Ni vizuri ukawasiliana na Dr aliyekufanyia TURP kwa ushauri zaidi. Kukosekana kwa chachu zinazotoka kwenye tezi la Prostate hazizuii mbegu (sperm cells) kukomaa, tatizo hapo kama laivyokueleza Omholo ni kuwa mbegu hizo zinarudi kwenda kwenye kibofu badala ya uke. Sio lazima ukiwa na retrograde ejaculation shahawa yote irudi, sometimes kuna kiasi kinapita na kuingia ukeni, kwa hiyo kuna possibility ya kutungisha mimba, ila kama alivyoshauri FF, kama imeshindikana...basi waweza fanya In-Vitro Fertilization (IVF). Siku hizi Bongo kuna IVF clinic pale Mikocheni opposite na Cloude Entertainment, baada ya kuonana na Dr aliyekufanyia operation unaweza pia kwenda pale kwa ushauri juu ya IVF kama ni muhimu sana kuzaa.