Ukitenda wema leo hii, wema huo unaweza usikulipe wewe ila ukawalipa watoto au wajukuu zako

alafu malipo ya wema huja wakat ambao ni mwafaka kabisa

nakumbuka tukiwa wadogo baba alikua anawasaidia sana wapita njia, so baada ya mda akatimuliwa kazi akabaki home muda mrefu bila ajira, mambo yakawa si mambo bt chakushangaza katika huo wakat mgumu mmoja wa alowasaidia alikuja home akiwa mambo safi anamtafta mzee ajili yakutoa shukrani.

alitoa then mzee akamsimulia kilichomsibu yule bwana akamtafutia kazi mzee maisha yakaendelea, baba akatufunza daima tusichoke kusaidia pale tunapoweza coz kufanya hivo kuna manufaa makubwa ndani yake
 

Dogo umeandika vizuri....ni wazi hiki kiss ni Cha kweli...hongera
 
Daima kwenye maisha, kama upo katika position ya kumsaidia mtu juu jambo lolote na halina athari kwako fanya hivyo haraka!
Miaka 8 iliyopita nilimsaidia dogo mmoja aliekua na maisha magumu shuleni kwa mahitaji yake kwa kuguswa tu na hali yake nikiwa kama mwalimu wake. Miaka kadhaa mbele dogo akafaikiwa kuajiriwa kwenye chuo flan hapa nchini baada ya ya kufanya vzr Bachelor yake, kipindi chote alinichukulia kama brother na akiendelea kunipa updates za hatua zake kimasomo, nami nikajiendeleza na kufanya masters. Dogo akapata SCHOLARSHIP na kwenda kufanya shahada ya pili nje....nami nlikuja muajiriwa chuo kimoja cha private na kuanza kazi. Siku moja nafungua email, nakuta amenitumia forms za scholarship, akisisitza bro jaribu kuomba hizo kuna jamaa angu amenitumia.....mzee nikajipinda, nikatuma..nimeshtuka may 13 mwaka jana nafungua email yangu, dah alhamndullilah, nimepata full scholarship ya PhD, sasa nakula mema ya nchi. Unapoweza kumsaidia mtu fanya hivyo, it pays a lot! Nimejifunza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…