Ukiugua sana unajikatia tamaa ya kuishi

ashomile

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Posts
2,739
Reaction score
2,697
Huwa inauma sana pale unapougua kwa muda mrefu bila kupata suluhu ya kinachokusumbua , inafika sehemu unawaza heri ufe tu ili upumzike , ili nafasi yako aichukue mwingine aendelee kuishi badala yako.
NIMESHANGAA TUUPELE TUDOGO TUDOGO TUMETOKA SHINGONI MWANGU HATA SIELEWI.

UGONJWA :NAUMWA KIFUA NI MUDA WA MIEZI 7 MPAKA SASA .

Mwanzoni nilikuwa nakohoa kikavu lkn badaa ya kuanza mazoezi ndani ya wiki moja nikitoa makohozi ni mazito sana . Kila mara ni mtu wa kutoa makohozi lakini leo nimeamkia mazoezi nikapiga kidogo kifua kikachemka nikashindwa .

KUMBUKA :NIMEFIKA HOSPITAL MBALI MBALI NAPEWA TIBA, LAKINI TIBA HAZISAIDII ZAIDI YA KUTULIZA TU .

Mpaka naingiwa na mawazo hizi ndoto za mauti au ndo yamekaribia !!
Nakemea nakemea baada ya muda yanarudi [emoji25][emoji25].

MUNGU ATUPE MWISHO UWE MWEMA KWETU SOTE :

DAWA NIMEWAHI PEWA KILA NIKIENDA HOSPITAL NI , SEDITON, CETRLIZEN,AMPLICOX,ALBENDAZOLE TU .. KILA.SEHEMU NINAYOENDA MPAKA HOSPITALI YA MKOA SHINYANGA .

IMEFIKA MAHALA NAWAZA NIKAFANYIWE X-RAY YA MAPAFU. ?? NINACHOOGOPA NI GHARAMA MAANA NAPITA KIPINDI KIGUMU SANA .
 
pole, nenda hospital kubwa na ufanyiwe uchunguzi zaidi. usikate tamaa, ukiwa bado una pumzi ndani yako.
 
pole, nenda hospital kubwa na ufanyiwe uchunguzi zaidi. usikate tamaa, ukiwa bado una pumzi ndani yako.
Asante sana wacha nifanye kazi kwa bidii ili niweke kiasi cha kunisaidia
 
Mbona dawa ulizopewa ni za kawaida sana tofauti na uzito wa ugonjwa wako kama unavyoelezea? Inawezekana unaenda hospitali ndogo ndogo sana ndio maana unaishia kupewa hizo dawa za allergies nk..hebu kuwa serious na tatizo lako nebda hospital kubwa zenye ma specialists wa magonjwa hayo utapata suluhu tu ndugu ..pia uache kuhofia gharama kwwnye uhai wako mwenyewe maana umesema unahofia sana gharama why?
 
Pole sana pima na UKIMWI, ili kama tayari, basi uanzishiwe dose
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…