Kibunango wewe ndio unatakiwa ulete habari hizi ni ya kweli haya au hujapitapita...?
Mkuu Mwanakijiji
Tatizo siku hiz watu wanapenda uchonga sana, Wengine wameona bora kuingia JF kwa kuptia mlango wa Zenj, baada ya mazagazaga ya Bara kuwa mengi.
Kuhusu Michenzani, kuna Familia nyingi ambazo bado zinadai kupewa nyumba hapo Michenazani ya kubomolewa nyuma zao wakati zoezi zima la ujenzi wa nyumba bora kwa wakaazi wa Zenj. Na sasa Mhe. Karume anajaribu kuondoa tatizo hilo wa kumalizia nyuma za Michenzani ambazo zilianza kujengwa tokea wakati wa marehemu baba yake.
Katika awamu sita za uongozi wa SMZ ni awamu mbili tu ambazo ziiweza kuendeleza majengo hayo, na ni baada ya kupata misaada mbalimbali toka kwa wahisani.
Komandoo Salmin aliweza kuendeleza Majengo hayo baada ya kusaidiwa na Col. Gaddaf wa Libya, Zaidi ya kujenga nyumba hizo Mkuu huyo wa Libya alitoa misaada mingi mengine kama lami ambayo hadi leo inaendelea kutumika katika kukarabati na kujenga barabara za visiwani humo.
Mhe. Karume anaendeleza yale ambayo aliazisha baba yake na kuendelezwa na viongozi wengine katika SMZ. Umaliziaji wa Majengo ya Michenzani unatokana na msaada mkubwa wa Libya visiwani humo. Kwani SMZ haina ubavu wa ujenga nyumba hizo kwa bajeti yake yenyewe.
Kuna wakati ilipendekezwa kuwa ujenzi wa nyumba hizo ubinafsishwe, na hapo ndio China ikaanza kusikika katika kushiriki kwenye ujenzi huo. Hata hivyo wazo hili halikuweza kupata baraka za wananchi kwani sehemu kubwa ya ujenzi wa nyumba hizo ni kufidia wale ambao walibomolewa nyumba zao.
Michenzani ina sifa zengine zaidi kuna block moja ambalo lilimalizwa na Komandoo Salmin muda mfupi kabla ya Tanzania kiungia kwenye mfumo wa vyama vingi. Ili Komandoo ashinde uchaguzi wa kwanza aliamua kutumia block ilo kisiasa zaidi. Na ni pale alipoamua kuwapa Wapemba nyumba nyingi katika block hilo, badala ya kufidia wale waliobomolewa. Hadi leo block ilo linajulikana kwa jina la Pemba. Kwa waliofika Zenj block hilo lipo mita chache kabla ya kufika Mwembemadema polisi.
Wengi ambao wamepata nyumba hizi awaishi tena katika block hizo, badala yake wamekodisha nyumba hizo. Watea wakubwa ni wafanyakazi wengi wakiwa kutoka Bara na Kenya na wapo zaidi katika sekta ya utalii
Kutokana na aina ya ujenzi wa nyumba hizo, kulikuwa na upungufu mkubwa wa mahijati ya lazima kwa waakazi,hii ilipelekea awamu ya Komandoo kutoa ruhusa ya watu kuweka makontena katika eneo la Michenzani, ili usogeza huduma muhimu kwa waakazi wa apo na maeneo jirani.
Kuna kipindi watunzaji na wajenzi wa nyumba hizo walitoa ruhusa kwa waakazi wake kufungua maduka katika nyumba hizo, hii kwao ilikuwa ni sehemu ya vyanzo vya kodi ambazo hukusanya katika nyumba hizo
Uendelezaji wa Majengo ya Michenzani umeweza kutoa nafasi nyingi kwa wadau mbalimbali katika sekta ya Ujenzi visiwani humo. Asasi ya Utunzaji na Ujenzi wa Nyumba hapo visiwani, ndio wajenzi wakuu wa nyumba hizo(Main Contractor). Wazambazaji wa mahitaji ya ujenzi wapo wengi na hapa ndio maneno ya ajabu yanapo anzia.