Ukitaka kulimaliza Taifa lolote zimalize Taasisi hizi 4. Kagame yuko sahihi kutudharau Watanzania

Ukitaka kulimaliza Taifa lolote zimalize Taasisi hizi 4. Kagame yuko sahihi kutudharau Watanzania

Mtanikumbuka 🐼

Kagame ni mchumba tu
General Paul Kagame amezungumzia mgogoro wake na Congo. Moja ya vitu alivyovisema ni kwamba wale wote ambao wanaamini kwamba wanaweza kuitishia Kigali wakiwa mbali anao uwezo wa kuwafuata hukohuko makwao.

Akaendelea kusema kwamba, wale waliokuwa wanaiunga mkono serikali ya Congo, Rwanda iliwasamehe na kuwaacha wapite nchini Rwanda na kurudi makwao. Katika watu ambao waliruhusiwa kupita Rwanda ni pamoja na askari wa JWTZ ambao kuna video inaonesha wanasachiwa ili kurudi nyumbani.

Paul Kagame amesema, kama wale wanajeshi wangethubutu kutunisha misuli bila kusalimu amri basi wangeangamizwa wote. Tena kama kuna wengine wataendelea kufikiria kwamba wataitishia Rwanda basi watafuatwa hukohuko makwao.

Maneno ya Dikteta Paul Kagame yameanzia dakika ya 14 ya hii video niliyoambatanisha hapa. Ni ujumbe wa vitisho kwa mataifa ya SADC, ikiwemo Tanzania, Malawi na Afrika Kusini.

Kuna msemo husema hivi, "Usipokuwa makini, hata mbwa atakucheka"

Povu Ruksa, Karibu Sana......
 
Ukimsikiliza Kagame anavyozungumza hivi sasa, unaelewa kabisa huyu mtu anawajua majirani zake inside out kiasi ambacho hawawezi kumwambia chochote au kufanikiwa kumfanya chochote.

Ukimsikiliza Kagame vizuri utaelewa kuwa, kwa sasa anajua kabisa kuwa Tanzania ni Taifa ambalo limeshajifia kimfumo, kiasi ambacho mifumo yake inaingilika na iko wazi kutokana na kuendeshwa na siasa na Wanasiasa badala ya Wataalam na Utaalam.

Taifa lolote imara duniani linafanywa kuwa imara na uimara wa Taasisi zake kuu 4 ambazo ni Idara za Ujasusi wa Ndani na Nje, Mahakama, Jeshi la Ulinzi na Utumishi wa Umma.

Ukifuatilia mwenendo wa Tanzania kwa takribani miaka ishirini sasa utagundua kuwa, Taasisi hizi Kuu ambazo ndizo zingepaswa kulifanya Taifa letu liwe imara zimekuwa compromised na Chama cha Mapinduzi.

Taasisi hizi sizo zinazoamua mustakabali wa Taifa letu, Sera zake, Uchumi na Maendeleo yake bali zimedhibitiwa kabisa na Chama cha Mapinduzi ambacho ndicho kinachoamua mwenendo na Utendaji kazi wa Taasisi hizi.

Sio hivyo tu, kutokana na kuhodhiwa kwa Taasisi hizi, maamuzi na ushauri wa kitaalam wa Taasisi hizi kwa nchini Tanzania umekuwa ukiangalia maslahi mapana ya CCM ili kuhakikisha kinaendelea kuwa madarakani na kutawala hili Taifa badala ya kuangalia mustakabali mpana wa Taifa letu na Wananchi wake kwa miaka mingi ijayo. Hii ni kwa sababu uteuzi wa Viongozi wa Taasisi hizi umekuwa ukizingatia unyenyekevu wao kwa Chama cha Mapinduzi na Viongozi wake ila sio umakini, weredi, uwezo wa kiakili na uwezo wa kiutendaji.

Ni bahati mbaya sana watu mbalimbali waliowahi kuonya kuhusu haya kwa kulazimisha mfumo wa nchi ubadilike kwa kuipatia Tanzania Katiba Mpya iliyo bora walikuwa wanadharauliwa sana na kuitwa majina mbalimbali ikiwemo kuwashawashwa na kuambiwa kila zama zina majira yake hivyo watulie tu.

Inaelezwa pia kuwa, kwenye Taasisi hizi, Viongozi walioonekana au wanaoonekana kufanya kazi kwa kuzingatia misingi na kusema ukweli bila hofu kwa vipindi tofauti wanaondolewa kwenye nafasi zao na kuwekwa wale wasiohoji na wanakubalina na kila kitu kwa Maslahi ya Chama cha Mapinduzi na Viongozi wake wala sio maslahi ya Taifa.

Kwa Tanzania ya leo sasa, Idara zake za Ujasusi ni kama zimekufa. Kwa maneno ya Kagame kuwa wanajeshi wake wanaweza kutembea kilomita 2000 kushambulia maeneo ambayo mnayatumia kutushambulia ilimaanisha kuwa mifumo yake ya Ujasusi kwa sasa inaweza kufika Dodoma kwenye Ofisi Kuu za Serikali au hata Dar es Salaam kwenye Ikulu kongwe zaidi na Taasisi zetu nyeti za kifedha na kushambulia.

Naionea huruma sana Tanzania.

Sasa tunavuna mavuno ya kuwaendekeza kwa muda mrefu Wanasiasa kuwa juu ya mifumo na Utaalam.

Rest In Peace Tanzania.
Jibu ni ...kutokuwapa waislamu uongozi ..nilisha imba sana hapa
 
Unapambana sana kuidogodesha nchi kubwa ya Tanzania mbele ya hicho kijiji.
Tanzania ni kubwa na huwezi kufananisha na hiyo failed state.
 
hizi maneno anazoongea kagame ni ujinga wa mwisho kabisa

kagame anajijengea chuki na majirani zake

siku wakijiunga kagame anabanikwa kama kuku wa kuchoma

anaongea sana,sio strong kama anavyojitapa huyu matako
Anakina nani wa kuungana?
 
Back
Top Bottom