Ukitoa posa unatakiwa kukaa muda gani ndio utoe mahari?

Kwani hajakwambia watakuja lini?

Huwa wanasema, ili mjiandae..

Kila la heri, Mungu akuongoze
 
Kwani ukileta posa ndio wanapanga na mahari siku hiyo hiyo au
Ukitoa posa,, kwanza kabisa kabla ya yote unatakiwa kuandika barua ya kishika uchumba[nitaweka mfano wake] ndani ya barua hiyo ndiyo utaweka kiasi kidogo Cha pesa ya kishika uchumba kisha utatafuta mtu wa heshima akupelekee barua yako. Haijalishi ulishampanga binti yao au laa kinachomata ni YUPI? Kisha watatoa muda wa kuendea majibu ya ombi lako.

Kisha Kwa barua yako wazazi wa binti wataitana kikao kukujadili hapo sasa na wewe unakuwa unafunga ukiomba mambo yako yaende poa si unajua tena kitu 'ombi' halina jibu moja.

Endapo mambo yakienda sawa basi utajulishwa kuwa barua yako imepokelewa ndipo mtapanga siku ya kukutana kwao kwa ajili ya kupanga mahali (posa).

Baada ya hapo ndio mipango mingine ya harusi au ndoa inafata.




MAGUFULI4LIFE.
 

Kiasi gani huwekwa kwenye posa
 
Kiasi gani huwekwa kwenye posa
Posa ni hela ya kumtoa binti kwao (mahali) hii hufikiwa makubaliano Kwa pande zote mbili, ila nadhani unamaanisha kishika uchumba.

Hii itatokana na wewe mwenyewe kwa mapenzi yako may be elf 20,30, au hata 50 kama mfuko utaruhusu.

Sema kingine hapa Kuna familia huwa na mila zao kuanzia barua unaweza ukaambiwa chukua barua yako nenda kaifunge kwenye kitambaa kipya cheupe au familia zingine zikishagundua ni barua ya kuchumbia unaambiwa ndani ya bahasha kaweke nafaka za chakula aidha ulezi,mtama na vitu kama hivyo ndio kisha urudie kuipeleka.




MAGUFULI4LIFE.
 
This is Africa brother
 

Posa inaweza kuzidi elfu 50

Na utaratibu upoje anaeleta posa ndio anatoa hela ya chakula kwa binti kwa maandalizi ya uletaji posa ikiwa ni wao kula siku hiyo
Namaanisha siku hiyo ya posa hela ya msosi anatoa muhusika yaani mletaji posa
 
Posa inaweza kuzidi elfu 50

Na utaratibu upoje anaeleta posa ndio anatoa hela ya chakula kwa binti kwa maandalizi ya uletaji posa ikiwa ni wao kula siku hiyo
Namaanisha siku hiyo ya posa hela ya msosi anatoa muhusika yaani mletaji posa
Mchumbiaji ni mgeni tu kama wageni wengine hivyo familia ya binti ndio itahusika na zoezi zima la kukarim ugeni.

Yaani barua ya kishika uchumba unaweza usiweke hata sh.mia na bado ukawa hujakosea kitu kumbuka barua yenyewe ni kishika uchumba tosha. Huwa inawekwa hela kidogo kunogesha tu ujumbe.


MAGUFULI4LIFE.
 
Kuna mtu kanisubirisha miezi 5 nataka nirudishe posa yake akiwa tayari aanze upya
Muulize mwenzako msipende jiangalia nyie tu... Aanze upya kana kwamba wewe humuhitaji mwenzio?

Kaonyesha nia kwann usionyeshe njia na wewe,huwezi jua huko mambo yamekwama,wewe huku umekaa tu miguu juu unasuburi Mume arudi.

Sio sawa,Ukirudsha Posa Huolewi tena ni kujichuria tu ila kwa hii case yako inaonyesha Hujapenda wewe na uko tayari kuachana na jamaa at anytime yani umpate sawa usimpate Sawa, Sio mapenzi hayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…