star health talks
Member
- Apr 28, 2017
- 37
- 88
Habari ndugu zangu, katika pita pita za mahangaiko ya hapa na pale, nimebahatika kupita mikoa mbali mbali hapa Nchini kwetu Tanzania.
Mwaka juzi nikajikuta nimetua kwenye mkoa wa Wanyamwezi-Tabora, pamoja na sifa na changamoto kedekede nilizosimuliwa kuhusu mkoa huu jambo la kwanza lililonishangaza ni uwepo wa dawati la ukatiri wa jinsia katika stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani na wilayani mkoani hapo.
Ni jambo ambalo binafsi sikuwahi kulitegemea au kulishuhudia katika mikoa mingine niliyotembelea, zaidi nilikuwa nimezoea kuona dawati la jinsia katika baadhi ya vituo vya polisi.
Kutokana na nature ya kazi yangu, nimejikuta nikihuduhia wahanga wa matukio ya ukatili wa kijinsia nikiwa mkoani hapo Tabora. Idadi ya watu ninaokutana nao wakiwa wamefanyiwa ukatili wa kijinsia ni kubwa sana! Kwa siku huwezi kukosa mtu mmoja au zaidi mwenye changamoto ya kufanyiwa ukatili wa kijinsia.
Wahanga wakubwa ni watoto wa kiume wenye umri mdogo, hawa mara nyingi wanakuja wakiwa na tuhuma za kulawitiwa au kunusurikaa kulawitiwa na vijana wenzao au watu wazima.
Kundli la pili ni la watoto wakike wenye umri mdogo, hawa wanakuja wakiwa na tuhuma za kubakwa au kujaribu kubakwa na watu wazima, kwenye kundi hili nliwahi binafsi kukutana na mtoto wa kike mwenye umri wa miezi mitano aliyekuja na mzazi wake akiwatuhumu vijana anaohishi nao kumbaka mwanae!
Kundli la tatu hili ni la mabinti wa umri wa kati hasa wanavyuo au wanawake wa ‘mjini’ hawa mara nyingi kwa uchunguzi wangu binafsi, wasiporidhishwa na makubaliano au ujira kutoka kwa mwanaume waliyefanya nae ngono, huwageuka hao wanaume na kuja na kisingizio kuwa wamebakwa.
Haya matukio ni mengi sana mkoani Tabora, binafsi nimejaribu kujiuliza ni sababu zipi zinazopelekea ukithiri wa tabia hizi zisizofaa hapo mkoani Tabora.
Mojawapo nliwaza inaweza kuwa ukosefu elimu au elimu duni kwa wakazi wengi wa mkoa huo, maana katika kupitia takwimu za kitaifa, mkoa wa Tabora ni mkoa unaoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wasiojua kusoma na kuandika.
Pili inaweza kuwa ukithiri wa imani za kishirikina katika mkoa huu, maana wakazi wake wengi wanaimani za kishirikina sana.
Nadhani wote tutakuwa mashahidi wa taarifa za kuogofya na za matukio ya ajabu zinazotrend kwenye mitandao ya kijamii kuhusu haya matukio yanayotokea mkoani hapo, ila nafikiri ni idadi ndogo sana ya matukio yanaripotiwa. Hivyo tatizo ni kubwa sana.
Kiufupi Jitihada za ziada zinahitajika sana kupambana na ukatili wa kijinsia katika huo mkoa.