Ukistaajabu ya Musa. Mashabiki wa Yanga wakana kuwa Simba siyo Makolo

Ukistaajabu ya Musa. Mashabiki wa Yanga wakana kuwa Simba siyo Makolo

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Wanasema tii sheria bila shuruti.

Kutokana na tuhuma zinazomkabili msemaji wa Yanga Ali Kamwe, mashabiki wengi wa Yanga wamejitokeza kumtetea huku utetezi mkubwa ukiwa eti hakuna timu ligi kuu inayoitwa Kolo au Makolo.

Tukumbuke Simba imeimbwa hadi katika nyimbo za Yanga kama Kolo au Makolo, leo hii ghafla bin vuu, hawaitambui hilo jina na wanakana halihusiani kabisa na timu ya ligi ya NBC. Wengine wanadai eti wanamaanisha Kolo ni katimu fulani huko mtaani. Kwa hiyo wanamaanisha Yanga ni level za timu ya mtaani maana mtani wake yuko huko, aisee!

Hii inamaanisha nini?

Je taratibu ufahamu umeanza kuwaingia hawa vyura kiasi cha kufuta kebehi na kejeli zao na badala yake kuipa heshima mabingwa watarajiwa wa NBC na CAFCC, Simba SC?

Muda haujawahi kushindwa na ni kitu cha kuheshimu sana.
 
Tutaita makolo kwenye maisha ya mtaani ikija kwenye sheria si hatujui hao watu, mbona sisi tunaitwa vyura au zaidi uto au utopolo mbona hatukunji ngumu!!

Hapa ukweli usemwe kijana ana PhD ya kukera maneno kama my wetu, wamegawa utamu mara saba ni maneno yanawauma sana makolo, kijana ana majivuno kwa timu yake kuwa na mafanikio makubwa na anajua kukera haswa hadi watu huko duniani wameshindwa kuvumilia wanamzushia kesi ili atoke wapumzike!

Kisheria hawatamuweza kijana maana ile sote tunaijua kama ni simba sports club kila mahali imejitambulisha hivyo kisheria kwahiyo ni kweli ligi kuu hakuna timu inaitwa kolowizard, kijana ni mshindi katika hilo watafute jingine, wakimfungia ana haki ya kuwashtaki Fifa na atashinda kesi asubuhi tu
 
Tutaita makolo kwenye maisha ya mtaani ikija kwenye sheria si hatujui hao watu, mbona sisi tunaitwa vyura au zaidi uto au utopolo mbona hatukunji ngumu!!

Hapa ukweli usemwe kijana timu yake ina mafanikio makubwa na anajua kukera haswa hadi watu huko duniani wameshindwa kuvumilia wanamzushia kesi ili atoke wapumzike! Na kisheria hawatamuweza maana ile ni simba sports club kila mahali imejitambulisha hivyo kwahiyo ni kweli ligi kuu hakuna timu inaitwa kolowizard, kijana ni mshindi katika hilo watafute jingine, wakimfungia ana haki ya kuwashtaki Fifa na atashinda kesi
Eeh huko huko mtaani vibaka pia wanakamatwa au unadhani mitaani ndiyo hakuna sheria?
 
Hawa vijana washamba sana.
Fifa wenye mpira wao wanasisitiza sana Fair Play.

Kuitana majina ya akina Haji Manara ni ushamba mno na kurudisha mpira wetu nyuma.

Manara amejaa Chuki, Hasira Roho mbaya nk

Binafsi siwezi kabisa kutumia majina kama...
1. Ma kolo
2. Utopolo.
3. vyura.
4. Wa mchangani.
5. Nyuma mwiko nk
Ni ushamba sana.
 
Hawa vijana washamba sana.
Fifa wenye mpira wao wanasisitiza sana Fair Play.

Kuitana majina ya akina Haji Manara ni ushamba mno na kurudisha mpira wetu nyuma.

Manara amejaa Chuki, Hasira Roho mbaya nk

Binafsi siwezi kabisa kutumia majina kama...
1. Ma kolo
2. Utopolo.
3. vyura.
4. Wa mchangani.
5. Nyuma mwiko nk
Ni ushamba sana.
Mwiko nyuma haikweoeki ni motto ya timu yetu
 
Back
Top Bottom