Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
UKITAKA UFANIKIWE KWA JAMBO LOLOTE, TUMIA KANUNI YA KUSHAMBULIA SANA KULIKO KUZUIA SANA/KUPAKI BASI.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Ninafuraha nimerudi tena baada ya kupumzika kidogo katika kutoa miongozo kwa wale wenye kupenda maarifa na ufahamu.
Andiko hili lisomwe na watu wote na liwafae watu wote.
Niite Taikon Master, Mtibeli Kutoka Nyota ya Tibeli.
Tayari nilikueleza mambo ya muhimu katika harakati zako za Maisha. Maisha ni vita ya hiyari na wakati mwingine vita isiyo ya hiyari.
1. Unakumbuka nilikuambia umuhimu wa Kupata taarifa. Si unajua information is power.
2. Unakumbuka nilikuambia huwezi Kupata taarifa sahihi kama hutatumia Akili kujua mahali pa Kupata hizo taarifa, namna ya kuzipata, kuzichambua, na kisha kuzihifadhi na kuzitumia. Unakumbuka?
2. Unakumbuka nilikuambia hata kama kwenye maisha yako utaamua kuwa Mwongo, tapeli na dhulmati lakini huwezi kufanikiwa kama hutoujua UKWELI wa Mambo. Hivi unajua ukweli wa mambo ndio Taarifa zenyewe! Unaelewa?
3. Hivi unajua yakuwa ili ushindwe kwenye Jambo lolote itakupasa uwe na Adui?
Aidha ni adui wa kuonekana au kutokuonekana.
Hivi unajua adui lazima atoke Nje asiwe wewe?
Ukiona adui anatoka nafsini mwako ujue kuna adui wa nje alimweka. Unalijua Hilo?
4. Elewa, Adui mahiri na ambaye atakushinda kirahisi ni Yule aliyetumia Mbinu ya kumuingiza adui nafsini mwako. Yaani wewe unajigeukia kujidhuru mwenyewe.
Elewa, unajua kuwa Mwili hauwezi kujidhuru au wewe hauwezi kujidhuru.
Ikitokea Mwili umejidhuru, kimedani za kivita tunasema adui ka-implant kirusi kwenye mwili wako ili ujidhuru.
5. Unakumbuka nilikuambia ili uwe na Mbinu na Mbinu zako ziwe na ufanisi dhidi ya adui zako lazima uwe na taarifa za msingi na za mapema kumhusu adui yako?
6. Labda hujui, Kitu pekee ambacho kina thamani kwa adui yako ni Kupata taarifa zako. Na kitu pekee cha thamani ambacho adui yako anacho ni kujua taarifa zake.
Aaanh! Taikon Master unazungumzia mambo gani? Hatutaki mambo marefu Sisi.
Sawa! Nimewasikia.
Katika Kanuni za kivita, au Mapambano kuna Kushambulia na kujilinda. (attacks and Defense)
Kushambulia kuna kanuni zake na kujilinda kuna Kanuni zake. Lakini vyovyote iwavyo mambo hayo mawili yote yanategemea taarifa za kiintelejenia ulizonazo.
Kwenye Maisha kama zilivyovita vingine, kuna mambo lazima uyaelewe. Mambo hayo ni kama ifuatavyo;
1. Kuna mahitaji au Rasilimali ambazo unazihitaji na utakazozihitaji.
2. Kuna Vihatarishi
3. Kuna Viunzi au madaraja ya Kupata hizo rasilimali
4. Kuna Muda au Wakati.
Katika Kipindi cha Utafutaji usikae katika Defensive Mode (Hali ya kujilinda, KUPAKI Basi) Kipindi cha Utafutaji ni Kipindi ambacho unatakiwa ufunguke, ushambulie, (Attacks Mode)
Kwenye vita ya Maisha ambapo ni Mchezo kama Squad game ambapo ili wewe uishi lazima mwingine afe. Au kwa Lugha ya kiuchumi, Ili wewe upate lazima mwingine akose.
Unaweza ukaniuliza haiwezekani kugawana?
Hapo nitakucheka Sana!
Haiwezekani kugawana kwa Sababu, ninyi ni watu wawili tofauti, kila mtu anamhitaji yake, maono yake, ndoto zake, mitazamo yake, mipango yake, familia yake.
Ikitokea kwenye maisha mtu akakuambia Tugawane Rasilimali hapo kuna mambo mawili, Moja, ni aidha mtu huyo kwa sasa Hana uwezo wa kukukabili au kuna mambo nyeti uliyonayo anayoyategemea.
Taikon kama mwanafalsafsa na mwanasaikolojia, nitakuambia mpango huo usitishe au usikubali ikiwa umepewa option na mtu Kwa namna hiyo. Kwa sababu huko mbeleni mtaenda kugeukana. Kama sio ninyi basi watoto wenu.
Naendelea....
Katika Kanuni ya Kushambulia, kuna kanuni ndogo nitakayokupa ambayo ni Kanuni za kitibeli, isemayo; usikitafute kitu ukiwa na shida nacho bali kitafute ukiwa hauna shida nacho. Hiyo ni Sheria namba Moja ya vita katika maisha na mahali popote.
Sheria ya pili, ondoa upinzani wa kihatarishi kabla kihatarishi hicho hakijaanza kuwa Hatari.
Hizo ni Moja ya Sheria kuu za kitibeli zilizopo katika Kanuni ya Kushambulia.
Nitakupa Mfano;
1. Ikiwa unajua IPO siku Utahitaji MKE/Mume Basi ni vizuri zaidi na utafanya vizuri zaidi kama utamtafuta mapema Kipindi ukiwa haumhitaji kivile. Mfano, unajua Kabisa ukifikisha miaka 35 utaoa Basi ni vizuri utafute Mke mapema polepole ukiwa na utulivu tangu ukiwa na Miaka 25 -27
2. Ikiwa unajua Kabisa Utahitaji kuwa tajiri au kuwa na Pesa.
Itakupasa uanze mapema kuzitafuta pesa ukiwa hauna shida nazo. Lazima ujifunze kuzitafuta, kuzihifadhi, kuzizalisha n.k.
3. Ikiwa unajua IPO siku utataka kuwa na nyumba.
Lazima mapema ujiulize, kwa nini huna nyumba Muda huo, nini kinakuzuia kuwa na nyumba,
Nini ufanye uwe na nyumba,
Utajenga wapi hiyo nyumba,
Lini itatakiwa kuwa imekamilika.
Wahusika watakao kaa kwenye hiyo nyumba ni kina Nani?
Kisha, Anza mapema kuvunjavunja Mpango Mkubwa kuwa mdogo kwa kutimiza kidogo kidogo malengo yaliyomo kwenye nyumba.
Mfano, kidogokidogo, Nunua Kiwanja,
Kidogokidogo Anza Ujenzi rahisi kulingana na kipato chako.
Hiyo iende sambamba na kujenga wahusika watakaokaa kwenye hiyo nyumba.
Ni muhimu, wakati unajenga uwe na picha Halisi ya nyumba na maisha yatakayoendelea ndani ya hiyo nyumba. Hivyo wahusika ambao ni Mke/Mume lazima nao uwaandae sambamba na Ujenzi unavyoendelea.
Ili ukimaliza wahusika uwe tayari unawajua watakaokaa kwenye nyumba yako.
4. Ikiwa unajua IPO siku utazaa watoto lazima ujiandae na kufanya mambo kwa mapema zaidi ili kujiweka katika nafasi nzuri.
Kumbuka harakaharaka haina Baraka, na hii kauli inahusu wale wasio na taarifa za kutosha. Kwamba usifanye Jambo bila kujiridhisha.
Kanuni ya pili ya ondoa kihatarishi kabla kihatarishi hicho hakijaanza kuwa Hatari.
Inatumika mapema zaidi katika harakati. Jambo lolote ambalo ukishalinusa kama ni kihatarishi andaa Mpango WA haraka wa kuliondoa Jambo hilo kabla Jambo hilo halijaanza kukuletea madhara.
Nitakupa Mfano,
Ikiwa upo kwenye uchumba au ndoa Changa alafu ukagundua mwenza wako anatabia hatarishi na Tabia hiyo inamfanya kuwa kihatarishi, muache mapema kabla hamjafika mbali.
Tabia hatarishi ambazo mwenza Akiwa nazo unatakiwa kumfuta kwenye circle yako;
1. Msaliti kuchepuka (Hasa kwa mwanamke) kwa mwanaume ni kama anatabia ya kuchepuka chepuka. Yaani kwa mwaka ana-cheat mara kwa mara. Huyo mfute. Lakini mwanaume kama ana-cheat mara Moja kwa mwaka au mbili huyo endelea naye.
Mwanamke aki-cheat mara Moja mfute.
2. Mshirikina au mchawi.
Mwenza yeyote ambaye anatabia za kishirikina huyo ni kihatarishi. Usisubiri mambo yaharibike ndio utafute suluhu. Muache siku hiyohiyo mara tuu utakapojua anatabia hizo.
Usitumie Muda wako wowote kumshauri au kushauriana naye Wala kuomba ushauri popote pale.
Au mwanamke au mwanaume. Akiwa mshirikina huyo ni kihatarishi. Ni bomu ambalo siku yoyote litalipuka. Sasa Sisi Watibeli hatusubiri vilipuke.
3. Ubinafsi Mkali
Mwanamke au mwanaume anayejifikiria mwenyewe kuliko ninyi au familia yenu mliyoianzisha au mnayotaka kuianzisha huyo ni kihatarishi. Fukuza mara Moja.
Mwanamke anayetaka kupewa zaidi huyo ni kihatarishi.
Watibeli tunafukuza
Mwanaume anayependelea na kutanguliza wazazi au ndugu zake kuliko wewe Mkewe huyo ni kihatarishi. Vunja ndoa hiyo mapema na Wala asitafute ushauri popote.
Halikadhalika na mwanamke anayetanguliza wazazi na ndugu zake kuliko wewe mumewe huyo hakufai. Fukuza mapema huko mbele mtaenda kuumizana pakubwa.
Kuna Ile mnaishi vizuri na Mkeo/Mumeo mara anakuja Mhusika mwingine kwenye familia yenu labda ni Houseboy au housegirl ambaye kwa Jinsi anavyoonekana anatamanika. Huyo ni kihatarishi. Msisubiri baadaye kulaumiana. Usisubiri Mkeo Alambwe ndio umlaumu wakati ulikuwa ma nafasi ya kumwondoa huyo mfanyakazi mapema.
Au usisubiri Mumeo amle huyo mfanyakazi wakati wewe kama Mke ulikuwa na uwezo wa kumtoa huyo housegirl au mfanyakazi mapema. Usisubiri kulaumu au kukita. Chukua maamuzi mapema
Kwenye siasa au utawala, mtu yeyote ambaye unamuona ni kihatarishi mbele yako hata kama ni mdogo vipi usisubiri awe Mkubwa. Mdhibiti mapema.
Upo Ofisini, katika chunguzi zako umegundua Mmoja wa wafanyakazi wenu anatabia za Fitna, majungu. Huyo ni threats(kihatarishi) kwako. Panga Mpango wa kukabiliana naye. Mfuteni.
Wanasema mmalize kabla hajakumaliza.
Mimi acha nipumzike sasa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam