Ukitaka kumwambia mtu pole kwa kingereza, utasemaje?

Ukitaka kumwambia mtu pole kwa kingereza, utasemaje?

Halo JF habari mchanganyiko.

Juzi nilikuwa na watasha ama wazungu sehemu. Moja alikanyanya jiwe dogo na kuteleza nusura aanguke.
Nilishindwa kabisa cha kuongea kwa kumpa pole baada ya neno pole kunitoa ushamba.

Ukitaka kumwambia mtu pole kwa kingereza utasemaje?
Inategemea situation ... Kama amefiwa sema "My condolences" au kama ikikushinda sema "I am sorry for your loss" ... Kama ameumia au anaumwa sana sana anayeumwa sema "Sorry, get well soon" na kuumia sema "Sorry, hope you are ok?" ... Kama umebeuwa au cheuwa au kufanya kitu cha kujiabisha sema "Excuse me" au "Pardon me" ... Lakini all in general sema "Sorry"
 
Umeona ?
Screenshot_20190728-173313.jpeg
 
kwa kingereza changu cha kwenye moovie natumia sorry japo nijuavyo sorry ni samahani....tusubir wazee wa language


Sorry, ni samahani pia ni pole, inategemea tukio, mfano anakuja mtu ili umsaidie jambo na wewe hutaki au huna uwezo wa kunsaidia, unaweza kumjibu; " I am sorry I can't help you", yaani nasikitika/samahani/pole siwezi kukusaidia. Hili ni neno la kuonyesha masikitiko unaposhindwa kumsaidia mtu kulingana na mazingira uliyonayo.

Sorry, inatumika kama pole pale ambapo mtu amepatwa na masahiba mfano; kuumia, kufiwa nk.

Unaposema; pole (nasikitika) kukujulisha kuwa rafiki yako amefariki, utasema; I am sorry to tell that your friend has passed away.

Kwahiyo, Sorry ni samahani/sikitiko pia ni pole.

Excuse, nayo ni samahani, hii inatumika pale ambapo unakusudia kuwavurugia watu mambo yao, mfano watu wapo kwenye sherehe yao na wewe unataka kwa muda huo waache sherehe yao na wakusikilize wewe juu ya jambo lako hapo utapaswa utoe "excuse" na ndipo utaeleza jambo lako.
 
Wengine za kwenye move huwa nasikia "my condolence" kama mtu ka RIP
 
Back
Top Bottom