Ukitenda Mema Unajitendea Mwenyewe na Ukitenda Mabaya Unajitendea Mwenyewe

Ukitenda Mema Unajitendea Mwenyewe na Ukitenda Mabaya Unajitendea Mwenyewe

La Quica

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2017
Posts
1,009
Reaction score
2,315
Palikuwa na mtu mmoja kichaa katika kijiji fulani. Basi huyo mtu likuwa akipita na kelele sana kila siku akipiga kelele alikuwa anasema maneno haya "Ukitenda mema unajitendea mwenyewe na ukitenda mabaya unajitendea mwenyeweeeee".
Hayo ndo yalikuwa maneno yake katika mizunguko yake yote, akipata njaa hupita majumbani mwa watu kuomba chakula, kisha huendelea na safari zake.
Watoto wa kijiji kile walimzoea sana na walipenda hata kumtania na kucheza naye hata wakampa jina la "Ukitenda mema umejitendea mwenyewe..." kutokana na yeye kupenda kutamka hivyo.
Basi, palitokea mama mmoja katika kijiji hicho ambaye alikuwa hapendezwi kabisa na kichaa huyo, hivyo alipanga kumuua kwa kumpatia mkate[emoji506] wenye sumu kwani mara kwa mara kichaa huyo alipenda kwenda kwake kuchukua chakula.
Sikumoja, kichaa na kelele zake kama kawaida akafika kwenye ile nyumba ya yule mama akaomba chakula. Yule mama akachukua mikate[emoji506] akaweka sumu akampa, yule kichaa akaondoka zake huku mikate mkononi; mwanamke akaamini siku hiyo ilikuwa ndo hatima ya kichaa huyo.
Kichaa alichukua mikate alopewa na yule mama kisha akaondoka ili badae ale. Lakini njiani akakutana na watoto wa yule mama wanatoka shule; wakaanza kumchezea na kumtania kama kawaida yao. Na kwa sababu walikuwa na njaa, walipomuona ameshikiria mikate, wakamuomba ili wale, kichaa akawapa ile mikate wakala, yeye akaendelea na safari zake.
Watoto kufika nyumbani wakaanza kulalamika tumbo, tumbo, tumbo mama yao akawauliza, "Mmekula nini shuleni?" Wakamwambia, "Hatujala chochote Ila tulikutana na Ukitenda mema umejitendea mwenyewe... Tulikuwa na njaa tukamuomba mikate akatupatia tukaila",
"Daaa, kichaa kaniulia wanangu, mikate ilikuwa na sumu ileee". Mama akaweka mikono kichwani akaanguka, akazimia baada yakuzinduka hospitalini akakuta taarifa kwamba watoto wake wameshakufa wote kwa mkupuo.
_____[emoji320][emoji326][emoji320]_____
Mpendwa, bila shaka tumejifunza kitu katika kisa hicho
Ni hakika kabisa, tukitenda mema tunajitendea wenyewe, tukitenda mabaya tunajitendea wenyewe.
Hata maandiko yanasema,
"...yoyote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo..."
Mathayo 7:12

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni hakika kabisa, tukitenda mema tunajitendea wenyewe, tukitenda mabaya tunajitendea wenyewe.
 
Huyo kichaa anayegawa chakula chake, atakua alishapona siyo kichaa...

Kheri ilivyo kua story kwa sababu... kiuhalisia hakuna mtu anayeweza pokea chakula toka kwa kichaa hata watoto pia...


Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom