Ukituliza Akili Utagundua Kuna Makosa Tulikuwa Na Nafasi Ya Kuyaepuka Ikiwemo Haya Makosa Matatu

Ukituliza Akili Utagundua Kuna Makosa Tulikuwa Na Nafasi Ya Kuyaepuka Ikiwemo Haya Makosa Matatu

Dr. Zaganza

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
1,414
Reaction score
2,181









Niko Kilomita zaidi ya elf nane (8, 000 km) kutoka jiji langu la Dar lenye pilika nyingi zinazoninyima nafasi ya kuandika mawazo yangu yawe mchango kwa wengine wanaopambana kama mimi kuwa bora kiuchumi, kiafya, kiimani na kifamilia au kijamii kwa ujumla.

Nikiwa hapa Guangzhou (China) kusaka machombo ya bidhaa , hasa mitaa hii ya Xiaobei (Shaobei) yenye muingiliano wa mataifa mbali mbali , kabla ya kuja China nilikuwa na hofu ya vyakula labda hotel zetu kuna vyakula vya Kichina, Lakini ukifika hapa Xiaobei utakula migahawa ya Waturuki (Pilau, chips, chai maziwa kwa chapatti n.k) .

Kwa kweli ukiwa nje ya nchi unapata muda hotelini wa kutafakari na kuandika hiki na kile maana hapa hata simu zinazoingia ni za Whatsapp tu ,tena baada ya kuweka VPN.

Kwa umri wangu naotimiza miaka 40 muda wowote, natafakari tangu utoto mpaka nilipofikia, nagundua mwanadamu kuna makosa aina 2. Aina ya kwanza ni ubinadamu huwezi epuka mfano ukitukana ukiwa umelala, hapo huna lawama.

Lakini akili ikiwa imetulia nikakutana kichwa na makosa ambayo toka mwanzo kabla ya maamuzi

Hapa nimetafakari makosa matatu napenda share na wengine wakipata wasaa wayaepuke



Washauri kabla na baada ya ndoa

Kila mmoja ukimwambia mtaani kwake au mkoa Fulani alowahi kaa, ataje ndoa ya mfano alowahi kushuhudia wanandoa wanaishi kwa kuvumiliana mapungufu yao, wanatazama zaidi yale wanayofanana kuliko yale wanayopishana, Wanazungumzia mustakibari (future) yao kuliko wakati uliopita hasa nyakati mbaya , wanandoa walochagua kila mmoja kuwa mjinga kwa maslahi ya ndoa yao , naamini kila mtu anawajua, si moja, si mbili ndoa hizi zipo .

Kosa linalofanyika

Mtu akipata mchumba , anaenda kwa kundi la marafiki zake kuomba ushauri. Mwingine anakuja mtandaoni anafungua uzi, ‘Je mchumba huyu atanifaa’ au kama washaoana,changamoto moja tu ,anarudi mtandaoni ‘Je niendelee na mke/mume wangukafanya ABC’

Kosa ni kutojua nyuma ya kifaa cha internet iwe simu au computer ni nani anakushauri. Tafiti zinaonesha asilimia kubwa wanaopenda kushinda mitandaoni (ambao kazi zao za kipato hazihusiani na Internet) ni watu wenye msongo mkubwa. Na kipimo ni pale unapoona unaweza shambuliwa kwa matusi kwa kupost au kucomment kitu cha kawaida, tena mtukanaji akawa ni mtu msiyefahamiana.

Yes. Wana msongo wa ndoa,msongo wa maisha, msongo wa afya ,msongo wa uchumi. Vipi ukiwapelekea faili lako watoe hukumu (ushauri)?

Hakimu akiamka na hasira au msongo, wakuu wake hawampangii kesi kwanza,mpaka waone ka-relax. Wewe umeleta kesi kwa watu wengi wao hawajawahi kutatua hata ugomvi mdogo tu wa ndugu walopishana jambo dogo. Katazame status za waliokushauri , wao wamejiweka kundi la malaika hawakosei na kila rafiki na ndugu anayemzunguka ni snitch n.k

Bwana mmoja kila ikikaribia mwisho wa mwaka anawakumbusha rafiki zake na ndugu kwamba mshahara au kipato cha biashara cha December wakitunze ili ada za Januari zikaanza wasimuite Snitch maana simu za kuomba msaada zinamuelemea!! Kawashauri vyema.

Omba ushauri kwa mtu unayemjua kwa macho kwamba anachokushauri amekiishi, utaepuka makosa mengi.





Kuacha Kazi na Kuanza biashara

Biashara ina changamoto na faida zake. Biashara ikichanganya inakupa uhuru kama kusafiri ndani na nje ya nchi bila kuhitaji ruhusa ya mtu. Lakini biashara inahitaji uzoefu. Soma historia ya wafanyabiashara wakubwa kama Alhaji Aliko Dangote, walianza kutumwa na wajomba zao enzi hizo, baadaye wakawa wanachukuwa mitaji na kuanza biashara, nyingi zilikufa .Baadaye wakapata uzoefu wa biashara za kimataifa.

Binafsi nimekuzwa na familia ya wafanyabiashara kwa zaidi ya miaka 30 sasa nimeona panda shuka.



Kosa linalofanyika

Kukusanya mtaji na kuanza kwa pamoja. Utakuwa umeweka mayai yote kwenye kapu moja. Kapu Likikanyagwa?

Njia sahihi, tumia weekend kuanza kukusanya taarifa juu ya biashara unayopanga kufanya .

Ukishakuwa na taarifa za kutosha kama machimbo (utakaponunua kwa bei nafuu) na vichochoro au madocho (masokoau wateja wakuaminika), hapo chukua likizo yako mwezi mmoja kazini anza na kiasi kidogo cha majaribio. Utajua nini uongeze na kupunguza likizo ijayo na kuacha kazi itakuwa automatically baada ya kukua biashara na kushindwa kuhudhuria majukumu ya kazini ulikoajiriwa vyema.

Kosan i kuuliza mtandaoni usiowajua, waliokomaa kibiashra watakwambia acha kazi ,anza biashara. Walioko kazini watakuonya, utabaki njia panda.

Nikiri wazi , kwa uzoefu wangu mdogo, ukiacha kazi baadaye utatoboa biashara ILA kuna kipindi cha mpito ambacho wengi kinaacha mke akimbie (asiye mvumilivu), marafiki wapungue, wewe mwenyewe pia utajitilaumu kwa kucha kazi.

Je, kipindi hiki cha mpito umejiandaa nacho?





Kuamini uwepo wa Mungu au kutoamini


Binafsi naamini nuwepo wa Mungu na naamini tukifa tutafufuliwa na kulipwa mazuri tulofanya mshahara (thawabu ) na mabaya tulofanya kama hatujatubia kuna adhabu.

Niko na marafiki zangu kadhaa wao hawaamini habari za kufufuliwa ,kwamba tukifa habaari imeishia hapo. Kuna muda baada ya kuzozana sana upande upi uko sahihi tkaona tumualike mwalimu wa dini atusaidie.

Mwalimu akaja akasikiliza kila upande. Kisha akatupa sasa muelekeo wa kuepuka makosa yanayoepukika.

Akasema kama yeye atafanya utiifu wa Mungu kwa miaka 70, kasha baada ya kufa akakuta hamna habari ya kufufuliwa, atapata hasara ndogo tu kwamba kafanya utumishi bila malipo.

Upande wa pili akasema endapo yeye akaamua sasa anakula riba, anafanya kila dhuluma na maasi kwa miaka 70, baada ya kufa akakuta habari za kufufuliwa zipo kweli. Hapo hasara ya pili ni kubwa zaidi

Kufanya maandalizi ni moja ya njia za kuepuka makosa yanayoepukika.



Kumekucha sasa, kuanza muingia treni za chini wanaita Metro, kuenda machimbo mbali mbali ya Guangzhou. Kisha nitawaachia flight cargo ili ziwahi (siku 10 takribani kufika Tanzania) kisha nielekee Baiyun international Airport (CAN) kuwahi ndege za Emirate tayari kuanza safari kurudi nyumbani nikipitia Dubai .
 
Duh... Umeeleweka vizuri sana..
Sasa me nataka uniletee baby walker za watoto
 
una mada Jengeshi,tafakarishi,wezeshi Sana...nk..naomba nifahamu Huwa unakula vyakula gan vya kutunza Afya ya ubongo wako...kuweza kufanya yote hayo..
 
una mada Jengeshi,tafakarishi,wezeshi Sana...nk..naomba nifahamu Huwa unakula vyakula gan vya kutunza Afya ya ubongo wako...kuweza kufanya yote hayo..
Hamna kuu ni vyakula vya TZ, ugali kiasi, wali kiasi matunda na mboga mboga kwa wingi
 
Nauli ya ndege go and return ni sh.ngapi
milioni 3.5 nililipa (May 2023), Emirates nilitumia ili tulale Dubai kidogo maana safari ni ndefu bei zinabadilika .
 
Back
Top Bottom