Ukitoa namba ya simu na usipotafutwa potezea; amekuepusha kwenye matumizi ya ovyo

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Wengi tunajua mahusiano ni gharama, hasa kwa upande wa wanaume. Kutumia maelfu, milioni n.k ni kitu cha kawaida kwenye mahusiano.

Mbaya zaidi, ufujaji wa hizo fedha hauendani na uingiaji wa hizo fedha katika akaunti yako. Utokaji unakuwa ni mkubwa sana kuliko uingiaji.

Tunajua ni hisia pamoja na matamanio, ndio yanayotufanya kuingia kwenye mahusiano na mtu fulani.

Wengi, huwa tukivutiwa na wadada, huwa tunawaomba tubadilishane nao namba za simu.

Sasa, baada ya kubadilishana namba za simu, kinachofuata ni mawasiliano.

Utatakiwa umpigie mara moja tu, baada ya hapo mpatie nafasi, yeye ndio awe anakutafuta.

Kukutafuta kwake, ni ishara ya kukuonyesha wewe, umekubalika vipi katika nafsi yake.

Ukienda tofauti na hapo, jiandae kulizwa.
 
Wanachokosea Sana vijana mpaka hawapigiwi simu Ni wanakurupuka sana kuchukua/kutoa namba bila kufuata utaratibu.

Ujue Kuna hatua muhimu Sana zinatakiwa zifuatwe ili hata ukimpa mwanamke namba, yeye mwenyewe awe na shauku kubwa ya kukutafuta wewe.

Na sio wewe umtafute yeye

VIJANA SIJUI MNAKWAMA WAPI[emoji848]
 
Matumizi ya ovyo inategemea Ni mwanamke wa viwango gan unafukuzia na wee mwnyw uko serious Kias gan.

Kuna mwanamke ukiwa nae unastuka kumkucha umebaki na elf 2 mfukoni na Wala hujutii[emoji4]
[emoji3][emoji3][emoji3]aisee
 
Wengi tunajua mahusiano ni gharama, hasa kwa upande wa wanaume. Kutumia maelfu, milioni n.k ni kitu cha kawaida kwenye mahusiano.

Mbaya zaidi, ufujaji wa hizo fedha hauendani na uingiaji wa hizo fedha katika akaunti yako. Utokaji unakuwa ni mkubwa sana kuliko uingiaji.

Tunajua ni hisia pamoja na matamanio, ndio yanayotufanya kuingia kwenye mahusiano na mtu fulani.

Wengi, huwa tukivutiwa na wadada, huwa tunawaomba tubadilishane nao namba za simu.

Sasa, baada ya kubadilishana namba za simu, kinachofuata ni mawasiliano.

Utatakiwa umpigie mara moja tu, baada ya hapo mpatie nafasi, yeye ndio awe anakutafuta.

Kukutafuta kwake, ni ishara ya kukuonyesha wewe, umekubalika vipi katika nafsi yake.

Ukienda tofauti na hapo, jiandae kulizwa.
Sababu ya umaskini hii. Unajikngezea gharama za bure tu.

Husiana na mtu mtakayerdhishana, na kugawana gharama. Sio mzigo mzito, kila ukiwaza aidha unapata hofu (unapigiwa) au unapata hofu ya kufilisiwa.

Yaani unakuta mtu anataka mtoke kula bata kila week end, na ukimbadilishia mtoko uwe wa jambo jinhine ananuna. Na ili awe sawa umpe tena zawadi n.k Haya sio mapenzi bali mateso
 
Ujue we huwa ni mtu mmoja amaizing sana mtraaamu yani...sema una vichembe chembe vya ubahili vinavoichafua CV yako 😁
Hata mimi nimemshangaa jamaa,yani utoe namba kwa pisi kali afu usitafutwe ushukuru!!! mwaka jana kuna mtoto wa kizungu nimekutana naye Hotelini nikampa namba hajanitafuta mpaka leo
hii inaniuma sana
 
Amekuepusha na changamoto, si ajabu angekuibia figo
 
Back
Top Bottom