Kuna watu tabia zao ni mbovu hata kabla hajaoa wala kuolewa, Kwahiyo akiingia ndoani hakuna kitakachobadilika.
Hamjawahi sikia mtu anaambiwa yaani huyu kwa tabia zake sijui ataolewa/atamuoa nani. Sasa anatoka mtu huko hawajuani… hayawi hayawi kaolewa/kaoa. Shida walizokuwa wanazipata ndugu, jamaa, marafiki na majirani anahamishiwa “mwenza” na anatakiwa adeal nazo to the rest of his/her life. We kuweza??
Kuna watu wanatabia ngumu nyie acheni, sisi kuna shoga etu anaitwa M****** huwa tunamwambia M******* we utakuwa mchawi si bure!! Msichana ana tabia mbovuuuuuu! Mchoyo, msengenyaji, mchafu, mbinafsi, ana mdomo, mzururaji, controlling, manipulator, she knows it all , muongo kila kitu kibaya yeye, hanaga jema yule dada.
Sasa mtu kama huyu aolewe kweli jamani huyo shemeji hamna rangi ataacha ona.