Ukitaka kuwa Milionea ndani ya Mwezi mmoja fanya hivi

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
3,401
Reaction score
1,610
Fikiria kufanya biashara ambayo utauza kitu ambacho kitakuwa na bei ndogo halafu uwafikie watu wengi kadri uwezavyo. Natoa mfano mdogo wa jinsi wa kuwa Milionea ndani ya mwezi mmoja.

Mfano:
Kuwa mbunifu kisha uje na idea ya kuuza utakachokuwa umekifikiria kwa bei ya shilingi 700 tu. Katika hiyo sh. 700, sh. 500 iwe ni gharama za uendeshaji kama kulipa wasaidizi wako, bills, rent na kodi (TRA) kisha hicho kitu uwauzie watu milioni moja tu kwa mwezi katika nchi hii yenye watu zaidi ya milioni 44.

Kwa maana hiyo itakuwa:
700(bidhaa)x1000000(watu)=700,000,000

Ukitoa sh.500 kwa kila hiyo bidhaa yako kama gharama ya uendeshaji utabakiwa na sh. 200,000,000(milioni mia mbili) ndani ya mwezi na kwa mwaka mmoja utakuwa na zaidi ya Bilioni moja.

SWALI:
Ni biashara gani gani hiyo? Hapo ndipo tunahitaji muda wa kufikiri kiubunifu zaidi.

Ukiweza kupata idea ya namna hiyo ndani ya mwezi mmoja unakuwa milionea,
MCHUNGUZI HURU
 
Babu samunge alipiga tshs 500 kila kikombe cha maji tuu sasa ana cruiser nyumba akaunti nmb
 
katika kila kikombe babu alikuwa anachukua sh. 100 tu, kkuna jinsi ambavyo alikuwa anazigawa sh. 400 ikiwa ni pamoja na kupeleka kanisani. hiyo ni kwa muujibu wa yeye
 
Kuwafikia watu hao 1m napo unahitaji kununua hiyo bidhaa lets say kwa 2,000 ili uuze kwa 2,700 so msingi wake nao ni 2billions!
 
mind kama zako ndizo zinafanya tuwe masikini.... kwanza unafikiria kuwa dalali wa kununua vitu kwa bei ndogo na kuuza kwa bei kubwa na haufikirii kuwa mzalishaji ili upate faida kubwa, thinking kama yako ndiyo umeua viwanda nchini kwetu.
 
  • Thanks
Reactions: GKM
Hahaha no shortcut way kwenye lyf jamani vijana tujifunze kutafuta pesa na co kuwaza kuwa watumwa wa wenye pesa.
 
Gharama ya uendeshaji kila bidhaa umesema iwe mia 5 sasa zidisha mia 5 mara bidhaa milioni jibu inakuja milioni mia tano. Kwa hiyo ili upate faida ya milioni mia 2 kwa mwezi unatakuwa uwe na msingi wa milioni mia tano. Conclusion utafiti wako unatekelezeka kwenye makaratasi, mtz yeyote aliye na mtaji chini ya milioni mia hawezi kutengeneza faida ya milioni mia 2 kwa mwezi never ever!!
 
Mkuu umemaliza..
 
Last edited by a moderator:
mind kama zako ndizo zinafanya tuwe masikini.... kwanza unafikiria kuwa dalali wa kununua vitu kwa bei ndogo na kuuza kwa bei kubwa na haufikirii kuwa mzalishaji ili upate faida kubwa, thinking kama yako ndiyo umeua viwanda nchini kwetu.

M.H kwenye bizness lazima kuwe na capital, kudalalia gari au nyumba inahitaji nayo msingi labda uwe dalali mtu wa kati.
 
Hiyo ni nadharia ambayo ni nzuri sana, na inafaa kwa mafundisho jinsi ya kuwapa moyo watu wafikiri inawezekana ukawa tajirii katka kipindi kifupi tu sasa nadharia kuiweka katika vitendo ndio changamoto kubwa Sanaa, ndio maana hata Mchunguzi Huru ameshindwa kuweka nadharia yake katika vitendo japokuwa ni nzuri sana. Cha Kujifunza hapa ni kwamba ukiwa mbunifu ukatumia jamii na wakati uliopo unaweza kufanya mambo makubwa sana yakakutoa katika umaskini, kiuchumi kuna principle unasema you can not make someone better off without making someone else worse off, sasa kwa kuwa rasilimali ni chache lazima kuwe na competition ya hizo rasilimali hivyo ni ubunifu ndio utakusaidia kutumia rasilimali chache kuzalisha Mali ghafi nyingi utakayoiuza sokoni upate fedha nyingi hii tunaiita minimize resources and maximize production to get maximum profit
 
Vitu vingine tunapeana moyo tu,

Swali linasema UKITAKA KUA MILLIONEA, so linamlenga mtu asie millionea. Sasa ni mtu yupi huyu asekua millionea mwenye uwezo wa kuingia gharama za Tshs 500 x Watu 1,000,000 = Tshs 500Mil???

Pili Population ya watu 1Mil ni labda robo ya wakazi wote wa Dsm including watoto. Otherwise kama ni watu wazima tu ndio walengwa basi inabidi ufike na mikoa mengine, ni bidhaa gani ya aina hii itakayokidhi hivi vigezo?

Tatu Hiyo kazi itakua na "pattent rights" ili wengine wasiige ubaki na "monopoly"?

Hii kitu iko theoretically zaidi kuliko practically aplicable!!
 
Gharama ya uendeshaji kila bidhaa umesema iwe mia 5 sasa zidisha mia 5 mara bidhaa milioni jibu inakuja milioni mia tano. Kwa hiyo ili upate faida ya milioni mia 2 kwa mwezi unatakuwa uwe na msingi wa milioni mia tano. Conclusion utafiti wako unatekelezeka kwenye makaratasi, mtz yeyote aliye na mtaji chini ya milioni mia hawezi kutengeneza faida ya milioni mia 2 kwa mwezi never ever!!

By the way huo mtaji tu unaohitajika wanao mamilionea tu, sasa awe milionea mara ngapi.
 
bidhaa iwe inahitajiko la muhimu ktk maisha ya binadamu na si ziada //nimeongezea //ni point muhimu sana !
 
Fikiria kufanya biashara ambayo utauza kitu ambacho kitakuwa na bei ndogo halafu uwafikie watu wengi kadri uwezavyo. Natoa mfano mdogo wa jinsi wa kuwa Milionea ndani ya mwezi mmoja.

Mfano:
Kuwa mbunifu kisha uje na idea ya kuuza utakachokuwa umekifikiria kwa bei ya shilingi 700 tu. Katika hiyo sh. 700, sh. 500 iwe ni gharama za uendeshaji kama kulipa wasaidizi wako, bills, rent na kodi (TRA) kisha hicho kitu uwauzie watu milioni moja tu kwa mwezi katika nchi hii yenye watu zaidi ya milioni 44.

Kwa maana hiyo itakuwa:
700(bidhaa)x1000000(watu)=700,000,000

Ukitoa sh.500 kwa kila hiyo bidhaa yako kama gharama ya uendeshaji utabakiwa na sh. 200,000,000(milioni mia mbili) ndani ya mwezi na kwa mwaka mmoja utakuwa na zaidi ya Bilioni moja.

SWALI:
Ni biashara gani gani hiyo? Hapo ndipo tunahitaji muda wa kufikiri kiubunifu zaidi.

Ukiweza kupata idea ya namna hiyo ndani ya mwezi mmoja unakuwa milionea,
MCHUNGUZI HURU

Ndugu yangu kila kitu kinawezekana kwa mfano angalia hapo ulipo nini hakipo kama una hisi upo na interest nakupa aidea ya biashara.Apple fruits zimekuwa tunda anasa sana hapa bongo wewe angalia eti apple fruits kwa sasa shilingi 500-700 ni kwa sababu source imekuwa moja south Africa.Mimi naweza kusuply apple kutoka ulaya hata container 10 kwa mwezi ambazo bei yake unaweza kuingiza sokoni kwa shilingi kama 200 kwa aple.Faida yake nini ...Apple sasa litakuwa si tunda la anasa kama tulivyo zoea apple sasa litaliwa mpaka mikoani .Na kama kweli unavyosema unaweza kusuply hata kwa watu milion moja basi ndugu yangu inawezekama

Kama una cash na upo serious basi semeni mimi nitatafuta muda kukaa chini na kufanya michanganyuo wote mpaka kukupeni exactly bei ya mwisho

siku njema
 
Gharama ya uendeshaji kila bidhaa umesema iwe mia 5 sasa zidisha mia 5 mara bidhaa milioni jibu inakuja milioni mia tano. Kwa hiyo ili upate faida ya milioni mia 2 kwa mwezi unatakuwa uwe na msingi wa milioni mia tano. Conclusion utafiti wako unatekelezeka kwenye makaratasi, mtz yeyote aliye na mtaji chini ya milioni mia hawezi kutengeneza faida ya milioni mia 2 kwa mwezi never ever!!

Yeye anaangalia faida tu amesahau kama kuna gharama za uendeshaji wa biashara husika.
 
Gharama ya uendeshaji kila bidhaa umesema iwe mia 5 sasa zidisha mia 5 mara bidhaa milioni jibu inakuja milioni mia tano. Kwa hiyo ili upate faida ya milioni mia 2 kwa mwezi unatakuwa uwe na msingi wa milioni mia tano. Conclusion utafiti wako unatekelezeka kwenye makaratasi, mtz yeyote aliye na mtaji chini ya milioni mia hawezi kutengeneza faida ya milioni mia 2 kwa mwezi never ever!!

Wewe heb chunga kauli zako, sikubaliani na hoja yako.... Wapo kibao mjini hapa na hata siku moja mtu hawez kuambia password yake ya mafanikio. Sema wewe ndio hujui wenzio wanafanyaje. Kama wewe ni indeed mtu wa mishe huwez kataa nachokuambia. Watu wanaishi kwa mbinu mjini hapa.
 
Back
Top Bottom