Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Kwema Wakuu!
Nipo kwenye kumi la tatu. Lakini Watu wengi wanapokutana na mimi hushindwa kukadiria umri wangu na wengi huniona nina umri mdogo. Yaani huniona kama nipo chuo hivi au nimezaliwa miaka ya 2000 jambo ambalo sio kweli.
Nimeandika hivi kwa wale ambao wanataka miili yao isichoke mapema, yaani Forever young.
Hivi ñdivyo ninavyoishi;
1. Sinaga chuki wala kinyongo na mtu.
Moyo wangu unaamani siku zote. Utakapokutana na mimi basi asilimia 90 utanikuta naongea kwa furaha, tabasamu na utani wa hapa na pale.
Wengi huniita mpole, muungwana, na nisiyependa vurugu. Uzee wa mtu huanzia ndani. Moyo uliojikunja huzeesha pia mwili. Kuwa na furaha, furahia Scripts zako ulizoandaliwa na aliyekuumba. Usichukulie mambo too much serious. Hata hivyo usiwe mpuuzi na mzembe. Fanya kila kitu kwa uwezo wako bila kuwa na matarajio makubwa.
2. Usile vyakula vinavyoharibu mwili
Kama pombekali, viungo vikali vya chakula. Usiweke chumvi nyingi. Usile sukari nyingi.
Napendelea vyakula vipikwe kienyeji.
Kula protein zaidi kuliko wanga. Protini nikama maharagwe kwa jamii yake, maziwa, dagaa, samaki, nyama n.k. hicho ndio kiwe chakula. Wanga utumie kidogo sana yaani kaugali kawe madogo. Ushauri huu ni kwa wale ambao kazi zao hazihitaji nguvu nyingi. Kama yangu ya kukaa ofisini na kuandika andika,kusimamia wengine na biashara.
3, Kunywa maji mengi.
Kilo zangu zinanitaka ninywe Maji lita tatu kwa siku. Napiga lita maji kwa kiwango hicho.
Ngozi yangu iko njema kabisa. Kuumwa sio rahis magonjwa kama kichwa sijui mafua nimesahau.
Zingatia kuumwa pia huchangia kuzeeka na mwili kuchoka kwa haraka. Maji hufanya seli za mwili kufanya kazi zake vizuri. Ni vizuri ujiwekee rariba ya maji. Ujazo wa damu upo vizuri juzi nilipocheki body checkup zilikuwa lita 15.6.
4. Nina mke mmoja na sifanyi ngono zembe. Ngono zembe hufanya mwili, hisia na akili kuçhoka.
Kitendo cha kuwaza ku-cheat na kufanya uzinzi kinazeesha kwa sababu ni mwanzo wa kukosa amani na furaha ya nafsi na kwenye familia. Uaminifu ni moja ya mambo yatakayokufanya usizeeke kwa haraka.
Migogoro ya kifamilia hasa inayotôkaña na mambo ya usaliti huzeesha kwa sababu huwezi kuishi kwa amani baada ya usaliti.
Nilichagua binti mmoja mkali, mrembo aliyenyooka karîbu kila idara. Nikatulia zangu.
Chagua binti mzuri au kijana mzuri kulingana na vigezo vyako. Undeni familia. Fanyeni maisha. Epuka ngono zembe. Au kuishi kihuni.
Elewa kuwa usaliti wa mara moja huondoa uaminifu milele zote. Uaminifu ndio kitu pekee ambacho kikivunjika hakiwezi kurudi kama zamani. Upendo unarudi lakini uaminifu noop!
4. Pumzika kwa Wakati,
Lala muda wa kutosha hasa usingizi wa usiku. Kupumzika ni sehemu ya kuzipa nguvu na muda seli zako kûjizalisha upya. Kumbuka mwanadamu hukua na kuendelea kulingana ña seli za mwili wake. Kila unachokiona mwilini mwako ni matokeo ya seli. Kuanzia ngozi, nywele zako, nguvu ya macho kuona kusikia n.k.
Pumzika vizuri, lala vizuri, kula vizuri. Matunda na mboga kwa wingi. Kupumzika ni pamoja na kutafuta furaha kwa wengine. Kusamehe wengine na kujisamehe ni sehemu ya kupumzika.
Kupunga hewa safi salama ni sehemu ya kupumzîka. Furahia na wengine. Kama kuna mtu unajua unamtesa mpumzishe. Kupumzisha wengine ni kujipumzisha
5. Pendelea kufanya vitu vinavyoichangamsha akili yako.
Hakikisha akili yako isiwe imepooza. Tafuta game la kutumia akili cheza. Soma vitabu hasa riwaya,
Cheza Draft,
6. Jifunze mambo mapya.
Mimi nilijifunza Martial Arts, kuogelea na kulenga shabaha. Yapo maeneo hapa mjini yanatoa mafunzo mbalimbali. Hakikisha mafunzo unayoenda kujifunza ni by doing yaani kwa vitendo sio kushikishana madaftari.
Sio lazima hivyo nilivyovitaja. Yapo mambo mengi ya kujifunza kulingana na mazingira iliyopo.
Kujifunza mambo mapya huufanya mwili usizeeke kwa upesi kwa sababu ubongo unakuwa active.
7. Usitamani kuwa nà Maisha ya MTU mwingine.
Andaà mark scheme yako. Roadmap yako. Vile utakavyoishi. Usiwe mjinga WA kutamañi maisha ya wengine.
Maisha uliyonayo ñi mazuri kama ukijua kuyafurahia na kuyafanyia modification.
Moja ya dalili kuwa unatamaa mbaya na huenda utazeeka mapema ni pamoja na kuchukia mafanikio ya wengine. Kuumizwa na kwenda kwa miaka yako huku ukijiona hujafanya lolote.
Hujafanya lolote kwa sababu unàtaka kufanya kama wanavyofanya wengine.
Hapo ulipo unaweza kufanya jambo n. Watu wàkakuona kama unatija kwenye jamii yako. Chochote utakachoamua kukifanya ukikifanya kwa nia,bidii na maarifa lazima Watu watakusifu na kujifurahisha na kujivunia uwepo wako. Amua kufanya.
8. Kuwa Msafi.
Usafi wa roho na moyo. Kisha hisia na akili.Siô kila mwanamke au mwanaume ni wakulala naye. Huo ni uchafu. Usiwe mchafu. Usile vitu vichafu. Usikubali maneno na mawazo machafu yatawale akili yako. Roho yako usikubali ikatekwa na mapepo wachafu watakaoigeuza ni Jalala la kutupia uchafu wao. Mawazo ya ushoga, tamaa za uzinzi,kila Mwanamke mwenye msambwanda unataka kuruka naye. Kama vipi tafuta mke mwenye chura ili usizeeshe hisia zako ikafikia kipindi huoni maajabu kwa mwanamke utakayemuoa.
Oga mara moja kwa siku. Kama kuna ulazima paka mafuta kama haunywi maji mengi. Lakini kama ni mnywaji mzuri mafuta sio lazima sana.
9. Wapende wengine kama ujipendavyo hii itakusaidia kutovunja sheria za nchi na sheria za Mungu unayemuamini. Raha ni kuwa ukiwa kwenye jamii wàtu watakutambua vile utakavyojitambulisha.
Zingatia. Ukiwaza na kuwatendea Watu ubaya lazima ubaya utaambatana na wewe. Lakini ukitenda na kuwaza mema, mema yatakujia.
Hiyo itakufanya uishi kwa amani na utajikuta miaka nenda rudi huzeeki. Na kama nikuzeeka unazeeka polepole sana wakati wale waliorika lako wakizidi kuitwa Wazee na wakichakaa.
Kufikia hapa acha nipumzike.
Robèrt Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam