Ukitumia internet vizuri kufanya utafiti wako binafsi utagundua Uchawi haupo. Hakuna mganga wala nabii atakayekutapeli. Wajinga ndio waliwao

MELEKAHE

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2023
Posts
1,340
Reaction score
5,588
Habari wadau

Binafsi nashangaa sana watu hasa wasomi wenye smartphone wanaoamini story za ushirikina zama hizi

Ukweli ni kwamba ukijipa muda wako kujifunza zaidi kuhusu cognitive science and psychology, Human psychology na Science of Emotion ilivyo. watajua ukweli mwingi sana wa ubongo wa binadamu unavyofanya kazi na unavyodanganyika

Watu wakijipa muda zaidi na kusoma kuhusu history za uchawi hasa msako wa wachawi (Witch Hunts in the Western World) kwenye karne zilizopita ulikuaje na kwa nini kilisababisha msako huo usitishwe. pia wakasoma kuhusu msako wa wachawi uliotokea marekani pia maarufu kama The Salem Witch Hunt na ilikuaje marekani wakaachana na misako hiyo pia, watajua ukweli kuhusu uchawi.

Kisha wakarudi kwenye youtube na kuangalia video za magic tricks zinavyofanya kazi. watajua waganga na wanaojifanya wachawi wanatumia mbinu gani kuhadaa watu.

Mfano kuna video nyingi za youtube za Sheikh Othman michael akishirikiana na Shehe Jafar kitwana ( mganga mstaafu) wakieleza kila kitu kuhusu uchawi na huku wakionesha na mifano ya jinsi waganga wa kienyeji na wachawi wanavyotapeli watu kwa kutumia Placebo effects na magic tricks. yaani ukizijua hizo hakuna mganga ataeweza kukudanganya hasa ukielewa mbinu zao na mazingaombwe yao.

Nashangaa sana kijana wa zama hizi kuamini ushirikina na kwenda kwa waganga wa kienyeji wakati elimu zinapatikana kwa urahisi sana.

Jamani kwenye internet tusiangalie tu kina mwijaku na diamond. tumieni internet kupata elimu na kuelewa jinsi ya kusolve changamoto zetu.

Your browser is not able to display this video.
 
Mazingaombwe unayaelezeaje?

mazingaombwe ni kiswahili cha neno la kiingereza magic tricks.

udsm tuki wanasema mazingaombwe ni kiini macho ambacho hufanywa haraka mno kiasi kwamba huwahadaa watazamaji kuwa yatokeayo ni ya kweli.

Oxford dictionary inasema magic tricks - A remarkable act carried out purportedly by magical means but actually by trickery or illusion
 
Pumbaa
 
Hakika nakuambia, amini usiamini, kila penye mafanikio hasa yale ya ghafla, ushirikina upo. Unakumbuka nabii Issa alipomtoa mtu mapepo kisha yakakimbila kwa nguruwe, moja kwa moja mpaka baharini?

Huo ndio uchawi ulioshuhudiwa na Yesu. Watu wanaishi kishirikina kwa siri na kuwahadaa watu! Acheni hizo!! Kuna mmoja alikataa kabisa mambo ya uchawi, akapigishwa chura tumboni, sauti ya chura ikawa inatoka tumboni, akaaguliwa na hao aliowadharau. Sasa hivi yupo makini na anaamini uchawi.
 
Kwanini wazungu waliacha witch hunting?


Gunduzi za kisayansi ndio sababu. magonjwa ambayo waliokuwa wanaamini yanasababishwa na uchawi, waligundua sababu zake kumbe ni za kisayansi.

Kadiri viwango vya elimu na kusoma na kuandika vilipoongezeka, watu walizidi kukosoa hali ya kuwinda wachawi na kuanza kutilia shaka uhalali wake. Elimu ndio ilileta mabadiliko katika mitazamo ya kiakili na kitamaduni. Rationalism zilianza kuchukua nafasi ya ushirikina na hofu, na kusababisha kupungua kwa imani katika uchawi na nguvu zisizo za kawaida.

Zaidi ya hayo, mifumo ya kisheria na mahakama katika Ulaya ilifanyiwa mageuzi ambayo yalifanya iwe vigumu zaidi kuwashtaki na kuwanyonga watu kwa madai ya uchawi. maana sheria mpya zilitaka hukumu ziendeshwe kwa kufata ushahidi unaonekana kwa macho, na sio kwa imani tena

serikali za ulaya ziliamua kuachana na sheria za Kanisa ( church laws) katika kuendesha nchi zao, sababu kanisa ndio lilikuwa na mchango mkubwa katika kuamini kuendeleza na kuendeleza uwindaji wa wachawi. maana biblia ilisema wachawi wauwawe, kumbuka zamani nchi za ulaya zilikuwa zinaendeshwa kwa kufata biblia na sheria za kanisa zinasemaje kama vile saudi arabia leo wanavyofata quran inasemaje katika kuendesha nchi yao.

Zaidi ya hayo, mabadiliko ya kiuchumi na kijamii, kama vile mabadiliko kutoka kwa ukabaila hadi ubepari, yalisababisha kuporomoka kwa miundo ya jadi ya jumuiya ambayo iliunga mkono mawazo ya kuwinda wachawi. Kadiri viwango vya elimu na kusoma na kuandika vilipoongezeka, watu walizidi kukosoa hali ya kuwinda wachawi na kuanza kutilia shaka uhalali wake.

Kwa ujumla, mchanganyiko wa mabadiliko ya kisayansi, kiakili, kisheria, kidini na kijamii ulichangia kuachana na uwindaji wa wachawi huko Ulaya na America
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…