Ukitoa posa unatakiwa kukaa muda gani ndio utoe mahari?

Dah wakuu na mimi imenikuta scenario iyo iyo kuna mchumba nimempata yupo tanga sasa kanambia mahari ni 1.5m nikamwambia why pesa iyo ndo akanipanga kuwa 500k yake,500k mama ake na 500k baba ake sasa sijui amekaririshwa vibaya kuwa mimi nina pesa kisa na kajumba ka kuanzia maisha.Juzi ananiambia kuwa alishatolewa barua mwezi wa 3 na mahari mwezi wa nane yani kishika uchumba shilingi laki 6.Amenambia kwamba nipeleke mahari ili familia yake warudishe iyo laki 6 kwa mposaji wa mwanzo anasema hakumpenda je wakuu mnalionaje ilo?
 
Twende kwenye mfano wa barua sasa


Karumekenge Mpendashepu
0762xxxxxx
Mkoa wangu.
17/11/2023.

Kwa wazazi wa Ms Eyes.

Yah:OMBI LA KUZALIWA KUPITIA MLANGO WAKO.

Tafadhali husika na mada tajwa hapo juu, mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 32 ninaishi Buza Kwa mparange.

Bila kushawishiwa na mtu na nikiwa na akili zangu timamu ninaomba kuzaliwa watoto kupitia binti yenu Mis Eyes.

Endapo ombi langu litakubaliwa, Kwa barua hii ninamchumbia binti yenu Ms Eyes.

Mimi,
Karumekenge Mpendashepu.




[Unaweza ukanunua marashi mazuri ukaipaka barua yako].





MAGUFULI4LIFE.
 
I
Ilikuwaje ukapanga mahali na yeye wakati wazazi wake wapo?




MAGUFULI4LIFE.
 
Turudi kwenye mada kuu.

Mtu akishachumbia na akakubaliwa lakini kiwango Cha mahali kilichokubaliwa pande zote kikamshinda kukipata basi busara za wazazi hutumika ikiwa ni pamoja na kulegeza masharti ili vijana wao wakaanze maisha yao.

Endapo mahali ikamshimda mwanaume na kwa bahati nzuri mchumba wake akawa yupo vizuri si mbaya kumkopesha namaanisha kumkopesha mume wake mtarajiwa ili kumsaidia jambo lao lipite.

Endapo mahali ikamshimda mwanaume, na wazazi wa binti wamekaza na kwakuwa anania ya dhati na mtoto wa watu basi sio mbaya kuonesha umafia wako kumtorosha usiku na kuondoka naye ilimradi tu kesho yake ipelekwe taarifa kuwa msimtafute binti yenu ninaye kwangu.

Endapo mwanaume akashindwa kuendelea na hatua za ndoa Kwa kupuuza tu na ikiwa tayari alishachumbia na kukubaliwa,basi ajue amefanya kosa la udharirishaji wa kijinsia na atahukumiwa Kwa mujibu wa sheria. (SOSPA)

Hivyo,muda si kitu ila kutoa taarifa mapema ndio jambo jema na la maana mnapokuwa katika hatua hiyo.

Mwanzo nilisema kufunga na kuomba ili mambo yaende vizuri,haya maneno siyo madogo, vijicho vya watu navyo vinapambana kuvuruga mipangilio ya watu.




MAGUFULI4LIFE.
 
Sikupanga nae huo ndo utaratibu wao kwa maana alinambia kulikuwa na mposaji wa kwanza aliambiwa 1.5m akashindwa.
Inshu ilikuwa ndogo tu, mngejadiliana kwanza na wanaoenda kukusaidia kupanga mahali kwamba nyie mwisho wenu kabisa itakuwa shilingi ngapi zaidi ya hapo mngetangaza kushindwa kutokana na ukubwa wa mahali.



MAGUFULI4LIFE.
 
Nipeni range ya kutoa posa na mahali huwa vinachukua muda gani wapendwa.[emoji23][emoji23][emoji23]

Yaani ukitoa posa unakaa muda gani ndio utoe na mahari?
Ukitoa posa unatakiwa ukae miaka 4 ndio ulipe mahari ambayo bibie ameitumikia kwa hiyo miaka 4.
Yani shakewell b4 use,si nasema ukweli ndgu zangu
 
Unatapeliwa wewe...kuna vitu havilazmishwi kma kaletewa posa aende huko
 

Tulipanga akileta posa ni moja kwa moja hakuna kusubiri na nilishamueleza awali swala la mahari iweje asuesue
 

Yaani 1.5 ni ndogo wewe toa tu kama mnapendanaa
 

Mmh
 

Mwambie kila la Kheri.
Mtu kama hakupendi atakusumbua huko ndoani.
Kama mtu katoa mahari kwao hiyo kwako inakuhusu nini? Mwambie aache ujinga
 
Pangilia maneno haya upate sentensi yenye maana

Gunia mbuzi aliuziwa kwenye
1: Mbuzi aliuziwa kwenye gunia
2: Aliuziwa mbuzi kwenye gunia
3: Gunia aliuziwa mbuzi
4:kwenye gunia, mbuzi aliuziwa
5:Aliuziwa kwenye gunia mbuzi

MAJIBU YOTE NI SAHIHI, ILA KAZI KWAKO UCHAGUE JIBU SAHIHI ZAIDI
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…