuuza bidhaa feki? Kwa kumfungia kaptura badala ya suruali aliyochagua eti kisa mteja kaangalia pembeni kidogo tu?

Faida inatokana na pesa wanazokuletea watu, na wewe ukawapa bidhaa, kwa hiyo thamini sana pesa za watu kama ambayo wao wamethamini bidhaa yako na kuamua kuleta pesa zao kwako.

Ili upate faida ya kweli na yenye matumaini katika biashara yako unatakiwa kuuza bidhaa za uhakika, usiseme kuwa eti na wewe uliuziwa hivyo, kwani wakati unakwenda kununua kwa watu wa jumla hukufanya udadisi kabla ya kununua ili kujiridhisha na ubora wa hizo bidhaa?

Faida Mara nyingi hupatikana kwa watu walio “serious” na biashara zao, kuanzia utafutaji wa mtaji, utafiti wa soko, udadisi wa ubora wa bidhaa, uandaaji wa mandhari ya sehemu ya biashara, motisha za wateja, na hata usajili wa biashara kulingana na ukubwa na aina ya biashara.

Bila kuwa “serious” na biashara yako maana yake ni kwamba unapoteza muda wako. Na hawa ambao hawako “serious” na biashara zao ndiyo hao mara nyingi huwahubiri watu huku wakisema kuwa biashara haina tija ni kupoteza muda, sasa unajiuliza! Anataka afanye nini hapa duniani? Kuishi kwa kuomba omba? Hayo ndiyo maisha yasiyo na hasara? Kila mtu anaishi kwa kuuza kitu (bidhaa au huduma).

Faida ipo tena kubwa sana katika biashara, faida hii huwezi kuiona au kuipata kirahisi, hadi uwe “serious” na biashara. Kuanzia leo usichukulie neno “faida” kama neno lilivyo unapokuwa katika biashara. Kama huioni hiyo faida kila Siku unapokwenda huko kwenye genge lako au sehemu yako ya biashara basi unatakiwa kujitafakari, kwa sababu faida ni lazima ionekane kwa watu wanaofanya biashara kwa maarifa yao yote.

Asante
0759708499
www.mgejwajr.com
 
Nini maana ya FAIDA?

Maana yake ni Jumlanya Mapato ukitoa Jumla ya matumizi.

Sasa ukipiga hapo hatabjibu ukipata 1000 hiyo ni faida na ni Progress kubwa.

Hata jawabu likija 50 hiyo ni faida tiyari.

Faida sio kitu kigumu ipo na watu wanapata kabisa.

Mama muuza vitumbua au.mama mkaanga mihogo wanazipata.

Kitu ambacho watu wanapigania ni SIPUER NORMAL PROFIT hii ndo huwa kazi kuipata
 
Back
Top Bottom