Kuna jamaa Alinipigia wale matapeli wanajifanya wanakupa Dili la hela nyingi, nikaongea nae vizuri tu japo nilishamshtukia, jamaa akanipanga weeee, akaniunganisha na matapeli wenzake kama watatu ivi mi nawachora tu, wakanipanga wewe mpaka mida ya jioni ndo ikabidi nimchane jamaa kua nilishamshtukia kuanzia mwanzo nilitaka tu kujua wanapigaje watu
Jamaa aliongea kwa uchungu sana "kaka kwanini umenipotezea siku nzima aisee, hizi ni kazi kama kazi zingine, kwanini hamheshimu kazi za watu, ungeniacha nitafute kichwa kingine?" Nilicheka balaa