Ukitahiriwa umri wa miaka 18, inachukua muda gani kupona?

Ukitahiriwa umri wa miaka 18, inachukua muda gani kupona?

Hakuna tatizo ukitahiriwa ukubwani japo haishauriwi sana kuchelewa hii kitu.

Kama hauna maradhi kama kisukari wiki mbili adi 4 unakua poa kabisa mkuu, ila sasa ni marufuku kuwaza ngono maana mnara ukisoma tu jua kidonda!

Vyakula, piga supu za adabu, matunda na maji yakutosha kama unavuta sigara aina zote pole na kali sitisha mkuu pamoj na pombe. Hii ni kwa manufaa yako tu

Haya kila la heri mkuu, ila usione soo unezajiopolea na kanesi mchumba huko huko, [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mimi nimetahiriwa nikiwa na 23, wala hakuna aibu ya hiiivo, kama wanavyoiweka hao wanaume wa dar. Na ilikua ni maamuz binafsi wala co msukumo wala nn. Mwezi mmoja nikawa nimerudi kwenye hali yangu.
Nenda hospital unayopenda ufanyiwe na waambue tu unataka huduma ya kutahiriwa, kila kitu kitakua sawa.

I bet wew ni ngosha mtani kama si Akwiii...[emoji2][emoji2]
 
Huchukua wiki mbili hapo kupona Uzi unaanza kutoka chenyewe mpk kumalizika km wiki ya 4 hivi! Ila maji isiguse kidonda kwa wiki mbili zote!

Usiwaze mambo km yale yanayosababisha uume kusimama utaumia sana!! Ndani ya wiki ya pili utaweza kutembea na Uzi hata kama haijatoka!

Kukutana kimwili na mwanamke baada ya mwezi na wiki 3 hapo waweza kutana na mwanamke vizuri tu!
 
Nenda fasta kalitoe. Mi nililitoa nikiwa nakaribia 29, na nikafanya mapenzi siku ya 13 baadae. Isikutishe lakini jiandae kisaikolojia, zile siku tatu za mwanzo utaskilizia. Usiku lazima udindishe, na hapo nyuzi zinajikaza sawasawa. Ila ukiamka ukapigwa upepo basi linalala.

Sent using Jamii Forums mobile app

[emoji38][emoji38][emoji38] kwa huu ufafanuzi kwel mkuu una uzoefu [emoji38][emoji38]
 
Aibu lakn kutahiriwa ukubwani pole sana kwa kuchelewa kukatwa
Hakuna aibu yoyote ni mitazamo potofu tu kuhisi mtu akiwa hajatahiriwa ni dosari.

Kiuhalisia mtu ambaye hajatahiriwa yupo na kiungo cha asili cha mwili wake na hakuna uhusiano wowote kati ya kutahiriwa na kuwa na dosari ya kimwili. Sababu ya kutahiri ni kufanyia usafi mwili wako ila unaweza kubakia hivyo hivyo kama tu utazingatia usafi wa kusafisha hayo maumbile yako kwa wakati.

Na kuhusu kuchelewa kutahiriwa, watu hutahiriwa wakiwa bado wadogo kwasababu katika umri huo huwa wanakuwa homoni za kuasimamisha kadudu zinakuwa bado hazijachangamka sana. So dogo akitahiriwa kidonda hupona kwa haraka tofauti na mtu ambaye amebalehe ambaye kila akiamka kitu kimesimama sasa nyuzi zitakuwa zinakaza maana wakatati anashonwa dudu inakuwa imelala sasa imagine akiamka halafu ikadinda atakuwa kila wakati analia mwenyewe na kutoka damu mana nyuzi zitakuwa zinavuta na kuchana ngozi na vidonda kuanza upya.

So kama yupo comfortable kuishi nayo ni sawa tu maana hata wanawake nasikia wanapenda sana mtu mwenye ile kitu na kama utakwenda hospitali basi itabidi ujiandae na hilo balaa la kusikilizia maumivu.

SONY Xperia Z5 Premium
 
Kama ni hizi za hospitalini ni miezi tatu tu umepona ila kama ni ile ya kavu kavu ni miezi 6 ila utakuwa powa kabisa miezi 8. Kuhusu chakula kikubwa ni kula vyakula vya mafuta kwa wingi na hasa nyama nyama na mtori kwa wingi. Kikubwa zaidi pima kwanza kama umeathirika usikubali kutahiriwa maana wengi nliowaona wamefanyiwa hivo wakiwa na Uathirika walikufa. Usiogope kupona utapona haraka tu ni mambo ya kawaida
 
Mimi nimetahiriwa nikiwa na 23, wala hakuna aibu ya hiiivo, kama wanavyoiweka hao wanaume wa dar. Na ilikua ni maamuz binafsi wala co msukumo wala nn. Mwezi mmoja nikawa nimerudi kwenye hali yangu.
Nenda hospital unayopenda ufanyiwe na waambue tu unataka huduma ya kutahiriwa, kila kitu kitakua sawa.
Naombaa nipe maelezo ya Kutoshaa mkuu
Maelezo kama yapi mkuu kua huru. Hili c jambo la ajabu.
 
Inategemeana na dawa utakazotumia na hali ya usafi wako na pia hali ya hewa. Lakini haizidi wiki 2
 
Back
Top Bottom