Wanasiasa wengi duniani wamesoma uchumi, sheria au politics.
Halikadhalika kuna nchi ambazo ni class societies zinataratibu zao za kutengeneza wanasiasa.
Mfano asilimia kubwa ya wanasiasa bunge la uingereza na senior civil servants traditional ni OxBridge (wamesoma Oxford na Cambridge) japo idadi yao inapungua miaka inavyooenda.
Oxford wana course yao maalum ya kutengeneza wanasiasa ndio wengi wanasomea P.P.E (Philosophy, Politics na Economics) hiyo ndio kina Rish Sunak, David Cameron, Jeremy Hunt, Rachel Reeves etc wamesoma.
Ukienda kwenye senior civil servants ya uingereza P.P.E wamejazana zaidi.
Lakini siasa kwa upana wake aihitaji kuwa na watu hao tu, inataka mtu mwenye interest na mambo ya jamii.
Halafu discipline nyingi zinafundisha interchangeable skills ambazo unaweza tumia kwenye siasa au hata hao wanasiasa kabla ya kufanya maamuzi inabidi wa-consult na watu wa discipline zingine.
Mfano muhasibu
Serikali inakopa inahitaji mtu anaefahamu debt management, interest risks za mikopo, currency risks, inflation risk. etc
Unataka kusaidia wananchi kuishi vizuri uzeeni unahitaji mtu mwenye uelewa wa personal finance ambae anakusaidia sera za watu ku-invest hela zao vizuri, kuwaingiza watu kwenye homeownership, kuelewa savings and investment ya hela zao.
Una miradi na taasisi za kibiashara unahitaji mtu anaelewa risk management on financial perspective.
Una tengeneza budget kila mwaka unahitaji mtu mwenye uelewa financial modelling na uelewa wa budget yenyewe inavyotengenezwa na kuelewa uhalisia wa vyanzo vyenyewe.
Una panga na kukusanya kodi unahitaji muhasibu ndio kasoma kodi in depth. Maafisa wa kodi nchi nyingi including TRA wanasoma kodi juu juu tu na kuendelezwa kwa course wanavyozidi kupewa majukumu. Ila muhasibu anaijua kodi kwa mapana yake. To name a few I can go and on.
Same thing ukienda kwa daktari, engineer na wengineo na wenyewe wana hoja zao kwanini wana umuhimu kwenye siasa.