Ukitaka kumkopesha pesa ndugu yako hakikisha mnakumbatiana kabisa

Ukitaka kumkopesha pesa ndugu yako hakikisha mnakumbatiana kabisa

Ndugu hakopeshwi..

Ukweni hakukopeshwi..

Mpenzi au mke hakopeshwi..

Mwanafunzi hakopeshwi ...

Baba na mama usiwakopeshee
 
Tusipromote roho mbaya.Sio ndugu wote.Hebu ujikute umebanwa sehemu huna hata buku halafu umkope ndugu yako akunyime uone utakavyoumia.Tusigeneralise.
Weka vitu ktk uhalisia huwezi kwenda kumkopa nduguyo 1,000/= akunyime hiyo ungeweza kumuomba rafiki yako kwa ndugu utaenda kuanzia 50,000/= ambayo ukiwa na shida utaahidi hata mwezi haupiti utailipa.

Lakini mwezi utapita hujalipa na kadiri atakavyokuwa anakukumbusha utamuona anakusumbua simu usipokee um-block huku ukimsemea kwa ndugu zako wengine jinsi jamaa alivyo na roho mbaya kisa kukumbusha hela yake,usituone walevi kwamba tunajiandikia tu hapa ni mambo yametukuta nina ndugu yangu mtoto wa baba mkubwa ana 600K yangu amefikia kuniambia nikitaka nikafungue kesi nimfunge ila hela yangu atanipa wakati anaotaka yeye huku wakati nampa aliniambia kuna sehemu amemaliza mradi anasubiri kulipwa wiki haipiti hela yangu analeta leo nahesabu mwezi wa kumi.
 
Wanajukwaa kama mnavyojua kumkopesha pesa ndugu yako lolote linaweza kutokea hivyo hakikisha mnakumbatiana kwa mara ya mwisho.....

NB; Usimkopeshe ndugu yako pesa bali mpe kabisa
Iko hvi akitaka umkopeshe laki mbili unamwambia ntakusaidia 50k ila laki mbili Sina...unamnyima mkitindo Yani hizo ni kutakana lawama ukimkopesha umekwisha
 
Weka vitu ktk uhalisia huwezi kwenda kumkopa nduguyo 1,000/= akunyime hiyo ungeweza kumuomba rafiki yako kwa ndugu utaenda kuanzia 50,000/= ambayo ukiwa na shida utaahidi hata mwezi haupiti utailipa.

Lakini mwezi utapita hujalipa na kadiri atakavyokuwa anakukumbusha utamuona anakusumbua simu usipokee um-block huku ukimsemea kwa ndugu zako wengine jinsi jamaa alivyo na roho mbaya kisa kukumbusha hela yake.
Buku nimetolea mfano tu jinsi utakavyokuwa umepigika halafu umuombe nduguyo msaada akunyime eti kisa ndugu akopesheki.Inauma aise.Au unisaidie huku una mashaka na mimi nduguyo.Ndio maana nikasema hebu vaa uhusika ndio ww una shida ya hiyi 50000/= halafu nduguyo ajakupa 30000/= eti kisa hana uhakika kama itarudi.Basi hapo hamna undugu.Ni undugu wa mashaka.
 
Kukopesha ndugu/rafiki ni kupoteza ndugu/rafiki na pesa.
kunae Rafik yangu kila siku hana pesa inatumika yangu nikishik cm yk kuangalia sms nakuta sms ya tigo pesa anafanya miamala tu iliniuma sana

mbaya kuna siku kaniomba pesa kumbe anataka kumtumia demu wake nikaona sms duh 🙄
 
Ukiona mtu yeyote amekuja kukopa alafu kulipa kageuka mbogo jua huyo yupo na changamoto,

Kuna baadh ya familia zinajua nn maana ya pesa,

Wanakopa na kulipa,

Ukiona mtu halipi huyo hajui nn maana ya pesa
 
jino kwa jino jicho kwa jicho



kazi kweli kweli/jobtruetrue
 
Back
Top Bottom