Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
swali kwako--- kinachokuza lugha ni maneno mapya ama wigo wa uongeaji(matumizi ya ) lugha husika?
Kiini cha lugha ni nini? Ni maneno au ishara ambazo watu hutumia kujieleza ama kuelezea mawazo, fikra, na hisia zao baina yao.
Kwa hiyo, kinachokuza lugha ni matumizi ya misamiati ya hiyo lugha lakini uongezekaji wa misamiati mipya nayo hukuza lugha.
Nyongeza yoyote ile ya kitu chochote kile hukuza kitu hicho!
Kwenye kamusi za Kiingereza, kwa mfano, kwenye baadhi ya maneno huwa wanaweka na miaka ambayo neno au msamiati ulianza kutumika/ulipoingizwa kwenye kamusi.
Kwenye Kiswahili hilo sijaliona bado.