Ukitaka kujuwa kuwa kiswahili hakijitoshelezi sikiliza 'Clouds FM'

swali kwako--- kinachokuza lugha ni maneno mapya ama wigo wa uongeaji(matumizi ya ) lugha husika?

Kiini cha lugha ni nini? Ni maneno au ishara ambazo watu hutumia kujieleza ama kuelezea mawazo, fikra, na hisia zao baina yao.

Kwa hiyo, kinachokuza lugha ni matumizi ya misamiati ya hiyo lugha lakini uongezekaji wa misamiati mipya nayo hukuza lugha.

Nyongeza yoyote ile ya kitu chochote kile hukuza kitu hicho!

Kwenye kamusi za Kiingereza, kwa mfano, kwenye baadhi ya maneno huwa wanaweka na miaka ambayo neno au msamiati ulianza kutumika/ulipoingizwa kwenye kamusi.

Kwenye Kiswahili hilo sijaliona bado.
 

Asante sana mkuu, sina la kuongeza kwani yote umeshayasema!
 
Sasa ingaliitwa MAWIMBI RUDIA MAWINGU huoni kama watu wangechoka kuitamka, au hata kuiogopa !!

yapo maneno mazuri ya kiswahili kama vile RONGOYA TABORA, RONGOYA MAWINGU n.k inapendeza sana tujivunie lugha yetu wadau, hata waingereza walitumia nguvu sana kuisambaza lugha yao ya kiingereza mfano walipo ingia afrika ya kusini walilazimisha wazawa kuizungumza lugha hiyo ya kiingereza.hivyo nasi tuitilie mkazo, JE MNAFAHAMU KUWA LUGHA YA KISWAHILI INAFUNDISHWA HATA UINGEREZA? TAFAKARI HILI!!!!
 
Duuuuuuuuu!!!!!!!!!! NIMESIKITIKA SANA KUSIKIA ETI KISWAHILI LUGHA YENYE THAMANI KUBWA, LUGHA AMBAYO ILITUMIWA NA BAADHI YA WAASISI KAMA MWL. JK NYERERE KUTUUNGANISHA NA KUWA HAPA TULIPO LEO ETI HAIJITOSHELEZI!!!! HUU NI UTATA WA KUTUPOTOSHA KAA CHINI NA UFIKIRI MCHANGO WA KISWAHILI!!!!! LUGHA IPI ILITUMIKA KUTUUNGANISHA TUKAPATA UHURU? SI KISWAHILI? SEMA MBONA KIMYA? TAFAKARI KABLA YA KUWASILISHA HOJA YAKO!!!
 
JF is the home of GREAT THINKERS. Kujitosheleza ni pamoja na MATUMIZI yake ndugu. Hebu nieleze ipi ni sahihi kati ya 'tunatoa huduma saa 24' au 'tunatoa huduma masaa 24'? Vile vile nipe tafsiri ya 'college, institutes (medical, technical, etc), polytechnic, vocational centers, university na kadhalika.
Je ni tafsiri sahihi ya Regional/District Commissioner kuwa Mkuu wa Mkoa/Wilaya?
Nasisitiza TAFSIRI na sio MAANA yake.
 
ukikitia mafuta kitapanuka
 
Sawa kabisa mtaalam.
 
Usisikitike hivo ndugu bali LAUMU waliopewa dhamana ya kikikuza. Mie nilielezwa kuwa Wajerumani haswa ndio WALIOKISAMBAZA Kisawhili Tanganyika (na sio Kijerumani lakini alipoingia Mwingereza yeye alitilia maanani lugha yake) wakati wakitutawala ndio maana Baba wa Taifa alipata nafuu ya kukitumia kuwaelewesha wananchi maana ya UHURU.
Tatizo nililonalo ni kuona wale waliopewa dhamana ya kukikuza hawafanyi hivo, hebu fikiria kama tokea uhuru kiswahili kingeondokana na Uarabu/Uingereza badala yake kingekuwa na mchanganyiko wa Kinyamwezi, Kigogo, Kiha, Kingoni, Kimaasai, Kinyaturu n.k. radha yake ingekuwaje? Katika vitu vizuri alivotuachia Baba wa Taifa letu tunavomuenzi ni pamoja na neno NG'ATUKA. Ikiwa yeye aliweza je hao wanaopata mshahara kila mwezi wanashindwa nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…