Ukitumiwa ujumbe na Matapeli huwa unajibu nini?

Ukitumiwa ujumbe na Matapeli huwa unajibu nini?

nafuta tu meseji sijibu kitu.

2).na kuna wale ...wanaotuma ..mzee fulani bingwa wa kutibu kwa tiba za kienyeji(waganga wa kienyeji)

3) na kuna wale tunakopesha mpaka milion kadhaa ,NIDA yako tu mkopo ndani ya saa 24.

4) na kuna wale namba yako imeshinda kiasi cha

au kiasi cha shilingi kimeingizwa kwako
 
Kuna jamaa Alinipigia wale matapeli wanajifanya wanakupa Dili la hela nyingi, nikaongea nae vizuri tu japo nilishamshtukia, jamaa akanipanga weeee, akaniunganisha na matapeli wenzake kama watatu ivi mi nawachora tu, wakanipanga wewe mpaka mida ya jioni ndo ikabidi nimchane jamaa kua nilishamshtukia kuanzia mwanzo nilitaka tu kujua wanapigaje watu

Jamaa aliongea kwa uchungu sana "kaka kwanini umenipotezea siku nzima aisee, hizi ni kazi kama kazi zingine, kwanini hamheshimu kazi za watu, ungeniacha nitafute kichwa kingine?" Nilicheka balaa
 
Kuna wale wa sauti ukiwashitukia unakula matusi chapchap kisha wanapotea hewani huwapati. Nikishagundua ni tapeli nampa makavu fasta nakata simu asiniachie matusi
 
Nawajibu nimeshatuma umeiona, kuna jamaa alijichanganya akaniambia yeye ni baba mwenye nyumba wangu nimtumie kodi yake wakati mimi naishi kwangu sijapanga nilimchanganya huyo tapeli kwani nilimjibu nimetuma sasa akaanza kupiga kuuliza nimetuma kwenye namba ipi ? Nilimchanganya huyo tapeli alipokuja kustuka aliishia kutukana matusi kama yote
 
Back
Top Bottom