Ukitaka Kufanikiwa Soma Hii..

Ukitaka Kufanikiwa Soma Hii..

Ryzen

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2012
Posts
7,301
Reaction score
8,706
Bwana Mmoja alikuwa akiuza chumvi kila siku, biashara yake ya kuuza chumvi aliifanikisha kwa kutumia Punda wake..
Katika njia yake ya kwenda sokoni kuna mto huwa anavuka, kwa bahati mbaya siku moja Punda wake akadumbukia kwenya Kijito hicho, Chumvi ikayeyuka (Dissolved).. Basi ule mfuko aliobebeshwa Punda ukawa Mwepesi sana na Punda yule akafurahi sana..
Punda Baada ya Kugundua kumbe Mzigo anaobebaga akidumbukia nao majini huwa mwepesi akaamua kufanya hiyo janja kila siku, akawa anajiangusha kwenye hicho Kijito kila siku..
Bwana yule muuza Chumvi akaja akagundua janja ya ya punda wake.. akawaza namna ya kumpa funzo punda wake..
Huyu Bwana akaona wacha safari hii ambembeshe Gunia la Pamba, kufika kwenye kijito kile yule Punda akajidondosha Makusudi Kama Kawaida Yake.. Kama Mjuavyo Pamba inanyonya Maji.. Basi lile Gunia likawa zitoo Mno kwa Punda yule..
Punda akajifunza Somo Pale..

Tunajifunza nini Hapa?.. Katika Maisha watu wengi tunategemea saana Bahati ..(Kama Punda alivyoanguka kwenye kijito na chumvi kuyeyuka bila yeye kutarajia)..Bila kujishughulisha kwa Uaminifu na pia sio Kila mara Tunaweza kuwa na Bahati.. Mara Pengine tuwe waaminifu na Wachapa Kazi..

Muwe na Jumapili Njema Ya Dominika ya 18 ya Mwaka B wa Kanisa..
#ChristusEleison

Architectus!
 
Back
Top Bottom